Mbowe kaumizwa sana, kufanyiwa oparesheni


Wewe sio wa kwanza, kuna mtu kaiarifu DW, Kuwa Mbowe katolewa Kituo cha afya Dodoma akiwa hana fahamu. Cha ajabu alivyoingizwa tu kwenye chatter akainuka na kupiga Salute kwa Makamanda😂😂
 
Alafu ndiyo hao hao wanaokuja front of th' camera wanasema kuna corona wakati hapo walipo wamebanana a.k.a zero distance.
Huwa wanasahau siasa za propaganda na maisha halisi
 
Hivi huyu Job Ndugai alikuwa na sababu ya maana kwenda kumjulia hali Mbowe? Maana kwa kauli anazotoa, ni kama alikwenda kuhakiki maumivu ya mbowe kama dozi inatosha au iongezwe. Uadui wa aina hii kwenye siasa ni hatari
USISAHAU mkuu pia wamejiongezea kinga kikatiba wasishitakiwe.
 
Namimi nakuunga mkono mkuu tungekuwa na usalama wa taifa wazuri wasingeacha wanasiasa wafanye haya wayafanyayo Leo.
 
Bado jumapili wataenda kanisani kuomba waombewe mbele ya MADHABAHU jamani Kama kweli Mungu yupo haya atayajibu kwa wakati wake kutakuchwa tu Haina shida.
 

Writing in English doesn't add any value in your points. Pointless will remain as it is, since comes from the same poor Brain.
 
Nasubiri bill ya matibabu utaambiwa ni 1m kwa siku wakati mguu umeshawekwa p.o.p na anaweza kaa nyumbani.
Kwani hiyo hela Hela unatoa wewe
Mbona inakuumaa

Ova
 
Hoja zako ni sahihi kabisa, hasa ikizingatiwa kuwa Mbowe kama binadamu ana maisha yake, marafiku na maadui. Kinachoharibu tukio/mkasa uliompata ni pale unapohusishwa na siasa pasipo ushahidi, ila hisia tu. Hivyo basi, upande wa siasa unaotuhumiwa nao wana uhuru na haki ya kujibu tuhuma hizo kwa njia ambayo wanaona inafaa.
 

Ungeachia tu kwenye kiswahili.

Amandla...
 
Kabisa
 
Kwa upande mmoja hoja yako ina mantiki pale Bunge, chini ya Spika, limeshabikia tuhuma ambazo hazijathibitishwa. Kwa Taasisi kubwa kama hiyo, tulitegemea ingetumia busara kusubiri matokeo ya uchunguzi na si ushabiki.

Kwa upande mwingine, Uongozi wa CHADEMA nao umekurupuka kwa tuhuma zenye mlengo wa kisiasa pasipo kuwa na subira ya uchunguzi. Nia yao dhahiri ni ya kutafuta huruma na hasa hasa shutuma ya Kimataifa dhidi ya Serikali iliyoko madarakani. Na hili ndilo lililotokea pale taarifa za kuilaumu Serikali zimeanza kutolewa kimataifa.

Matokeo ya kukurupuka kwa pande zote mbili kuathiri matokeo ya uchunguzi unaofanywa na Polisi kukubalika au la. Ni matumaini ya kila mtu Polisi watatumia weledi wao kutoa taarifa ya ukweli wa tukio zima na pande zote mbili kuipokea na kuikubali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…