Mkuu kwa maoni yangu nadhani ungetangaza upande wako wa kisiasa kabla ya hujaweka hoja yako hapa ili tuweze kuchangia kujadili hoja objectively.
Nianzie hapa kwenye "msingi" wa hoja yako.
a) Mkuu una maoni nje ya mada. Ni ustaarabu uliojengeka kujikita kwenye mada. Si kujihangaisha na mleta mada.
b) Huoni kama yakiendekezwa maoni yako, labda tuanze na wewe kujiuliza swali hilo hilo?
c) Kwani hata nikiweka utambulisho huo, si bila shaka utataka uthibitisho?
d) Fuatilia mada nzima kujiona kutambua kuwa:
"Huu ni ushauri wa bure kwa walengwa wawili. Yaani Mbowe na Lissu." Haipo shuruti.
e) Hata kama ni kweli kuwa labda wewe ni kiziwi au kipofu:
4. Haipo siri kuwa katika siku za karibuni hali inataka kuelekea kubaya badala ya kuliko tarajiwa (changamoto safarini).
11. Hali hii haipaswi kuachwa kuendelea au hata kuvumiliwa.
Mbowe, Lissu chukueni hatua kurejesha nidhamu kwenye chama
f) Kwamba wewe hujui kwenye jumuiko lolote nidhamu ni muhimu?
g) Kwamba umekereka kusikia kuitishwa nidhamu? Hivyo tuache mada tuanze kuongelea milengo ya kisiasa ya watu?
h) Wewe hautakuwa ni CCM au kibaraka wao kwa kujua au kutokujua? Bila shaka Lissu akiwaongelea watu kama wewe?
Tundu Lissu: Kauli ya Diaspora watuache ni ya CCM, anayesema kauli hiyo anafanya kazi ya CCM
i) Kumbe hoja zako zote zilizojengwa kwenye msingi usiokuwa na maana zitakuwa na thamani gani ndugu?
"Kimsingi kwa majibu yangu ningeishia hapa. Zaidi ya hapa ninaamua kukupa msaada kukusaidia tu."
"Wanasema, ukivuliwa nguo chutama."
Au nasema uongo yangu?
Nasema hivyo kwa sababu:
1. Huwezi kutoa ushauri chanya na wenye nia njema kwa mhindani wako.
a) Ushauri ni kwa Mbowe na Lissu si kwako au awaye yote mwingine. Si lazima. Kuuchukua au kuukataa, hiari yao. Sasa hapo mshindani wangu Mbowe au Lissu?
b) Ningekuelewa sana kama ungejikita kuwashauri kuuchukua au kuukataa.
c) kama unadhani maoni hapa ni kwa mujibu wa mlengo wa mtu kwanini yako yasiwe pia hivyo hivyo? Kwani mlengo wako uko hapa?
d) Bila kusahau hoja hapa tokea msingi mbovu, hoja yako hii Ina thamani gani?
2. Taasisi yoyote hai lazima pawepo na ushindani au misigino ya mawazo, hoja na fikra.
a) Tofautisha uliyoorodhesha na matusi. Zaidi sana zingatia maneno haya: "ridhaa ya chama:"
13. Wahuni hawawezi kuachwa kujinasibu kwa niaba ya chama kwenye lolote lisilokuwa na ridhaa ya chama."
b) Sambamba na hili nikualike kwenye uzi huu kuona uko nje ya mada:
CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni
3. Tofautisha mawazo, mitazamo na misimamo binafsi ya mwanachama dhidi ya taasisi husika.
a) Maneno
.. bIla ridhaa ya chama[ uliweza kuyaona mara zote?
13. Wahuni hawawezi kuachwa kujinasibu kwa niaba ya chama kwenye lolote lisilokuwa na ridhaa ya chama."
b) Maneno hayo hayo yamu humu pia:
CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni
c) Kulikoni kulia machozi ya mamba ndugu?
4. Tofautisha katika ya kukosoa, kufikirisha na kusema ukweli dhidi ya kutukana au kukashfu.
a) Kwamba hata ni siri ndugu? Kuwa hali siyo hii?
5. Kauli za kushangaza (kibri, matusi, kejeli, nk) kutokea kwa baadhi ya wenye kujinasibu kuwa wanachama, zimekuwa zikisikika.
6. Imekuwa ni kama zogo la magenge ya wahuni.
b) Kwamba ni wewe peke yako ndiyo huoni hivyo? Kama ndivyo nikuitishe kujipapasa, kujisachi na kujiangalia vyema. Huenda unaweza kuwa mmoja wao!
5. Tuache watu aongee kwa uhuru ili mradi hawavunji sheria ya nchi. Tukubaliani kutofautiani bila ugomvi.
a) Wapi unasoma kuzuiliwa kuongea au hata kuzuiliwa kuvunja sheria za nchi kama ndivyo wanavyotaka?
5. Kauli za kushangaza (kibri, matusi, kejeli, nk) kutokea kwa baadhi ya wenye kujinasibu kuwa wanachama, zimekuwa zikisikika.
6. Imekuwa ni kama zogo la magenge ya wahuni.
b) Kwamba ni maoni yako haya yaachwe kuendelea kwa ridhaa ya chama? Kwamba ni kwa maono yako huo ni uhuru wao?
c) Zingatia maneno haya:
13.Wahuni hawawezi kuachwa kujinasibu kwa niaba ya chama kwenye lolote lisilokuwa na ridhaa ya chama.
d) Tunachokataa ni kujinasibu kwa jina la chama na bila ridhaa kama ndicho kinachotokea labda kama ridhaa hiyo wanayo:
CHADEMA wakaneni hadharani chawa hawa wa mitandaoni
(e) Au wanayo ridhaa ya chama ndugu?
Kumalizia tusitake taasisi shindani ifanane na taasisi tuliomo kwa itikadi, mawazo, mitazamo na misimamo. Hiyo itakuwa midoli sasa!
a) Kumalizia nikukumbushe kuwa hitimisho lako hili kutokea kwenye msingi dhaifu mno, halina thamani yoyote.
b) Zaidi sana kwa sababu naona yawezekana hukusoma vizuri, ninakazie kwa kuyaweka haya hapa chini:
"11. Hali hii haipaswi kuachwa kuendelea au hata kuvumiliwa.
12. Ni muhimu zikachukuliwa hatua sahihi zenye kuonekana ili kuweka nidhamu kamili chamani.
13. Wahuni hawawezi kuachwa kujinasibu kwa niaba ya chama kwenye lolote lisilokuwa na ridhaa ya chama.
14. "Lissu, Mbowe chukueni jukumu hili sasa."
CHADEMA inaweza kufanya vizuri zaidi na mno, kuliko kumwendekeza mhuni yeyote.
Mhuni ni mhuni tu!"
Koleo ni vyema kuliita kwa jina lake mapema asubuhi, kuliko kukomalia kujidanganya vinginevyo.
Habari ndiyo hiyo.