Mbowe: Mama! Mama! Mama! Kwenye hili HAPANA

Mbowe: Mama! Mama! Mama! Kwenye hili HAPANA

Alitaka kujifurahisha nafsi yake zaidi
Huu ni mtazamo wako! That guy kwa tafsiri nilionayo alikuwa a solid leader! Sio mtu wa ku meander ama ku compromise...Sasa watu wengi walizoea utawala wa kuwa baby sitted kudekezwa kwake hakuwa na hilo! Ni kama baba wa Kambo🤣🤣🤣
 
Uchumi uendelee kujengwa lakini na mambo mengine lazima yaendelee!Tusitoe mwanya wa hivi maana itakuwa kisingizio cha kila Rais akiingia madarakani!
Kwenye suala la katiba kidogo anahitaji some space maana ni suala la kibajeti pia ila mikutano ina athari gani kiuchumi sasa yani kusema tu au leo hii mikutano ingekuwepo uchumi utazidi shuka???
 
Nyie watu hivi mna huruma Kama binadamu nyie. Mbona mmejawa na chuki kwa kiwango cha kupitiliza???

Mkuu Jumbe Brown ni Chawa mpya. Huyo ni chawa wa mama si chawa wa mwendazake.

Kuna tofauti ya kumwunga mkono mama na kuwa Chawa wake. Ninamwunga mkono mama lakini siyo chawa wake:

 
Acha uongo,pesa ilikuwepo hadi kwa waosha vioo vya magari barabarani!
Ajira kama sekta ya Afya na Elimu ilikuwa uhakika,kulikuwa hakuna kuapply bali watu walisubiri kupangiwa tu vituo vya kazi mara baada ya kuhitimu!
Au ulikuwa mdogo?
Kwahio sahizi pesa za waosha vioo vya magari hamna chief? Au we huwapagi tu?

Hilo la afya na elimu uko sahihi! Ila uchumi haukuwa wa afya nakwambia hata sasa hali ile itajirudia sababu mianya ya rushwa inaenda kufunguliwa vizuri kwahio watu watapiga hela soon utaanza kuona mtaani kila mtu ana hela. Wacha uoga upungue pungue zaidi watu wanze kujichotea mabillion ya serikalini!
 
Wanachokipigania kitakusaidia na wewe, swala la katiba haliwahusu mbowe peke yake hata mm mwanaccm linaniusu, wakati fulani itikadi ni vyema tukaweka pembeni
Mkuu haya Majinga hayaoni mbele...

Wale Mbung'o wa Bungeni Wakifanya mikutano na Sisi Tunafanya nao.
 
Mnamuona faala sasa mwamsheni halafu muanze kutupigia kelele kila anayekuja kwenu m baya hata dunia itawashangaa, nilijua tu hii mara mbeya mara wapi haina jema mlikuwa mnapima upepo, ingieni barabara mtakwenda wasimulia wake zenu, Sisi tupo watoa pole
Waache tu kudaadeki zao
 
Mama amekwishasema yeye yoyoooo people power na ulevi wa Konyagi na mwenyekiti milele wasubiri.Big up mama na mkimtest hapigi na mikanda kama Baba atawafinya na kuwamwagia radhi mpate laana.
Swala la katiba sio swala la mtu binafsi ni swala la kitaifa, na hata wewe unahitaji katiba mpya
 
Mkuu saivi nikimuona anasogea namzuia,gari naosha mwenyewe nikipata nafasi!
So hata mzunguko kwao umepungua,watu wamekuwa wagumu kweli!
Braza hata jero hutoi mzee baba😂😂😂 acha hizo bana kaka! Mie sio fan wa kupeleka gari car wash ila dah nawapaga coin wale madogo
 
Exactly,ndiyo point yake huyo zuzu. Halafu watu tukisema nchi kuongozwa kwa "mfumo wa mtu mmoja" ni upumbavu wa hali ya juu,wanasema tunakosea.
Mh. Rais Samia akitaka hii nchi ipige hatua kikweli kweli, basi aruhusu kutengenezwa kwa "mfumo wa pamoja". Na mfumo unaanza kutengenezwa kwa katiba ya wananchi.
Ni kweli mkuu lakini kutengeneza katiba ni mchakato ambao hawezi kufanyika ndani ya miezi 3
 
..Mama ameteleza.

