Uchaguzi 2020 Mbowe kusema No Lissu, No Election ni dharau kwa Vyama vingine vya Siasa

Uchaguzi 2020 Mbowe kusema No Lissu, No Election ni dharau kwa Vyama vingine vya Siasa

CCM imekuwa aibu tupu, sijui hata wanachama wanaficha wapi nyuso zao, aibu tupu, mnaogopa uchaguzi kama ukoma?! Kitaeleweka tu.
 
Wanadanganywa na huyo mzungu aliye andika barua za kuitisha Tanzania. Kawapa kiburi na jeuri Mbowe, Lissu na genge lao.Kama wananchi watanzania tutakubali huu ujinga watu millioni 60 na ushee tutakua Taifa la ajabu kuwahi kuwepo chini ya mbingu.

Mbona tuliandamana pale SA walipo zuia ndege yetu?! Inashindikana nini kuandamana kuwaonesha hawa wanaokejeli maendeleo na miundo mbinu iliyojengwa na inayoendelea kujengwa kuwa wanatukera na wafunge mijidomo yao michafu.

Dunia na mataifa mengine watakuwa wanatudharau na kutushangaa kwa kweli. Wao wanatamani wangepata Rais mchapa kazi kama huyu wa kwetu, JPM. Sisi anatokea mtu/Watu tena wachache ambao wanatamaa na kusukumwa na maslahi yao binafsi zaidi, wanaongea maneno ya kejeli na kashfa na tuna waangalia pengine kuwashabikia. Tunashindwa hata kuonesha kukereka tu!! Tumedanganywa na kudanganyika kwamba mambo ya siasa yamegeuka ushabiki wa Simba na Yanga. Hii si sawa hata kidogo, kama Taifa tumekosea pahala tujisahihishe.
 
Hatuta elewana ohoooo tunamtaka lisu hao wengine ni wenu
 
Tabia ya kudharau vyama vingine ni Mbaya Sana.
 
Back
Top Bottom