Mbowe, Lissu chukueni hatua kurejesha nidhamu kwenye chama

Mbowe, Lissu chukueni hatua kurejesha nidhamu kwenye chama

Ni vizuri chama kuchukua hatua kudhibiti nidhamu ndani ya chama.

ANGALIZO: Hatua hizo zifuate HAKI ya mwanachama kuitwa na kuhojiwa, kamwe hatua hizo zisiwe chanzo Cha kuminya DEMOKRASIA na uhuru wa Kutoa maoni.

Tutafika tu.

Umeandika vyema.

Lengo isiwe kumwonea mtu. Chama kinahitaji "afisa mnadhamu" pia "kamati za nidhamu" kama zile za "maadili" walizo kwisha kuzikalia kina Paskali na kina Rashid.

HIzi ni changamoto za kukua kwa chama. Kusilelewe matatizo. Wanachama wapewe maelekezo.

Chama hakiwezi kuwa kama shamba la bibi.
 
CHADEMA inaweza kufanya vizuri zaidi na mno, kuliko kumwendekeza mhuni yeyote.[emoji419][emoji375]

CCM ndio wanafanya fitina zote hizi

Sent using Jamii Forums mobile app

Angalizo hapa:

CCM ndio wanafanya fitina zote hizi

Kwani Lissu anasema je?

Tundu Lissu: Kauli ya Diaspora watuache ni ya CCM, anayesema kauli hiyo anafanya kazi ya CCM

"Alaumiwe vipi shwetwani kwa binadamu kufanya dhambi?"

Kazi zingine za CCM wanafanya watu kwa kujua au hata kutokujua.

"Alaumiwe CCM kwa yeyote kuitikia miito ya ngoma za CCM kwa kujua au kutokujua kwao?"
 
Upo sahihi kabisaa aisee hii ni mistake wamefanya wao wenyewe Acha aendelee kuharibu mambo !!!

Ninadhani wawili hawa wanayo moral authority ya kumkemea yeyote na wakati wowote na akaufyata.

CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni

Mbona hata kwa kuwakana tu inaishia hapo?

13. Wahuni hawawezi kuachwa kujinasibu kwa niaba ya chama kwenye lolote lisilokuwa na ridhaa ya chama.

Labda dawa iko jikoni.

Wenye nchi wananchi. Wenye chama wanachama. Lakini hayupo aliye bora zaidi ya wengine.
 
Wameshauriwa sana, chama cha siasa kimejaa vijana wa hovyo waliojaa matusi mitandaoni kama akina Martin. Na kwa sasa hao watu wakisema jambo kinatafsiriwa na wengi kuwa ndio mwelekeo wa chama.

Ninakubaliana nawe. Uzi huu ulisheheni ushauri huo:

CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni

Tena bila ya kunung'unya maneno.

"Ni kugonga bila kuchoka, Hadi wafungue mlango. Kwa hakika wamo mle ndani, wanasikika."
 
Tutajitahidi kuwaelimisha mpaka wataelewa na kubadilika maana kwao wanaona maisha bila ccm maisha hayawezi songa,dhana hiyo tunastahili kwa pamoja kutoa darasa ili kupunguza idadi ya wahuni.

Hii ngoma inawahitaji wawili hawa au chama kutoa tamko rasmi. Tumekuwa tukisema sana na "ngoja ngoja huumiza matumbo:"

CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni

CCM inaingia vipi hapa? Hapa sijakuelewa.

Nikimrejea Lissu kuhusu CCM ninamwelewa sana:

Tundu Lissu: Kauli ya Diaspora watuache ni ya CCM, anayesema kauli hiyo anafanya kazi ya CCM

Wakemewe wahuni hawa kudemka na ngoma za CCM wakijinasibu kuyawafanya hayo Kwa ridhaa ya chama. Iwe rasmi tu si kwa niaba ya chama na wasijielekeze hivyo.

"Yaani kiroho safi tu."

Hawezi kulaumiwa CCM kwa uhuni wao, bali wahuni wenyewe.

Akisema Polepole:

"Mhuni ni ni mhuni tu! Ni wahuni!"

