Kila nafsi itaonja umauti"Leo asubuhi nilikuwa miongoni mwa viongozi na maafisa wa Chama tuliofika kumjulia hali Mh Mwenyekiti Freeman A. Mbowe. Pamoja nami alikuwepo Mh. Godbless Lema Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, James Mbowe na Aallan Bujo.
Mwenyekiti wetu kaumizwa sana, kaumizwa sana, Tumuombee oparesheni na matibabu mengine yaende salama apone haraka...
"Leo asubuhi nilikuwa miongoni mwa viongozi na maafisa wa Chama tuliofika kumjulia hali Mh Mwenyekiti Freeman A. Mbowe. Pamoja nami alikuwepo Mh. Godbless Lema Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, James Mbowe na Aallan Bujo.
Mwenyekiti wetu kaumizwa sana, kaumizwa sana, Tumuombee oparesheni na matibabu mengine yaende salama apone haraka.
Mwenyekiti wetu kaumizwa sana, Wanaoendeleza porojo kuwa alilewa akateleza na kuanguka wapuuzeni, Jeshi la Polisi ikiwa litakuwa na dhamira ya kuchunguza jambo hili naamini halitaacha kuwahoji wapotoshaji hawa wakiongozwa na Job Ndugai, Lusinde, Lijualikali, Silinde nk.
Uzuri Mbowe hajafa, akili yake na Moyo wake ni nzima isipokuwa mwili ndio umeumizwa. Hivyo uzushi wowote unaofanywa na makundi toka ccm watambue Mbowe anazungumza na akili yake iko vizuri.
Na Yericko Nyerere"
View attachment 1474265
Mimi binafsi toka Jana nishaamua sitatoa pole kwa kiongozi yeyote Wa ccm akifa wala kuumwa, nitashangilia tu.Kilichofanywa Jana bungeni kushangilia na kukejeliwa mbowe kwa yaliyompata maccm Ni wanyama.Sijui kama wote tunaiona hatari inayoelekea kuja hapo mbeleni,kukosekana wapinzani bungeni na ukandamizaji unaotokea vitajaibuka vikundi hatari na mashambulizi yanaweza elekezwa kwa wanaocheka Leo. Tujitizame Mimi ninawasiwasi maana wanasemaga what goes around comes around
Haahaa pombe so ndo rais auEti kaumizwa sana tena sana ... Mbona mnamdekeza sana. Walevi wangapi wanaanguka na haiwi habari ... POMBE SIO CHAI ☕
Ni aibu badala ya kujadili bajeti ya nchi, bunge linatumia siku mbili kujadili tukio la kuvamiwa kwa Mbowe. Cha kusikitisha hawajadili namna ya kumsaidia kama mbunge mwenzao bali wanapiga majungu.
Ni bora waendelee na bajeti kuliko kupoteza muda kupiga majungu. Jana Msukuma kasema Mbowe alikuwa anakunywa Konyagi Kubwa (Faru John) na ndio iliyopelekea kuanguka na kuvunjika. Ndugai kasema madaktari wake walimjulisha kuwa Mbowe alikua amelewa chakari. Kibajaj akasema alianguka akiwa na mwanamke na mwanamke huyo alikimbia. Waitara amemtaja mwanamke huyo kwa jina bungeni. Yani majungu majungu tu.
Kama kuna utata kuhusu kuvamiwa kwa Mbowe, utata huo unapaswa kumalizwa na mambo mawili tu.
#Mosi; Mbowe ana walinzi wa aina mbili. Walinzi wa serikali (TISS) na walinzi wa chama (Red Brigade). Serikali ilimuondolea Mbowe walinzi mwezi uliopita kwa sababu ya issue ya Covid19. Yani serikali iliona moja ya njia za kudhibiti maambukizi ya Covid19 ni kuondoa walinzi.
Lakini viongozi wengine walibaki na walinzi. Spika ana walinzi, PM, Naibu Spika etc. Hapa kuna kitu hakiko sawa. Kwanini viongozi wengine walibaki na walinzi kama issue ni Covid19? Na kwanini Mbowe hakurudishiwa ulinzi baada Rais JPM kutangaza maambukizi yamepungua?
Kwahiyo wanaohoji kuhusu ulinzi wa Mbowe wanapaswa kuhoji mambo mawili. Kwanini serikali haikumrudishia ulinzi hata baada ya Covid19 kupungua, kisha wahoji walinzi binafsi wa Mbowe (red brigade) walikua wapi wakati anavamiwa.
#Pili; Nyumba anayoishi Mbowe ina CCTV camera 24hrs. Kwanini picha za CCTV zisitolewe? Kama alianguka ataonekana na kama alivamiwa ataonekana pia. Kwnn tunapoteza muda kusigana kwenye jambo ambalo ukweli wake ni rahisi tu kupatikana?
Nyumba anayoishi Mbowe ni ya serikali. System za CCTV ni za serikali, hata "control room" wanaoaccess ni maafisa wa serikali. Kwanini serikali isitoe hizo picha zinazoonesha Mbowe akianguka badala ya kuendelea kupiga porojo?
Kwa ninavyoijua serikali ya CCM ingekua kweli Mbowe kaanguka usiku akiwa na mwanamke na "Faru John" mkononi, nina uhakika wangeprint hizo picha na kuzisambaza kuanzia Lupiro kule Ulanga hadi Yombo Buza kwa Abiola.
