Mbowe: Hatutompa muda Rais na hatukubali. Viongozi wa CHADEMA watakiwa kujiandaa kuanza mikutano nchi nzima

Mmmmhhhhhh, bagosha! Limagufuli walinywea nywee sasa kaja mwanamke wanaona itakuwa chee. Waache wajaribu wakishindwa tena wajinyonge kama Yuda Iskarioti.
 
Na aliyekuwa mkali amefikia wapi? Tumia akili.
Ni rahisi sana kupotezwa ukisimamia misingi, mbona hata huyo kwenye profile lako wwalimshoot mapema sana!!! Waoga wote ndio huishi miaka ya Mwinyi, heroes last a second, mfano Don Makavelli, Jesus Christ, Prophet Muhammad, Nesta Marley, Peter Tosh, Princess Diana, Adolf Hitler, Marcom X, Dr. Martin Luther King junior,..
 
Mkuu wasipoelewa hii kauli yako hawatamwelewa yeyote. Wewe ni Genius
 
Badala ya kujadili ujenzi wa madarasa na zahanati tumeanza tena u-basket mouth
Ujenzi wa madarasa na zahanati hauwezi kwenda concurrently na process za kuandaa Katiba yenye tija as well as mikutano?

Kuna shida gani kuruhusu watu wakutane kwa amani, wateme nyongo zao/madini yao then warudi kwao kulala? Enzi za Jakaya mbona iliwezekana na madarasa yakajengwa tu?

The guilty (and thieves) are always in constant fear.
 
Badala ya kujadili ujenzi wa madarasa na zahanati tumeanza tena u-basket mouth
Yaani Rais aache kushughulikia masuala ya muhimu ya nchi ahangaike na kina Mbowe!!.

JPM anasemwa vibaya na watu humu jukwaani baada ya kuitumia vyema katiba hii kwa kuwanyoosha watu wa aina hii.
 
Ngoja tuone kama mtaifanya hiyo mikutano kweli au mtaifanyia kwenye bafu za Segerea mkisimamiwa na Nyampala,mnampima mama imani mkizani yeye ni kamserereko sio🙄🙄
 
Kweli ccm wote ni wajinga sugu,Samia kasema kuhusu katiba avumiliwe.CHADEMA wamejibu hoja kwa kishindo.Inatakiwa maccm nao wajibu hoja siyokutumia polisi kujibu hoja za CHADEMA.Kutumia polisi kuzima hoja huo ni udikteta alio utumia shetani jiwe
 
kumbe ndio maaana hayati JPM aliamua kudili nao ipasavyo!
kumbe hawa jamaa ni wakorofi! hawana busara hata chembe.
wao nia yao ni kuvuruga vuruga na kutaka kuchelewesha maendeleo ya wanachi.
walianzaga kipindi cha JK, JK akwalegezea, wakadhani JPM angewalegezea kumbe aliwasoma watamchelewesha akawabana mbavu!
sasa wanaaanza tena kumbabaisha Mama yetu , ah! kwa fikra zao wanadhani utawala huu wa awamu ya 6 ni "kitonga" ah! wapi!haiwezekani,
hawa watu wamekosa uungwana na ustaarabu.
Chadema ni chama kisicho na nia njema na nchi yetu, ndio maana Mbowe kama mwenyekiti wa chama zaidi ya miaka 15 hata siku moja huwezi kumuona anashiriki kutatua kero za wananchi, huwezi kumuona anashiriki ktk maendeleo, yeye anaagalia masilahi yake binafsi na uchu wa madaraka basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
swala la msingi katiba ifuatwe ......kama ni haki yao kikatiba na wafanye
 
Ndo maana yake,,dunia haiko fair,ukijiweka front uwe tayari kwa lolote
 
Kweli ccm wote ni wajinga sugu,Samia kasema kuhusu katiba avumiliwe.CHADEMA wamejibu hoja kwa kishindo.Inatakiwa maccm nao wajibu hoja siyokutumia polisi kujibu hoja za CHADEMA.Kutumia polisi kuzima hoja huo ni udikteta alio utumia shetani jiwe
SSH ndiyo CCM kwanza. Aina haja kujibu wote.
 
Acheni Siasa za Maji taka, tuungane na Mhe.Rais Kujenga Nchi yetu! Hata Nchi zilizoendelea kama USA hawafanyi siasa kila siku! Aliposhinda Trump Democrats walitulia mpaka 2020 wakati wa uchaguzi, kashinda Biden,Republican wametulia mpaka 2024. Siasa zimehamia Bungeni, nyie mnataka tuandamane, hapana tujengeni Nchi. Mhe.Rais tupo pamoja tuchape kazi na kujenga Uchumi na Nchi yetu!
 
CDM wanarudi tena kwenye kosa kubwa walifanya wakati wa Magufuli, Kikwete aliwadekeza sana! Samia siyo Kikwete, kwa sasa mnachotaka kufanya ni kumtengeneza JPM out of Samia
 
Eti "hatukubali kupewa mda, watu wajiandae na mikutano ya hadhara vinginevyo tutakutana barabarani"

Kwahiyo ni lazima sasa.hiki ni kiburi.na wala sio siasa.

Hizi kauli na haya mashinikizo ya kibabe mbona hayakuthubutu kusemwa nyakati za magufuli?

Mimi ninaamini watz kama watz bado priorities zao ni Maji safi, barabara, ajira, elimu bora, afya,nk

Hizi huduma bado na ndio maana hata kwny chaguzi zetu tunapimwa na wananchi ni kwa namna gani tutakwenda kuzitatua changamoto hizi ili tupewe kura.

Manake IPO wazi.huwezi kwenda kakonko, ileje, rorya, mbinga,makete,kateshi,liwale,bahi wala ngara ukawaambia watu kwny kampeni strictly kuwa wewe mgombea x agenda kuu yako ni katiba na ukapewa kura.hupati kitu.

Hutapata kitu sababu hujameet mahitaji halisi yao.

Kwahiyo katiba as katiba mostly sio takwa la wengi.tusidanganyane.
Hata kama ni hitaji lao lakini si kipaumbele.
Kwasab katiba IPO.

Rais kasema kwasasa hata dili nalo.labda huko mbele.kubalini.

Si juzi tu hapa walisema Samia anaupiga Mpira mwingi.(pro chadema)
Leo wafuasi hawa wamemgeuka.
Wamegeuka kwasab mwenyekiti ameibuka na mpya.
Kumbe nimegundua hawa vijana wapo driven na mitizamo ya viongozi wao.

Wengine walishaanza na kumshushua kigogo wa tweet wakidai hajui anachokitaka.
(Maana kigogo hakuyumba kimisimamo toka awali)

Vijana sasa jisimamieni..Jana mmetoka kumsifu mama..kwa kupiga mpira mwingi leo mmegeuka kisa lisu/mbowe amebadili mtizamo

Namalizia kwa kusema kazi mojawapo ya serikali ni kutawala RAIA wanaotaka na wasiotaka hata wale ungovernable politicians.wanajulikana.
 
John Joseph alikuwa Duke kwelikweli. Ujinga huu asingevumilia kabisa.
 
Kuna kitu anakitafuta Ili apewe halafu akae kimya,

Si unajua Tena Ile ni investment ,

Halafu hii ni new administration.

Nadhani mtakua mmenielewa hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…