Mnyonge mnyongeni.
 
Wahuni hawana vitambulisho wala utambulisho. Kulikoni kutaka kuwafungamanisha na awaye yote ambaye hajasema au kukwambia wahuni unaowasema ni wake?

Nikukumbushe pia, mada haihusu uchaguzi. Zaidi sana nikuitishe kujikita kwenye mada Mkuu.

Vinginevyo maCCM makaanga mbuyu huwa hayachelewi ku kujikaribisha "uninvited" na upotoshaji wao uliopitiliza.

Waungwana imhotep, Elli, Zawadini, denoo JG, Pascal Mayalla, WALOLA VUNZYA, Rabbon, Pakawa, johnthebaptist na wenye nchi wenzangu angalau kupeana mashamba darasa wandugu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Nimesema hivyo nina hakika,we nenda kule twitter mseme Mbowe kwa jambo la ukweli utaona hizo comment na pia mseme na Lissu kwenye jambo pia la ukweli au hata uongo utaona comment zake ,kisha rudi hapa tujadili.
 
Kuna mjinga wao mmoja yupo kule twitter kazi yake ni kuwatukana watu mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu kama chadema wangekuwa watu makini Yule kijana mjinga angeshafukuzwa kitambo.
Huyu mjinga anakatisha Tamaa Sana na siasa zake za matusi
CHADEMA chukueni hatua dhidi ya kijana wenu Martin Masese huyu jamaa anawaharibia Sana na amevunja umoja wenu na wanachama wenu

Chama makini hakiwezi kuwa na wajinga kama huyo na msitegemee vijana kuwaunga mkono Kwa wapumbavu kama Martin
Yupo humu ,huyo mtu yeye kila kitu anajua,,siku moja kuna jamaa alimvaa kumbe anamjua akaanza kumtolea siri jinsi anavyodandia mali za wanaume wenzake na kutamba nazo mjini ikiwemo magari kwa mara ya kwanza alishindwa hiyo vita.
 
"Huu ni ushauri wa bure kwenu waungwana."

Ni muhimu kuyatambua yafuatayo:

1. CHADEMA kimekuwa ni chama chaguo la wengi kwa muda mrefu.

2. Si kwa sababu ni chama bora sana, ila ni kwa kuwa kinayo nafasi ya kufanya maboresho.

3. Kwamba ndani ya changamoto zilizopo, hatimaye tutafika.

4. Haipo siri kuwa katika siku za karibuni hali inataka kuelekea kubaya badala ya kuliko tarajiwa (changamoto safarini).

5. Kauli za kushangaza (kibri, matusi, kejeli, nk) kutokea kwa baadhi ya wenye kujinasibu kuwa wanachama, zimekuwa zikisikika.

6. Imekuwa ni kama zogo la magenge ya wahuni.

7. Hali hii haiwezi kuwavutia wenye akili zao kwa binafsi zao au hata kwa makundi yao.

9. Ukombozi unahitaji uungwaji mkono kutokea makundi mbalimbali hasa asasi za dini, kiraia, nchi, vyama washirika, nk.

10. Uhuni au wahuni hawawezi kuwa sehemu, kwenye uvutiaji wa uungwaji mkono huo.

11. Hali hii haipaswi kuachwa kuendelea au hata kuvumiliwa.

12. Ni muhimu zikachukuliwa hatua sahihi zenye kuonekana ili kuweka nidhamu kamili chamani.

13. Wahuni hawawezi kuachwa kujinasibu kwa niaba ya chama kwenye lolote lisilokuwa na ridhaa ya chama.

14. "Lissu, Mbowe chukueni jukumu hili sasa."

CHADEMA inaweza kufanya vizuri zaidi na mno, kuliko kumwendekeza mhuni yeyote.

