Pre GE2025 Mbowe: Mimi sijachoka, ukomo wa madaraka ni watu wanaokutaka au kukukataa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hizo nafasi ni tamu na zinalipa....sio rahisi mtu kuachia.

It's never about people, it's all about money and power.
Jamaa wanafanya biashara haswa, jiulize CHADEMA 2015-2020 ilikuwa inapata ruzuku ya 350M nje na michango lakini haikuweza kujenga vitega uchumi vyake inamtegemea Mbowe pekee, ni utapeli tupu
 
Kwani katiba inasemaje mzee? Mbona unajitoa ufahamu.
Kama katiba inaruhusu njia pekee ni kuibadili katiba ili ikizi matakwa.
Mbowe alisema ukomo wa madaraka sio issue kama watu bado wanampenda kiongozi meaning it doesn't matter katiba ina kubali au kukataa ila ukomo ni subjective.

Cha ajabu kwa JPM walipotaka badili katiba kuondoa vipindi viwili vya urais alipinga wakasema ni udikteta. Ndio sasa hizi double standards ndio tunapinga.

Kuhusu tubadili katiba, yes ndio ajenda ya Lissu kwamba akiingia ukomo unarudishwa maana chama kim3shakua sana
 
Jamaa wanafanya biashara haswa, jiulize CHADEMA 2015-2020 ilikuwa inapata ruzuku ya 350M nje na michango lakini haikuweza kujenga vitega uchumi vyake inamtegemea Mbowe pekee, ni utapeli tupu
Ndio nashangaa yaani tulikua na pesa nyingi ila eti bado Mbowe ndio kila kitu kufadhili chama. Huu ni ujinga, tunahitaji mabadiliko kwenye chama.
 
Jamaa wanafanya biashara haswa, jiulize CHADEMA 2015-2020 ilikuwa inapata ruzuku ya 350M nje na michango lakini haikuweza kujenga vitega uchumi vyake inamtegemea Mbowe pekee, ni utapeli tupu
Na ndiyo maana hawezi kuondoka kwenye hiyo nafasi kwa sababu anajua umuhimu wake kwenye mzunguko wake wa pesa na fursa zinazo pitia kwenye siasa...

Huyo bado yupo yupo sana kwa sababu CHADEMA kwake ni uwekezaji.
 
Jamaa ametukata maini asee
 
Hoja hii hii CCM itumieni kuendelea kukaa madarakani. Kiufupi wameyatimba wenyewe😆😆😆😆
 
Kwahiyo tusiwasikie tena mkitoa hoja kuhusu lipumba, spunda, cheyo nk.
Leo Chadema mnabariki u ayattolah!
Nyumbu hovyo kabisa.
 
Ni sahihi ila kama katiba inaruhusu acha ifuatwe hadi hapo watakapo badili. Ya magufuli ilipingwa kwa kuwa katiba haikuwa inaruhusu.

Huyu Lissu ni walewale, yupo chadema kitambo hajawahi kukisaidia chama kuboresha katiba. Leo anaona inampa wakati mgumu ndio anaanza kupiga kelele.

Kila siku tunasema sheria zitungwe sio zinamsaidia nani kwa wakati huo bali ziwe zinasaidia sawa na baadae kwa kila mtu.

Wakimaliza hili, iwe lisu kushindwa ama kushinda kama wanaona ajenda ya ukomo ni mhm basi waibadilishe.
 
kwa kuwa katiba haikuwa inaruhusu.
Ya chadema ilikua hairuhusu lakini mbona ikabadilishwa? Katiba sio Biblia au Quran kuwa haiwezi kuwa edited. Sasa Mbowe anasema muhula sio issue kama watu bado wanakupenda (hajaongelea katiba inamruhusu) meaning hata kwa JPM kama kuna watu walikua wanampenda ilikua sahihi aongezewe mihula.

Huu ndio unafiki naopinga,
 
Huyu Lissu ni walewale, yupo chadema kitambo hajawahi kukisaidia chama kuboresha katiba. Leo anaona inampa wakati mgumu ndio anaanza kupiga kelele.
Mbowe aliahidi kupisha 2023 kwahiyo walijua tu kufikia 2024 wangeshabadili katba na kuchagua viongozi wapya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…