Lakini ukiona serikali inakomaa kuwaaminisha watu kuwa Mbowe alianguka, lakini haitaki kutoa picha za CCTV, halafu serikali hiyohiyo iliyomuondolea Mbowe ulinzi mwezi mmoja tu uliopita, lazima uhisi kuna kitu. Watanzania wa leo sio wajinga.!!
"Leo asubuhi nilikuwa miongoni mwa viongozi na maafisa wa Chama tuliofika kumjulia hali Mh Mwenyekiti Freeman A. Mbowe. Pamoja nami alikuwepo Mh. Godbless Lema Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, James Mbowe na Aallan Bujo.
Mwenyekiti wetu kaumizwa sana, kaumizwa sana, Tumuombee oparesheni na matibabu mengine yaende salama apone haraka.
Mwenyekiti wetu kaumizwa sana, Wanaoendeleza porojo kuwa alilewa akateleza na kuanguka wapuuzeni, Jeshi la Polisi ikiwa litakuwa na dhamira ya kuchunguza jambo hili naamini halitaacha kuwahoji wapotoshaji hawa wakiongozwa na Job Ndugai, Lusinde, Lijualikali, Silinde nk.
Uzuri Mbowe hajafa, akili yake na Moyo wake ni nzima isipokuwa mwili ndio umeumizwa. Hivyo uzushi wowote unaofanywa na makundi toka ccm watambue Mbowe anazungumza na akili yake iko vizuri.
Na Yericko Nyerere"
View attachment 1474265
Je, mlimuuliza alikuwa anakwenda/kutoka wapi usiku wa manane?
Kwa kweli inasikitisha sana!!Mungu awalipe kwa kuwapa pigo takatifu mpaka wajute kwani wamejisahau sana kufikia hatua ya kusahau kuwa kuna Mungu.
Wamebakiza hatua ya kupiga teke na kutemea mate maiti za wale wenye itikadi tofauti na wao, huku kwingine wameshamaliza.
Anaekukejeli ukiwa kitandani,atashindwa kupiga teke mwili au jeneza lako akipata nafasi?
Kuna watakaokwenda kumuona kinafiki na kutoa chchote huku rohoni wakifurahia na pengine wakimuombea mabaya zaidi.
Hawa si watu ndugu zangu japo wanatembea kwa miguu miwili kama wanadamu.
Mkuu huyu ni ndugu malisa kachambua hili,tatizo vijana wengi hawatumii akili zao vizuri waimeishia kuwa mashabiki tuWw ndio umezungumza uhalisia na jinsi ya kumaliza hizi porojo zinazopigwa. Toka jana najaribu kuangalia nani ataongelea hizo CCTV Camera, inaonekana ni kweli alipigwa, ndio maana toka jana mpaka leo polisi haisemi chochote, bali upotoshaji uliofanywa bungeni ndio unataka kugeuzwa kuwa ukweli wenyewe.
Hatuzalishi punga kama wewe, kerkoj○€ ulale.!!Mwambie akutolee posa, maana huoni, husikii huelewi
Hakuna Katazo la kutembea usiku nchi hii. Na Mbowe sio mwanafunzi wa boarding school, useme alikuwa wapi nyakati za usiku. Labda kama umekosa hoja ila unataka uonekane na ww umechangia mada za hali ya Mbowe. Mke wake ndio anapaswa kumuuliza alitoka wapi usiku, sio sisi wanaume wenzake.
Ukishakuwa Kiongozi lazima ukubali kwamba Watanzania watahitaji kufahamu shughuli unazofanya hata usiku wa manane. Kama unahitaji mkeo tu ndio akuulize usiwe Kiongozi wa chama au Serikali. Kaa nyumbani na familia yako usijihusishe na uongozi, matendo yako ukiwa kiongozi yana matter.
Nje ya mada kidogo.. picha kali sana! Yani mmetokelezea mbaya! Big up sana wakuu! Yani mmeua mbaya.. hapo kakosekana mwamba tu ila sio kesi mmeiaribia kamera kinoma yani👊"Leo asubuhi nilikuwa miongoni mwa viongozi na maafisa wa Chama tuliofika kumjulia hali Mh Mwenyekiti Freeman A. Mbowe. Pamoja nami alikuwepo Mh. Godbless Lema Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, James Mbowe na Aallan Bujo.
Mwenyekiti wetu kaumizwa sana, kaumizwa sana, Tumuombee kama ni oparesheni na matibabu mengine yaende salama apone haraka.
Mwenyekiti wetu kaumizwa sana, Wanaoendeleza porojo kuwa alilewa akateleza na kuanguka wapuuzeni, Jeshi la Polisi ikiwa litakuwa na dhamira ya kuchunguza jambo hili naamini halitaacha kuwahoji wapotoshaji hawa wakiongozwa na Job Ndugai, Lusinde, Lijualikali, Silinde nk.
Uzuri Mbowe hajafa, akili yake na Moyo wake ni nzima isipokuwa mwili ndio umeumizwa. Hivyo uzushi wowote unaofanywa na makundi toka ccm watambue Mbowe anazungumza na akili yake iko vizuri.
Na Yericko Nyerere"
View attachment 1474265
Usiku Mbowe alienda kunywa pombe maana hajaanza jana na wala hataacha. Hakuna mtanzania ana muda na maisha binafsi ya Mbowe baada ya muda wake wa kazi. Jifunze kutofautisha majukumu ya kazi na maisha binafsi ya kiongozi. Labda uwe shambenga ndio utamfuatilia kiongozi hata wakati wa muda wake binafsi.