Mhuni ni mhuni tu!
Usifiche maradhi
1. Tatizo ni.Mbowe kuendelea kung'ang'ania madaraka. Amechokwa
2. Mbowe kukifanya Chama kama biashara yake. Kutumia vibaya Ruzuku huku wengine wakitaabika. Kumbuka katika operation ya hivi karibuni, yeye akiwa anaruka na Chopa huku akijilipa miposho kundi lingine likiongozwa na Lissu lilitumia usafiri wa kawaida kwa gharama zao na michango wa wananchi.
3. Mbowe kutokuwa na msimamo thabiti. Wengine siyo wanafiki kuhusu Bandari huku yeye anauma na kupuliza.
4. Kuwapuuza wanaharakati waliopambana kuhusu bandari na kujitenga nao. Alidharau nguvu ya Slaa, Mwambukuzi na Sauti ya Watanzania.

Kimsingi bila kukubali kutundika daruga basi chama linazama.
 
"Huu ni ushauri wa bure kwenu waungwana."

Ni muhimu kuyatambua yafuatayo:

1. CHADEMA kimekuwa ni chama chaguo la wengi kwa muda mrefu.

2. Si kwa sababu ni chama bora sana, ila ni kwa kuwa kinayo nafasi ya kufanya maboresho.

3. Kwamba ndani ya changamoto zilizopo, hatimaye tutafika.

4. Haipo siri kuwa katika siku za karibuni hali inataka kuelekea kubaya badala ya kuliko tarajiwa (changamoto safarini).

5. Kauli za kushangaza (kibri, matusi, kejeli, nk) kutokea kwa baadhi ya wenye kujinasibu kuwa wanachama, zimekuwa zikisikika.

6. Imekuwa ni kama zogo la magenge ya wahuni.

7. Hali hii haiwezi kuwavutia wenye akili zao kwa binafsi zao au hata kwa makundi yao.

9. Ukombozi unahitaji uungwaji mkono kutokea makundi mbalimbali hasa asasi za dini, kiraia, nchi, vyama washirika, nk.

10. Uhuni au wahuni hawawezi kuwa sehemu, kwenye uvutiaji wa uungwaji mkono huo.

11. Hali hii haipaswi kuachwa kuendelea au hata kuvumiliwa.

12. Ni muhimu zikachukuliwa hatua sahihi zenye kuonekana ili kuweka nidhamu kamili chamani.

13. Wahuni hawawezi kuachwa kujinasibu kwa niaba ya chama kwenye lolote lisilokuwa na ridhaa ya chama.

14. "Lissu, Mbowe chukueni jukumu hili sasa."

CHADEMA inaweza kufanya vizuri zaidi na mno, kuliko kumwendekeza mhuni yeyote.

Mhuni ni mhuni tu!

Mkuu kwa maoni yangu nadhani ungetangaza upande wako wa kisiasa kabla ya hujaweka hoja yako hapa ili tuweze kuchangia na kuijadili hoja yako objectively.

Nasema hivyo kwa sababu:

1. Huwezi kutoa ushauri chanya na wenye nia njema kwa mshindani wako.

2. Taasisi yoyote hai lazima pawepo na ushindani au misigano ya mawazo, hoja na fikra.

3. Tofautisha mawazo, mitazamo na misimamo binafsi ya mwanachama dhidi ya taasisi husika.

4. Tofautisha katika ya kukosoa, kufikirisha na kusema ukweli dhidi ya kutukana au kukashfu.

5. Tuache watu waongee kwa uhuru ili mradi hawavunji sheria ya nchi. Tukubaliani kutofautiani bila ugomvi.

Kumalizia tusitake taasisi shindani zifanane na taasisi tuliomo kwa itikadi, mawazo, mitazamo na misimamo. Hiyo itakuwa midoli sasa!
 
"Huu ni ushauri wa bure kwenu waungwana."

Ni muhimu kuyatambua yafuatayo:

1. CHADEMA kimekuwa ni chama chaguo la wengi kwa muda mrefu.

2. Si kwa sababu ni chama bora sana, ila ni kwa kuwa kinayo nafasi ya kufanya maboresho.

3. Kwamba ndani ya changamoto zilizopo, hatimaye tutafika.

4. Haipo siri kuwa katika siku za karibuni hali inataka kuelekea kubaya badala ya kuliko tarajiwa (changamoto safarini).

5. Kauli za kushangaza (kibri, matusi, kejeli, nk) kutokea kwa baadhi ya wenye kujinasibu kuwa wanachama, zimekuwa zikisikika.

