Mbowe kaumizwa sana, kufanyiwa oparesheni

Mbowe kaumizwa sana, kufanyiwa oparesheni

Hakuna kutoa chochote hilo lijamaa limetuibia pesa nyingi ya ruzuku B8!
 
Poleni sana mkuu....TUNAMUOMBEA SANA KAMANDA MH MBOWE APONE HARAKA ILI WAHUNI ccm WAENDELEE KUJIHARISHIA
 
Ndugai sina hakika kama ana akili timamu , nimeomba mara nyingi Chadema kuacha kushirikiana na wanaccm hata kwenye misiba , hilo ni kundi lenye kushabihiana na wachawi , ndio maana sikutaka jana Mwanaccm yeyote kwenda kumuona Mh Mbowe hospitali , si Waziri mkuu wala Rais , hawakutakiwa kuruhusiwa
 
Sijui kama wote tunaiona hatari inayoelekea kuja hapo mbeleni,kukosekana wapinzani bungeni na ukandamizaji unaotokea vitajaibuka vikundi hatari na mashambulizi yanaweza elekezwa kwa wanaocheka Leo. Tujitizame Mimi ninawasiwasi maana wanasemaga what goes around comes around
 
natamani sana uchunguzi ukamilike haraka ili ukweli ufahamike wazi. naamini hakuna kitu kitakacho achwa, na ikibainika kuna usanii umechezwa basi hatua kali zichukuliwe.
 
...Domo kubwa masikio madogo, kama wale walevi mnaowashabikia kwa kuropoka juu ya mtu kuumizwa. Mnaudhi sana. Angalia kwenye hili hata Magufuli amekuwa muungwana, lakini nyie madungaembe mkiongozwa na Ndugai wala!
Hayo mengine ni sawa na mpiga ngoma kubwa ni kushukuru mmeanza kumkubali taratibu japo mnasuasua ila tutafika tu.
 
Hali ni mbaya sana,wanowatetea waliofanya unyama huu dhidi ya Mh.Mbowe tuwaeleweje hasa?Jaribuni basi kuficha dhamira zenu ovu dhidi ya wapenda haki.Hao ni Watanzania wenzenu,kwa nini mnawatakia mabaya?Wamewakosea kipi hicho?
 
Wote tunajua kaumizwa sana maana kuteguka sio mchezo. Ngazi zile zimejengwa kwa zege kali ukiteleza pale, lazima zikuumize sana na hasa ukiwa umeranduka nyagi!
 
Eti kaumizwa sana tena sana ... Mbona mnamdekeza sana. Walevi wangapi wanaanguka na haiwi habari ... POMBE SIO CHAI ☕️
 
Utawala wa hovyo usiojiamini huwa ni kuwarisha wanasiasa wanahoji utendaji wake, waandishi wa habari, wanaharakati, Bunge na Mahakama....ukimaliza hapo nani wa kukusogelea ... hajipendi!!
 
Sijui kama wote tunaiona hatari inayoelekea kuja hapo mbeleni,kukosekana wapinzani bungeni na ukandamizaji unaotokea vitajaibuka vikundi hatari na mashambulizi yanaweza elekezwa kwa wanaocheka Leo. Tujitizame Mimi ninawasiwasi maana wanasemaga what goes around comes around
Wao wanayo mifano ya kukuonyesha, Rwanda, Uganda, Burundi na kwingineko.

Wanajua upinzani ukiwa dhaifu zaidi ndio raha kwao, ndio maana wanafanya juhudi zote hilo litimie.

Na kwa Tanzania yetu hii inavyoonekana sasa, hata hao Rwanda, Burundi, Uganda, n.k., wanayo nafuu zaidi. Sisi tutakuwa kondoo kabisa.

Hayo ya 'vikundi' sijui unayatoa wapi! Si hapa.
 
Ni aibu badala ya kujadili bajeti ya nchi, bunge linatumia siku mbili kujadili tukio la kuvamiwa kwa Mbowe. Cha kusikitisha hawajadili namna ya kumsaidia kama mbunge mwenzao bali wanapiga majungu.

Ni bora waendelee na bajeti kuliko kupoteza muda kupiga majungu. Jana Msukuma kasema Mbowe alikuwa anakunywa Konyagi Kubwa (Faru John) na ndio iliyopelekea kuanguka na kuvunjika. Ndugai kasema madaktari wake walimjulisha kuwa Mbowe alikua amelewa chakari. Kibajaj akasema alianguka akiwa na mwanamke na mwanamke huyo alikimbia. Waitara amemtaja mwanamke huyo kwa jina bungeni. Yani majungu majungu tu.

Kama kuna utata kuhusu kuvamiwa kwa Mbowe, utata huo unapaswa kumalizwa na mambo mawili tu.

#Mosi; Mbowe ana walinzi wa aina mbili. Walinzi wa serikali (TISS) na walinzi wa chama (Red Brigade). Serikali ilimuondolea Mbowe walinzi mwezi uliopita kwa sababu ya issue ya Covid19. Yani serikali iliona moja ya njia za kudhibiti maambukizi ya Covid19 ni kuondoa walinzi.

Lakini viongozi wengine walibaki na walinzi. Spika ana walinzi, PM, Naibu Spika etc. Hapa kuna kitu hakiko sawa. Kwanini viongozi wengine walibaki na walinzi kama issue ni Covid19? Na kwanini Mbowe hakurudishiwa ulinzi baada Rais JPM kutangaza maambukizi yamepungua?

Kwahiyo wanaohoji kuhusu ulinzi wa Mbowe wanapaswa kuhoji mambo mawili. Kwanini serikali haikumrudishia ulinzi hata baada ya Covid19 kupungua, kisha wahoji walinzi binafsi wa Mbowe (red brigade) walikua wapi wakati anavamiwa.

#Pili; Nyumba anayoishi Mbowe ina CCTV camera 24hrs. Kwanini picha za CCTV zisitolewe? Kama alianguka ataonekana na kama alivamiwa ataonekana pia. Kwnn tunapoteza muda kusigana kwenye jambo ambalo ukweli wake ni rahisi tu kupatikana?

Nyumba anayoishi Mbowe ni ya serikali. System za CCTV ni za serikali, hata "control room" wanaoaccess ni maafisa wa serikali. Kwanini serikali isitoe hizo picha zinazoonesha Mbowe akianguka badala ya kuendelea kupiga porojo?

Kwa ninavyoijua serikali ya CCM ingekua kweli Mbowe kaanguka usiku akiwa na mwanamke na "Faru John" mkononi, nina uhakika wangeprint hizo picha na kuzisambaza kuanzia Lupiro kule Ulanga hadi Yombo Buza kwa Abiola.

Lakini ukiona serikali inakomaa kuwaaminisha watu kuwa Mbowe alianguka, lakini haitaki kutoa picha za CCTV, halafu serikali hiyohiyo iliyomuondolea Mbowe ulinzi mwezi mmoja tu uliopita, lazima uhisi kuna kitu. Watanzania wa leo sio wajinga.!!

Malisa Gj
 
Back
Top Bottom