Mbowe katoka gerezani, Tundu Lissu yupo kimya, inashangaza! Ukimya unamaanisha nini? Kwanini Mbowe hajamtaja Lissu katika interview zake?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Freeman Mbowe kwa sasa ni mtu huru kama ilivyo kwa jina lake, kesi yake ilifutwa na Mahakama Kuu, mmoja wa watu waliokuwa wakipiga kampeni ya kuhoji juu ya kesi aliyofunguliwa Mbowe na wenzake watatu ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Lissu alifikia hatua ya kuomba kuonana na Rais Samia Hassan Suluhu wakiwa huko Ubelgiji, mara baada ya mkutano wao, Lissu akajitokeza hadharani na kufafanua yale aliyozungumza na Rais Samia, moja ya hoja yake ni kuwa alimwambia kuhusu kesi ya Mbowe.

Kujitokeza kwa Lissu kuzungumza kile walichozungumza na Samia ndani ya muda mfupi baada ya mazungumzi hayo iliwashangaa wengi lakini nilimuelewa kwa kuwa inawezekana alitaka kujisafisha, anajua CHADEMA wenzake wasingemuelewa kama angekaa kimya.

Sasa Mbowe ametoka gerezani, shangwe ni kubwa mitaani, mitandaoni nako kumechafuka kila mtu anazungumza lake kuhusu Mbowe kuachiwa, lakini ni tangu kesi hiyo ifutwe siku kadhaa zimepita sasa, Lissu yupo kimyaaaaaaa.

Kunani kwa Lissu kuhusu huu ukimya wake, mwenyekiti wake ametoka, yupo mtaani, lakini mbona hatuoni tamko lake wala reaction yake.

Wengi tunajua Lissu ni mmoj kati ya watu ambao akitaka kuzunguza kuhusu jambo lake huwa harudi nyuma, anazungumza hata kama jamii hasa wale wasiokubaliana na sera zake wataona kama anazingua, lakini kwa nini sasa yupo kimya.

Ampotea mitandaoni, hajaonyesha kama kilio chake kimesikika au hakijasikika, amefurahi au hajafurahi Mbowe kutoka gerezani? Cha kushangaza zaidi Mbowe mwenyewe hadi sasa hajataa jina la Lissu katika mahojiano yote aliyoyafanya hadi sasa tangu ametoka.
 
Kwani ZZK nae si alimuomba mama, mbona Mbowe hakumtaja, na Maaskofu nao hakuwasemea ingawa walienda kumuona Rais na kumuombea msamaha.

Acha upuuzi bana
 
Kazi ameshaimaliza hata katika mchezo wa mbio mwenye kukimbia mwingine Ila akifika kwenye mstari wa ushindi wanaopiga kelele nyingi ni wengine.
 
Tumia AKILI UNAJUAJE KAMA HAWAWASILIANI? SIO KILA KITU WAKWAMBIE
 
Ulitaka aseme Nini..kama wewe ungekuwa ni Lissu ungesema nini sasa hivi?
 
Tulia usiwe na hofu kwani Lissu atakuja nyumbani kwako kukujulisha aliwasiliana na Mbowe alipotoka.

Sasa tafutiza jingine la kuanzishia Post.
 
Mnahangaika sana. Mchango wa Lissu kutoka kwa Mbowe gereza ni extraordinary
 
Freeman Mbowe kwa sasa ni mtu huru kama ilivyo kwa jina lake, kesi yake ilifutwa na Mahakama Kuu, mmoja wa watu waliokuwa wakipiga kampeni ya kuhoji juu ya kesi aliyofunguliwa Mbowe na wenzake watatu ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu...
100% majungu.

Mbona Lisu alitajwa. Unafikiri nguvu ya umma ni wewe au Lisu na mashangazi?

"Nimetoka kwa sababu ya nguvu ya umma" Mowe alisema.

Nguvu ya umma huwezi wataja wote. Mi nakutajia tu hawa
1. TAL
2. Mashangazi
3. Jamii forums
4. Mimi
5. Twitter
6. Siyo wewe

Sent from my SM-A022F using JamiiForums mobile app
 
Freeman Mbowe kwa sasa ni mtu huru kama ilivyo kwa jina lake, kesi yake ilifutwa na Mahakama Kuu, mmoja wa watu waliokuwa wakipiga kampeni ya kuhoji juu ya kesi aliyofunguliwa Mbowe na wenzake watatu ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
An intelligent person does not react to the obvious.
 
