Mbowe kijana wa CCM kwa kivuli cha upinzani

Mbowe kijana wa CCM kwa kivuli cha upinzani

CCM kama chama dola nchini Tanzania kimefanikiwa sana kujitengenezea upinzani wake na wapinzani wake ambao kwa uhalisia nao ni Ccm nje ya Ccm. Mmoja wao ni Mbowe na chama chake cha Chadema.

Historia inatuambia, waanzilishi wote wa Chadema walikuwa Benki kuu. Yaani Mtei, Bob Makani na Mbowe na walitolewa kwa sababu maalum kutengeneza chama cha upinzani ili Tanzania itambulike na dunia kama imeruhusu mfumo wa vyama vingi na demokrasia.

Tangu Chadema iasisiwe, hatujashuhudia kiongozi tofauti ya hao watatu waliotoka BOT kwa shughuli maalim kuulaghai umma wa kimataifa juu ya uwepo wa vyama vingi na demokrasia Tanzania.

Baada ya Chadema kuasisiwa, wakaja wanachama wengi ambao hawakuwa sehemu ya mpango huo (Kuilaghai dunia) hawa wakaja kwa nia ya dhati kabisa ya kuiondo Ccm na hapo ndio Mbowe akawa mkali kama pilipili.

Tunaanza na Kaburu, huyu bwana alikuwa mwiba kweli kwa serikali ya Ccm. Mbowe ili kulinda maslahi yake mwaka 2005 alishilikiana na Ccm Bega kwa Bega kuhakikisha Kaburu anashindwa na Serukamba. Kwanza Mbowe hakumpigia kampeni Kaburu, Kaburu hakupewa sapoti na Chama kabisa mpaka alipoangushwa. Na kama zawadi Mbowe akapewa jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto kabwe.

Baada ya Kaburu kikaja kizazi cha pili, kizazi cha vijana waliokuwa na uchu wa mabadiliko kweli kweli. Hapa nawazungumzia kina Zitto, kafulila na Machali. Hawa wote walisambalatishwa kama upepo. Ccm ikapumua tena.

2010 mpaka 2015 hakuna mwanamageuzi aliyeonyesha njia kama Dr Slaa, Ccm ilikuwa inaondoka. Mbowe akakumbushwa wajibu wake wa kuilinda Ccm. Akaletewa criminal Lowasa na kumpoteza Dr Slaa ambae angeweza kutunishana misuli na Magufuli. Tukapoteza tena kizembe.

Kumpongeza Mbowe kwa kuiongoza Chadema miaka 20 pasipo kuitoa Ccm ni ujinga, kuimba nyimbo za Mbowe kuwaita wanaompinga wanafiki ni ujinga. Tunatakiwa kumuhoji Mbowe kwanini ndani ya miaka 20 ya uongozi wako hatujaona matokeo zaidi ya kubadilisha bendera na kauli mbiu?

Wanasiasa aina ya Mbowe wapo wengi duniani, upinzani ni sehemu yao ya agizo la kuvilinda vyama tawala na kuhakikisha upinzani wa kweli haupatikani.

Baada ya kuonekana Mama Samia hana Ushawishi Mbowe kaamua kumfanyia kampeni kwa dirisha la upinzani. Kuandamana bila bugudha mama aonekane ni mwana demokrasia, kumsifia majukwaani na kukiri kusaidiwa nae.

Mbowe anatengenezea sana sympathy na Ccm ili aendelee kuaminiwa kama kinara wa upinzani ila kiuhalisia hizo ni niia tuu za ku block upinzani wa kweli kuaminiwa. Wanaoelewa siasa watanielewa.

View attachment 2946424

Kwa leo naweka kalamu chini.

Kumchafua Mbowe na Lissu haitawezekana kwasababu wamekulia kwenye macho ya Watanzania. Lissu na Mbowe wanafahamika kuliko Samia na Mpango.
 
Mbowe ni tatizo kubwa linapokuja suala la mabadiliko. He is a problem na bahati mbaya bado kuna idle youths wanaomuamini
Baadala mjadili issues mnajadili personalities. Report ya CAG inaonesha ATCL imepata hasara ya bilioni 6 , umebaki kuleta nadharia za kijinga.
 
Ukiona comment fupi namna hii jua umechomwa mpaka akili. Pole sana
Pole wewe uliyepinda mgongo kuandika gazeti loooote lile ukiamini kuwa umeunda bomu la nuclear kumbe ni sawa na mpira wa makaratasi. Huna jipya,rudi tena kwenye drawing board. Chadema hii aliishindwa yule dhalim aliyekuwa CIC itakuwa wewe mtoto mdogo ambaye hata historia ya nchi huijui.
 
Mbowe atawafanya mharishe damu mwaka huu. Na bado tunae tena kwa miaka mingine mingi mbele! Ccm hamumtaki mbowe mnamtaka nani?
Halafu walivyokuwa wapumbavu wanadai kuwa ni mtu wao lakini ndiyo hao hao wanampiga vita 24/7 wanafanya kupeana zamu za kuanzisha nyuzi za kumshambulia mchana kutwa usiku kucha. CCM ina hazina kubwa sana ya wapumbavu.
 
Pole wewe uliyepinda mgongo kuandika gazeti loooote lile ukiamini kuwa umeunda bomu la nuclear kumbe ni sawa na mpira wa makaratasi. Huna jipya,rudi tena kwenye drawing board. Chadema hii aliishindwa yule dhalim aliyekuwa CIC itakuwa wewe mtoto mdogo ambaye hata historia ya nchi huijui.
Umeumia sana bro, kama umefunga tuliza munkari usiue swaumu
 
Halafu walivyokuwa wapumbavu wanadai kuwa ni mtu wao lakini ndiyo hao hao wanampiga vita 24/7 wanafanya kupeana zamu za kuanzisha nyuzi za kumshambulia mchana kutwa usiku kucha. CCM ina hazina kubwa sana ya wapumbavu.
Chadema mna hazima ya mazezeta na ndio mtaji wa kamanda wa Angq
 
Back
Top Bottom