6. Imekuwa ni kama zogo la magenge ya wahuni.

7. Hali hii haiwezi kuwavutia wenye akili zao kwa binafsi zao au hata kwa makundi yao.

9. Ukombozi unahitaji uungwaji mkono kutokea makundi mbalimbali hasa asasi za dini, kiraia, nchi, vyama washirika, nk.

10. Uhuni au wahuni hawawezi kuwa sehemu, kwenye uvutiaji wa uungwaji mkono huo.

11. Hali hii haipaswi kuachwa kuendelea au hata kuvumiliwa.

12. Ni muhimu zikachukuliwa hatua sahihi zenye kuonekana ili kuweka nidhamu kamili chamani.

13. Wahuni hawawezi kuachwa kujinasibu kwa niaba ya chama kwenye lolote lisilokuwa na ridhaa ya chama.

14. "Lissu, Mbowe chukueni jukumu hili sasa."

CHADEMA inaweza kufanya vizuri zaidi na mno, kuliko kumwendekeza mhuni yeyote.

Mhuni ni mhuni tu!
Chadema ni chama mfu wacha kupoteza muda wako bure
 
Wahuni wote wenye matusi wapo upande wa Mbowe yaani ukimgusa mbowe utatukanwa mpaka basi. Lissu nina aminj hata uchaguzi ujao ana kazi kubwa kushinda maana yeye hana siasa Za kinafki kama za viongozi wengine.
Hebu nitajie members wa kundi la Mbowe, na members wengine wa kundi la Lissu nami niwafahamu..
 
Nimesema hivyo nina hakika,we nenda kule twitter mseme Mbowe kwa jambo la ukweli utaona hizo comment na pia mseme na Lissu kwenye jambo pia la ukweli au hata uongo utaona comment zake ,kisha rudi hapa tujadili.
Kama hiki ndio kigezo chako cha kusema Chadema kuna makundi umefeli, ina maana twitter kumbe inaongozwa na Mbowe na kundi lake, hilo sio kosa lake, na iweje hivyo, wakati kila siku tumekuwa tukiaminishana Lissu hana mpinzani, anakubalika kote, sasa iweje kule twitter akose watetezi?

Usichanganye mtu kutoa maoni yake na kuwa shabiki wa fulani, utambue, kama mtu huyo leo yuko upande wa Mbowe kwa jambo moja, kesho mtu huyo huyo anaweza kuwa upande wa Lissu kwa upande mwingine, usitengeneze makundi simply because fulani anatetea jambo usilopenda litetewe, au kama anafanya hivyo, mpinge kwa hoja, lakini usilazimishe wote tufanane mawazo kila wakati.
 
Unasema ni chama bora, alafu kwenye andiko lako unasema kimejaza wahuni!

Mbona unajichanganya sana?
Hivi katika chama cha siasa kipi bora, kuwa na wahuni wengi au kuwa na wanafiki wengi?
Mfano;
1. Chama kiwe kimejaa watu kama Martin Maranja Masesa.
2. Chama kiwe kimejaa watu wengi kama Suphian Juma ?
 
Kuna mjinga wao mmoja yupo kule twitter kazi yake ni kuwatukana watu mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu kama chadema wangekuwa watu makini Yule kijana mjinga angeshafukuzwa kitambo.
Huyu mjinga anakatisha Tamaa Sana na siasa zake za matusi
CHADEMA chukueni hatua dhidi ya kijana wenu Martin Masese huyu jamaa anawaharibia Sana na amevunja umoja wenu na wanachama wenu

Chama makini hakiwezi kuwa na wajinga kama huyo na msitegemee vijana kuwaunga mkono Kwa wapumbavu kama Martin

Na jee CCM wenye kijana kama Suphian Juma unadhani waungwana wanawafikiriaje hicho chama? Vijana wengi wamefedheheka na chama kutumia vijana wenye tabia kama zake kutetea chama.
Kuna msemo kuwa ukitaka kukijua chama au kikundi tazama wafuasi wake. Jee ccm tuijue kwa kumtazama huyo kijana?
 
Back
Top Bottom