..Eti anarekebisha uchumi!

..Na kutengeneza ajira!!

..hizo ni kazi ENDELEVU, hufanyi miezi miwili mitatu halafu ukapumzika.

Nasio tu utelezi Kwenye hili

Changamoto amezikaribisha

Sasa atakumbana na mijadala

Na hata safari zake watakuwa wanamuuliza the same

Kazi imeanza kwake
 
Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako,mambo wanayodai wapinzani yapo kwenye Katiba au hakuna?tuanzie hapo,
Haya mambo ya kusema niache nijenge uchumi kwanza,haki za binadamu na kisiasa baadae,ndiyo yaliyotuletea Chato kuwa mkoa,airport ya Chato,wasiojurikana,1.5tilioni kupotea.
Na uchumi huo utajengwa mpaka lini???? Mbona tunadanganywa kama watoto wadogo, magufuli alisema hivyohivyo, Amepita badala ya uchumi kupanda ndo kushuka, leo na mama Naye anajenga uchumi, mpaka lini????
 
Na uchumi huo utajengwa mpaka lini???? Mbona tunadanganywa kama watoto wadogo, magufuli alisema hivyohivyo, Amepita badala ya uchumi kupanda ndo kushuka, leo na mama Naye anajenga uchumi, mpaka lini????
Mpaka uwe sawa 😂😂😂 nafikiri kwenye 2028 mwishoni utakuwa umeshakaa sawa kidogo kwahivyo tutaanza mchakato wa rasimu ya katiba mpya!
 
Mdude Nyagali ametoka RUMANDE kwa huruma ya mh.Rais Samia Suluhu Hassan......

Masheikh wa UAMSHO wanakula biriani mtaani kwa sababu ya huruma ya mh.Rais Samia Suluhu Hassan......

Mbowe amefutiwa kesi yake na kurudishiwa milioni zake 300 kwa sababu ya huruma ya mh.Rais Samia Suluhu Hassan......

Kwani MDUDE NA WENZAKE wangeendelea kukaa RUMANDE kingebadilika KIPI huku mitaani ?!!!!!!


#ChademaWameanzaKubeep
Kwa hiyo hata tigo waweza kug@w@ simply because mama kafanya hili na like.
Mke waweza mgawa simply because ushafanyiwa mawili matatu mazuri
pathetic
 
Braza hata jero hutoi mzee baba😂😂😂 acha hizo bana kaka! Mie sio fan wa kupeleka gari car wash ila dah nawapaga coin wale madogo
Mkuu hadi fungu la 10 nimelipinga panga sana!Yaani nimebana kila kona kiasi kwamba ninaokoa kama 250,000/= kila mwezi kutoka kwenye bajeti yangu ya awali!
 
Kimoyo moyo una kubali kuwa bila yeye matakwa yenu mengi yasingefanikiwa.
Uamsho
Mdude
Kina mbowe kurudishiwa fedha zao
Kesi ya kina Tito magoti na mengine mengi. Si mlikuwa mnapigania siku nyingi na amelegeza kamba. Kwanini unabisha tu ili mradi ubishe? Chadema bwana...
Na bado Kuna mambo mengi tu kutwa mnamuomba mama alegeze, analegeza na bado mnamponda

Nimekosa makubwa kuwachapa fimbo watoto kwasababu unawalisha na kuwapa makazi bila makosa

Haki hazilinganilishwi, kwamba sababu nakupa hiki basi nakuchinja
 
Mkuu hadi fungu la 10 nimelipinga panga sana!Yaani nimebana kila kona kiasi kwamba ninaokoa kama 250,000/= kila mwezi kutoka kwenye bajeti yangu ya awali!
Fungu la kumi hilo nalo achana nalo bana😅😅😅 yani unampelekea hela Mc Pilipili au Masanja mchekeshaji?

I would advise you to take the sum to orphanage centres!
 
Back
Top Bottom