Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Mbowe anasema wanaosema aachie madaraka wakome, hajachoka, bado ana nguvu za kutosha na kuweza kufanya mikutano 8 kwa siku bila kula, kama kuna mtu ana nguvu kama yeye ajitokeze.
Mbowe asema ukomo wa madaraka ni watu wanaokutaka au kukukataa, na huu ndio ukomo halisi wa demokrasia. Kuna watu wakiongoza mara moja wanakataliwa, lakini wengine wanachaguliwa tena na tena, hawawekewi ukomo kwa sababu watu wanawataka.
Pia soma: Pre GE2025 - Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura
Kama wanachama wanamtaka kiongozi fulani wewe ni nani kusema huyu amekaa miaka mingi aondoke?
Mbowe asema kuwa chama cha upinzani siyo kazi rahisi, ni kazi ambayo inahitaji watu waliyokuwa tayari na siyo kazi ya ukomo, ni kazi ngumu, kwahiyo watu wote wanaofanya kazi hiyo hawapaswi kubezwa wakati wowote, wanapaswa kupongezwa na kutiwa moyo kwasababu hawajajiweka wenyewe kwenye madaraka lakini pia wanafanya kazi ngumu ambayo watu wengi wanaikimbia, hivyo mmoja anatakiwa kupewa haki ya kugombea.
Mbowe ameongeza pia makelele ya mtandaoni hayamnyimi usingizi, anachoangalia ni kukijenga chama, na kuwaonya wanaoendelea kumtukana wasije kufikishana pabaya baada ya uchaguzi