Pre GE2025 Mbowe: Lissu alikuwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, na ndiye alitunga vifungu vya kuondoa ukomo wa uongozi kwa viongozi wakuu na wajumbe wa Kamati Kuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Aliyesema ogopa technology hakukosea, imesaidia sana kusaidia watu vigeugeu kuwabana kwa maneno yao waliyowahi sema na wanayakana
 
Tueleze Sababu za msingi zilizokuwepo wakati ule ambazo sasa hazipo zilizopelekea yeye kama mwanasheria kusimamia kuondoa ukomo uliowekwa na waasisi wa chama hicho.
 
..kwani lazima apeleke muda gani? Muda ilikuwa haujafika, mbowe Jana kachemka, alipaswa kujibu kiongozi kwamba muda utafika katiba itarekebishwa, kwa chadema bila mbowe kukaa pembeni kitakuwa kimefika mwisho
 
Tueleze Sababu za msingi zilizokuwepo wakati ule ambazo sasa hazipo zilizopelekea yeye kama mwanasheria kusimamia kuondoa ukomo uliowekwa na waasisi wa chama hicho.
Mkuu mfuatilie lissu utaelewa vizuri, lissu kanyooka kama rula
 
Huu wako udini, muislam Hana haki ya kutoa maoni humu? Kabendera sheikh wa wapi?
Pole kwa kutoelewa.

Tafuta Pepsi bariidi ukae hapo pembeni mwa duka omba kiti usome kwa kutulia ili uelewa!.
 
MWONGO MKUMBWA

Mbowe HAJASEMA Lissu alitunga vifungu vya kuondoa ukomo wa uongozi.

Mbowe amesema Lissu hajawahi kuleta kwenye chama hoja ya kupendekeza kufuta ukomo.

Upeo wako wa kuelewa ni finyu mno, au unaongopa makusudi.
 
Kasikilize vizuri
 
Mwanasheria mkuu ndio anarekebisha katiba?

Chadema ni Wahuni sana 😂😂😂
Bwashee ina maana hujui kuwa katiba ndiyo sheria mama ya chama? Wasiojua sheria wanaweza kubadilisha vifungu vya katiba bila kuhusisha mwanasheria mkuu wa chama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…