Pre GE2025 Mbowe: Mimi sijachoka, ukomo wa madaraka ni watu wanaokutaka au kukukataa

Pre GE2025 Mbowe: Mimi sijachoka, ukomo wa madaraka ni watu wanaokutaka au kukukataa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Mbowe anasema wanaosema aachie madaraka wakome, hajachoka, bado ana nguvu za kutosha na kuweza kufanya mikutano 8 kwa siku bila kula, kama kuna mtu ana nguvu kama yeye ajitokeze.

Mbowe asema ukomo wa madaraka ni watu wanaokutaka au kukukataa, na huu ndio ukomo halisi wa demokrasia. Kuna watu wakiongoza mara moja wanakataliwa, lakini wengine wanachaguliwa tena na tena, hawawekewi ukomo kwa sababu watu wanawataka.

Kama wanachama wanamtaka kiongozi fulani wewe ni nani kusema huyu amekaa miaka mingi aondoke?

Mbowe asema kuwa chama cha upinzani siyo kazi rahisi, ni kazi ambayo inahitaji watu waliyokuwa tayari na siyo kazi ya ukomo, ni kazi ngumu, kwahiyo watu wote wanaofanya kazi hiyo hawapaswi kubezwa wakati wowote, wanapaswa kupongezwa na kutiwa moyo kwasababu hawajajiweka wenyewe kwenye madaraka lakini pia wanafanya kazi ngumu ambayo watu wengi wanaikimbia, hivyo mmoja anatakiwa kupewa haki ya kugombea.

Mbowe ameongeza pia makelele ya mtandaoni hayamnyimi usingizi, anachoangalia ni kukijenga chama, na kuwaonya wanaoendelea kumtukana wasije kufikishana pabaya baada ya uchaguzi
Safi mwambaaa,
Wenye nongwa wajinyongeee
 
CHADEMA kwishney
Kura bado sasa kwishney ya vipi ,hakuna sababu ya kumlazimisha mtu asigombee acha kura ziongee, kazi kwa wajumbe sasa ,kukivusha chama au la ,simple.

Ninachojua lissu penye ugum ndo huwa anapenya ,mnakumbuka lile kipindi kile anagombea TLS alikutana na vikwazo vingapi na kushinda?
 
Hamjaanza leo kusema upinzani umekufa.
Mbowe ni mwamba Imara, ni jabali.
We kaandani na mumeo muache mbowe akapige kazi
Imara gani? Walau Lissu alikua anakipa uhai chama ila huyu Mbowe hana new ideas na siku akifariki ghafla utatokea ugomvi mkubwa sana wa madaraka. Bora angepisha mapema wagombee wengine ili awape mentorship akiwa bado yupo Hai. Mbona Odinga kapisha na zito kapisha why ahodhi madaraka mpaka leo?

Hiki chama ndio mwisho wake huu.
 
Sasa hawa jamaa huwa wanahubiri ya nini kuhusu demokrasia? Kumbe ukomo ni watu? Hii downfall ya hawa jamaa inapaswa kufundishwa mashuleni
Huu uchaguzi umetu expose sana unafiki wetu. Wanasema ubunge, udiwani na ngazi za chini uwe na ukomo wa awamu tatu mind you tulipinga JPM kuongezewa muhula. Cha ajabu leo tunapinga maneno yetu yale yale

So embarrassing
 
Back
Top Bottom