Mbowe: Hatutompa muda Rais na hatukubali. Viongozi wa CHADEMA watakiwa kujiandaa kuanza mikutano nchi nzima

Mbowe: Hatutompa muda Rais na hatukubali. Viongozi wa CHADEMA watakiwa kujiandaa kuanza mikutano nchi nzima

Dah...alikuwa ananiburudisha sana akikamata vijana wahalifu na kuwahoji😂😂😂
kijana mzuri mnene lakini mwizi huku anampiga piga mgongoni hahaha...
mimi nilikuwa napenda akitaja vifungu vya katiba "kifungu cha ine" halafu eti asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na kamanda dodoma..
 
kijana mzuri mnene lakini mwizi huku anampiga piga mgongoni hahaha...
mimi nilikuwa napenda akitaja vifungu vya katiba "kifungu cha ine" halafu eti asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na kamanda dodoma..
Hahahahahaha hapo kwenye kijana mzuri mnene 😂😂😂 mie ndio huwa sina mbavu huku anamgonga gonga bega!
 
Hahahahahaha hapo kwenye kijana mzuri mnene 😂😂😂 mie ndio huwa sina mbavu huku anamgonga gonga bega!
hahahahahaaaaa unakumbuka yule aliyemkuta na tattoo ya I LOVE YOU..
GILLES:hii ni nini wewe ni kabila gani..
GILESS:ni sanaa tu mkuu, mimi ni mndengereko..
GILLES:sanaa ya i love you?! wandengereko wanajua i love you!?....nadhani ndugu wana habari mnaona jinsi nguvu kazi inavyopotea..

hahahaaaa gilles alikuwa sio wa karne hii..
 
Hahahahhah Muroto ni funny sana yule mzee halafu anaonekana katili ila kimsingi ile ni mikwara tu nahisi watu wake wa karibu wanainjoy sana 😂😂😂...eti nahisi wanahabari mnaona nguvu kazi inavyopotea?
 
Hahahahhah Muroto ni funny sana yule mzee halafu anaonekana katili ila kimsingi ile ni mikwara tu nahisi watu wake wa karibu wanainjoy sana 😂😂😂...eti nahisi wanahabari mnaona nguvu kazi inavyopotea?
eeh eti kisa jamaa amechora tattoo ya i love you ndo nguvu kazi imepotea hahahaaha..
 
Tatizo wanasiasa wanatuvuruga hata wakati mwingine hawaeleweki, katiba iliyopo wanasema haifuatwi na viongozi! Sasa wameacha kuhimiza viongozi wa serikali wafuate hii iliyopo ili tuone Kama ikifuatwa ipasavyo itakuwa na mapungufu, Sasa wanacheza mziki wa katiba mpya? Hii iliyopo imefuatwa ipasavyo!????
Kutofuatwa katiba ya sasa ni kwa sababu ya mapungufu yake pia!
 
Baada ya Rais kusema kuwa anataka apewe muda ili ajenge uchumi kwanza na mambo ya katiba na mikutano ya hadahara itafata baadae.

Mh Mbowe leo amesema wazi kuwa hawatompa muda Rais samia na hawatakubali bali watafanya mikutano ya hadhara na watadai katiba kwa njia yeyote ile inayofaa na ikiwezekna wataingia barabarani kuidai katiba... na kwa sasa swala la katiba ni lazima watake wasitake ni lazima katiba ipatikane.

“Ombi la Rais Sami kwamba tumpe muda kuhusu suala la katiba, hatupo tayari kumpa muda na natoa agizo kwa Viongozi Nchi nzima wajiandae kwa mikutano ya hadhara siku ambayo tutaitangaza".

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza leo kwenye Kongamano la BAVICHA Tabata, DSM.

"Tutaidai Katiba mpya asubuhi, mchana hadi usiku. Kama wanataka tukae mezani, turidhie. Kama wasiporidhia, tutakutana barabarani. Hatutaridhia kushiriki Uchaguzi wowote bila kuwa na Katiba mpya au Tume Huru ya Uchaguzi.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza leo kwenye Kongamano la BAVICHA Tabata, DSM.

Kwani mbona Rais anatambua madai yao. Shida wao wanamsukuma afanye kwa muda wanaotaka wao. Mwisho wa siku watashindwa kwenda pamoja kwa sababu Rais ni taasisi isiyo pangiwa na vyama vya siasa.
 
"Huyu mnayemuona ndiye Rais wa Tanzania.... mwenye maumbile ya kike...."
 
Na tabia ya kujiita Makamanda muache maana Kamanda huwa hakimbii frontline sasa kidogo tuu huyu kakimbilia Chechinia, Cambodia mara Canada hamstahili kuwa makamanda.
 
Kwa sababu awapo bunge sasa. Wanatafuta fedha za kujiikimu kwenye bunge la katiba. Hii katiba siyo mbaya sana kama wanavyosema, sana sana kutaka ukubwa tu. Na kugawa nchi kama alivyotaka wa kujadili kwenye katiba pendekezo ya Warioba. Wanashindwa kukumbuka CCM ni wengi kuliko wao kwenye mahamuzi kokote kule. Maoni yangu, wazingumuze na wana CCM hili kupata muhafaka, hili CCM ndiyo wapendekeze wao kujadili kuhusi marekebisho au kubadili katiba. Kujifanya Wanaharakati ampati tu. Mtaishia jela tu
 
haya mambo kipindi cha awamu ya tano yalisahauliwa kabisa na tulikuwa tunaangalia inshu zingne na mambo yalikuwa yanaenda vizuri japo kila mtu huwa anaangalia manufaa yake binafsi au kikundi cha watu baadhi huwezi kumfurahisha kila mwanadamu hata Yesu Kristo alikuja kufa kwa ajili ya wenye dhambi lakn bado watu hawakumkubali hata wale wa jamii yake "NABII HAPATI HESHIMA KATIKA NCHI YA KWAO"
Rais magufuli aliyaona hayo ndo maana akaamua kufanya ambayo anaona kwa asilimia kubwa yatawanufaisha watanzania hao hao walikuwa wanapiga kelele kuhusu ndege ndo hao hao wanatumia hizo ndege kwenda kwenye mikutano yao na mabeberu
Rais Samia alivyowapatia uhuru wa vyama pinzani mi kwa upande wangu niliona ameenda kufukua makaburi ambayo mwenda zake alikuwa ameyafukia.
Rais Magufuli watanzania tutakukumbuka kwa mengi uliyoyafanya japo n kwa kipindi kifupi cha uongozi wako pumzka kwa amani shujaa wetu.
veronica__france-20210618-0001.jpg
 
Mama anatakiwa kuleta kura ya maoni nani anataka na nani ataki

Na kwenye usimamizi kila kitu wapewe chadema kusimamia

Im sure watu ambao hawataki katiba mpya watashinda tu
Kama mnazo pesa. Leteni hizo pesa tulete kura maoni
 
Watu tunaamini hivyo kwakua hizi kelele zenu hazikuwepo kabla ya Magufuli kufariki,hivyo basi mnamdharau sana Samia.

Kimsingi hiyo kauli ya Mbowe inaamsha hisia za SSH,kutaka kuwaonyesha makucha yake na mwisho wa siku tutarudi kulekule.
Huu ndo ukweli. Very sad hawa jamaa kuturudisha kule. Wengine hatupendi kabisa maisha ya mshikemshike.
 
Nilisema samia ataelewa tu jinsi nchi inavoelewa!!
Ndo kwanzaa wameanza kutikisa kiberiti
 
Back
Top Bottom