Kama hiki ndio kigezo chako cha kusema Chadema kuna makundi umefeli, ina maana twitter kumbe inaongozwa na Mbowe na kundi lake, hilo sio kosa lake, na iweje hivyo, wakati kila siku tumekuwa tukiaminishana Lissu hana mpinzani, anakubalika kote, sasa iweje kule twitter akose watetezi?
Usichanganye mtu kutoa maoni yake na kuwa shabiki wa fulani, utambue, kama mtu huyo leo yuko upande wa Mbowe kwa jambo moja, kesho mtu huyo huyo anaweza kuwa upande wa Lissu kwa upande mwingine, usitengeneze makundi simply because fulani anatetea jambo usilopenda litetewe, au kama anafanya hivyo, mpinge kwa hoja, lakini usilazimishe wote tufanane mawazo kila wakati.