Wakati fulani nilipopata habari hizi, nilijua ni muendelezo wa siasa zetu zisizo na afya njema.
Ila nilipata kusikia pia kuwa hivi sasa Meya wa Kinondoni, rafiki yangu Jacob pamoja na mameya wengine wa Jiji mama la Dar es salaam wamekuwa watu wa karibu na familia ya Mhe Lowassa.
Nyumbani kwa Mhe Lowassa ni ofisi ya pili ya Meya huyo wa Kinondoni, mwanzoni sikuwa naamini sana maana maneno maneno ni mengi, ila thread hii inanipa picha nyingine ambayo inakaribia kuondoa ule walakini niliyokuwa nayo hapo kabla.
Lisamwalo lipo, tusubiri hiyo Novemba.