Mbowe, Lissu, Dkt Kitima, Jenerali Ulimwengu, Dkt Slaa - ni wapotoshaji kuhusu DP World?

Hao ndio wanaookoa jahazi tuwasikilize kwa umakini mkubwa.
 
Yaani wewe ndiyo umewapinga hapa? Hoja zako ziko wapi? Au unatumia uhuru wako wa kikatiba? Wewe na Lusinde mnatofauti gani zaidi ya kutofautiana wingi wa makamasi?

Halafu umesahau kuweka namba yako ya simu hapo chini.
 


Acheni kila mtu aongee anachotaka because mfumo ndio uko hivyo

Ilitakiwa before anything kufanyika kwanza wataalamu wetu watupe uelewa, waitishe mikutano, kuwe na majarida, kuwe na makongano

Sasa wataalam wote wapo kimya wamewaachia wanasiasa unategemea nini?

Walishindwa nini since day one kuweka papers on the table na kupata maoni?

Sasa kila kitu done ndio mnakuja kuleta hoja mfu

Acheni waongee the way wao wanaelewa

Hata wewe mwenyewe unaongea mambo ambayo huyajui

Hata nakala ya makubaliano hauna
 
Hiyo alama ya kuuliza umeweka ya nini kwenye kichwa cha habari kama umehitimisha hoja kwenye ufafanuzi? Au hujui matumizi yake.!!
 
 
Na ukitoka hapa unaenda kulipwà et???
 
Hiyo alama ya kuuliza umeweka ya nini kwenye kichwa cha habari kama umehitimisha hoja kwenye ufafanuzi? Au hujui matumizi yake.!!
Msamehe ni wengi tu hawajui matumizi ya alama hasa zifiatazo. !, ?, ; na '. Mfano ng'ambo (n'gambo).
 
Sawa jibu hoja zao...

Mosi mkataba ni muda Gani?
Miez 12?
Miaka 5?
Miaka 50?
Toa huu ukakasi kwanza then tuje na hoja nyingine
Chukulia UN. Sisi ni wanachama tangu 1961 bila kutajwa ukomo. Ndani ya UN kuna miradi ya malaria (WHO) miaka 5. Kuna ya mazingira ( UNEP) miaka 3. Na kila miaka 5 kuna Uchaguzi mradi wa UNDP mwaka mmoja. Baadaye itakuja miradi ya ukimwi na ya climate change (miaka mingapi, lini, hatujui). As long as tu wanachama wa UN miradi itazidi kuja, Inshaallah. Hatuna sababu ya kutoka UN wala wao kutufukuza, kwa hiyo kutaka kujibu maswali yako ni vigumu.
 
Hyo sio UN mkataba ni Tanzania na DP..wewe acha kuish Kwa madhaanio..
 
Wapuuzi sana na vile wote ni Wapinzani wanatafuta kiki
 
Badala ya Kujadili Hoja kwanini ni Mzuri unajadili watu kwamba ndio wanapotosha; Jibu Hoja zao ;

Na hoja yangu ni kwamba kwanini tusiwape kule Tanga au Kigoma; na kama issue ni Technical Know How kwanini watu wetu wasipate hio technical know how...

Issue kama ni mitambo wao ndio wana exclusivity ya kununua mitambo ? Kama issue ni kuendesha manpower sisi hatuwezi tunashindwa nini kuwaleta kama expatriates watufundishie watu wetu ?

Sisemi hili ni baya na kila kitu tufanye ndani ila cancer ya kwamba hatuwezi kila kitu na tufanyiwe nachelea kujiuliza ni kipi tunaweza.....

Kama tumeshindwa kuwasimamia watu wetu wenyewe wanapofuja hao tutawabana vipi ? Kama incompetence ni serikali kwa kufanya hivi ndio itakuwa competent....

Yanayofanyika sasa ni kujaribu ku-band aid a leg which needs amputation...
 
Kapeleka ripoti Kwa mabwana zake 😁😁
 
Sawa jibu hoja zao...

Mosi mkataba ni muda Gani?
Miez 12?
Miaka 5?
Miaka 50?
Toa huu ukakasi kwanza then tuje na hoja nyingine
Muda katika mkataba ni jambo muhimu sana. Makaratasi yanayoonyeshwa hayana kipengere cha muda. Sawa kabisa. Hii maana yake ni kuwa HAKUNA MKATABA na kwa ujumla kuita hayo makaratasi mkataba ni kupotosha
 
Nakubali tena si watu wa kuwasikiliza. Hawafai kabisa na ni maadui wa taifa na utu.
 
Ungekua karibu ningekutia vibao,shenz
 
Kelele zipo huku JF na katika mitandao mingine ya habari. Hao wenye kujielewa walioongea wakiwa panelists jana ni watu wenye upeo mpana wa mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…