Tuko Watanzania milioni 60. Mbowe hawezi kututataja wote!!
Lissu alifikia hatua ya kuomba kuonana na Rais Samia Hassan Suluhu wakiwa huko Ubelgiji, mara baada ya mkutano wao, Lissu akajitokeza hadharani na kufafanua yale aliyozungumza na Rais Samia, moja ya hoja yake ni kuwa alimwambia kuhusu kesi ya Mbowe.
 
Freeman Mbowe kwa sasa ni mtu huru kama ilivyo kwa jina lake, kesi yake ilifutwa na Mahakama Kuu, mmoja wa watu waliokuwa wakipiga kampeni ya kuhoji juu ya kesi aliyofunguliwa Mbowe na wenzake watatu ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Chadema imeuzwa mkuu kitamboo, ata Lema, Msigwa, Heche ccm imefanikiwa mpaka kwa hao ma-giant wa chadema, Lissu atasema nini na kampigia mama magoti beligium, Mbowe kaachiwa breki ya kwanza Ikulu, mi sioni tofauti ya Mbowe na kina hao Covid-19 Halima mdee,

Tanzania bado tunahitaji kiongozi wa upinzani atayewavusha Watanania na utawala wa ccm uliokubuhu., Watanganyika ni viongozi rahisi sana hata uone wanapiga makelele vipi, wanafikia bei mapema sana.

Mbowe miezi 8 aliyokaa jela imetosha kuona udhaifu wa chadema, chadema wameshindwa vita, anajidhalilisha Ikulu kwa miezi 8 aliyokaa jela hata familia yake hakwenda kuiona kabla ameenda kwa mama, ovyo kabisa, poor chadema, walikuwa wanamsema maalim seif, zitto kabwe sana sasa wao wamefika wapi,
 
Freeman Mbowe kwa sasa ni mtu huru kama ilivyo kwa jina lake, kesi yake ilifutwa na Mahakama Kuu, mmoja wa watu waliokuwa wakipiga kampeni ya kuhoji juu ya kesi aliyofunguliwa Mbowe na wenzake watatu ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Sasa ana haja gani ya kuogelea hilo wakati kesha maliza kazi..
 
Freeman Mbowe kwa sasa ni mtu huru kama ilivyo kwa jina lake, kesi yake ilifutwa na Mahakama Kuu, mmoja wa watu waliokuwa wakipiga kampeni ya kuhoji juu ya kesi aliyofunguliwa Mbowe na wenzake watatu ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Lissu alifikia hatua ya kuomba kuonana na Rais Samia Hassan Suluhu wakiwa huko Ubelgiji, mara baada ya mkutano wao, Lissu akajitokeza hadharani na kufafanua yale aliyozungumza na Rais Samia, moja ya hoja yake ni kuwa alimwambia kuhusu kesi ya Mbowe.

Kujitokeza kwa Lissu kuzungumza kile walichozungumza na Samia ndani ya muda mfupi baada ya mazungumzi hayo iliwashangaa wengi lakini nilimuelewa kwa kuwa inawezekana alitaka kujisafisha, anajua CHADEMA wenzake wasingemuelewa kama angekaa kimya.

Sasa Mbowe ametoka gerezani, shangwe ni kubwa mitaani, mitandaoni nako kumechafuka kila mtu anazungumza lake kuhusu Mbowe kuachiwa, lakini ni tangu kesi hiyo ifutwe siku kadhaa zimepita sasa, Lissu yupo kimyaaaaaaa.

Kunani kwa Lissu kuhusu huu ukimya wake, mwenyekiti wake ametoka, yupo mtaani, lakini mbona hatuoni tamko lake wala reaction yake.

Wengi tunajua Lissu ni mmoj kati ya watu ambao akitaka kuzunguza kuhusu jambo lake huwa harudi nyuma, anazungumza hata kama jamii hasa wale wasiokubaliana na sera zake wataona kama anazingua, lakini kwa nini sasa yupo kimya.

Ampotea mitandaoni, hajaonyesha kama kilio chake kimesikika au hakijasikika, amefurahi au hajafurahi Mbowe kutoka gerezani? Cha kushangaza zaidi Mbowe mwenyewe hadi sasa hajataa jina la Lissu katika mahojiano yote aliyoyafanya hadi sasa tangu ametoka.
Mbowe kashukuru nguvu ya umma kumtoa gerezani,Lissu ni sehemu ya nguvu ya umma.

Toa funza kichwani uelewe mambo
 
Back
Top Bottom