Mbowe: Mama! Mama! Mama! Kwenye hili HAPANA

Mbowe: Mama! Mama! Mama! Kwenye hili HAPANA

Sikubali UNAFIKI mimi wa yeye kuukumbatia udikteta huku akienjoy utamu wa kitumbua chake kisha kutaka kujifanya anajiweka mbali na maovu ya dhalimu magufuli wakati huo huo anashindwa kuwachukulia hatua muafaka wahuni wote waliowabambikia kesi masheikh wa uamsho, Viongozi wa Chadema, Mdude na Watanzania wengine chungu nzima.
Narudia mama huyo ni dikteta hafai kuaminiwa hata chembe. Miezi mitatu inatosha sana kujua mtu mwenye nia njema na Watanzania au mwenye nia OVU. Samia ana nia OVU na Watanzania ya kuendelea kuminya uhuru na haki zetu za kuchagua Viongozi tuwatakao bila kuingiliwa na mtutu wa bunduki au Tume FAKE ya uchaguzi.
Unalaana ww

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Kwanza kabisa Mbowe, huyo ni Rais, si Mama yako.

Ukishaanza kumuita Mama utamuonea aibu kumnanga.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Watanzania kama wewe msiojua haki zenu za uraia ni tatizo kubwa sana la hawa wahuni kung’ang’ania madaraka.
Fikra za kijinga kabisa hizi, so mtu anaejenga uchumi ni lazima aumize watu?

Unaleta quotation ya kipuuzi kabisa humu.
 
Jiulize Mkuu hao waliohusika polisi na wanasheria kubambikia kesi FAKE Serikali haiwajui? Unadhani kwanini hawapandishwi kizimbani ili kujibu tuhuma dhidi yao ya kubambikia Watanzania kesi FAKE? Kama wametenda maovu kinyume na sheria za nchi kwanini waendelee kupeta mtaani? Kwanini hawafukuzwi kazi!?
Lakini kwanini hukumu kama hizo zinatoka awamu hii?mbona awamu iliyopita hazikutoka kwani ushahidi kama huo haukuepo au majaji hawakuwepo?
 
Sasa Mbowe anaomba au anapambania haki? Hakuna mtu atatoa ulaji wa bure kwa mshindani wake .

Yeye anatakiwa apambane,ccm ni wale wale
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Zinapigwa pote pote😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Hao waliohusika kuwabambikia kesi mbona kapiga kimya? Wametumia nyadhifa zao vibaya kubambikia watu kesi. Kwanini waendelee kuajiriwa na Serikali? Kwanini hawafunguliwi mashtaka?

Mathalani tungeambiwa hao wote amewatoa kwa huruma yake nani angemuelewa ? Lazima zitumike sababu za kufunika kombe mwanaharamu apite kama hizo za kutokuwa na ushahidi na mfano wa hayo.

Katika nchi zilizo pea watu kama Mbowe na mfano wake,hawatakiwi kudekezwa,naichukia sana Demokrasia.
 
Hao waliohusika kuwabambikia kesi mbona kapiga kimya? Wametumia nyadhifa zao vibaya kubambikia watu kesi. Kwanini waendelee kuajiriwa na Serikali? Kwanini hawafunguliwi mashtaka?
Ilipaswa hadi IGP awajibike na ashtakiwe
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Alidhani Watanzania wote ni wajinga hivyo uongo wake wa kujenga uchumi utakubalika.
Mkuu BAK:


Mbona tuko vizuri? Nini kimebadilika?
 
Mdude Nyagali ametoka RUMANDE kwa huruma ya mh. Rais Samia Suluhu Hassan......

Masheikh wa UAMSHO wanakula biriani mtaani kwa sababu ya huruma ya mh. Rais Samia Suluhu Hassan......

Mbowe amefutiwa kesi yake na kurudishiwa milioni zake 300 kwa sababu ya huruma ya mh. Rais Samia Suluhu Hassan......

Kwani MDUDE NA WENZAKE wangeendelea kukaa RUMANDE kingebadilika KIPI huku mitaani ?!!!!!!


#ChademaWameanzaKubeep
Kwa hiyo nchi na maisha ya waTanzania yategemee fadhira na huruma ya huyo huyo Rais Samia Suluhu Hassan...

Kuna watu kama nyinyi nadhani huko vichwani kwenu hakuko sawa kabisa kama hamuoni upotofu huu.
 
Kabisa Mkuu badala yake watenda maovu wote waliohusika kubambikia kesi polisi na wanasheria wa Serikali bado mama kawakumbatia. Anaogopa kuwafungulia mashtaka anaogopa kuwafukuza kazi.
Ilipaswa hadi IGP awajibike na ashtakiwe
 
Kabisa Mkuu badala yake watenda maovu wote waliohusika kubambikia kesi polisi na wanasheria wa Serikali bado mama kawakumbatia. Anaogopa kuwafungulia mashtaka anaogopa kuwafukuza kazi.
Anachofanya ni kuwabadilishia tu maeneo yao ya kazi tena wengine anawapandisha vyeo kama alivyofanya kwa DPP mganga
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kwa hiyo MBOWE akisema HAPANA ndio anawasemea WATANZANIA WOTE?!!!

Hapana yake ni ya KIJINGA TU.....walisema HAPANA....na hawakutokea pale UBUNGO.....asimbabaishe mtu bana....

#KaziInaendelea
Hapana ukisema wewe ndo tutakusikiliza wewe ni msaidizi wamalaika
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kitu ambacho si sawa hata kidogo hao ni wahalifu wanastahili kufukuzwa kazi mara moja na kufunguliwa mashtaka kwa uhuni walioufanya lakini mama anahofia anajua litakuwa balaa ambalo litamgusa na yeye moja kwa moja. Mbona ulikuwa kimya ulipokuwa VP? Hii miezi mitatu ya wewe kuwa madarakani umewezaje kujua kesi zote hizo zilikuwa ni FAKE hivyo umeamua kuzifuta ndani ya miezi mitatu tu?
Anachofanya ni kuwabadilishia tu maeneo yao ya kazi tena wengine anawapandisha vyeo kama alivyofanya kwa DPP mganga
 
Back
Top Bottom