Mbowe, mkanye Lissu

Lisu anaandika yaliyo moyoni mwake, mimi nimemuelewa kuwa hataki unafiki. Ningeshangaa sana kama Lisu angemsifia JPM na kwa kweli angekuwa mnafiki wa hali ya juu.
Wapo watu humu wanajifanya kumlilia JPM hadharani lakini ungeweza kufungua mioyo yao ungeona unafiki mtupu; nadhani ndiyo maana serikali iliamua kutangaza kwa nguvu zote kuwa kipindi hiki watu wasifanye sherehe yoyote. Kwa utamaduni wetu hatukupaswa kuambiwa hili kwani kwenye majonzi huwa hatufanyi sherehe lakini hadi serikali inaamua kutangaza hivyo basi iliona kuwa kuna watu watafanya sherehe na hao hao kabla ya msiba walikuwa mbele kusifia.
Ni suala la muda tu yote yataisha
 
Meko kafa huku Lissu (aliyekuwa amepangiwa na kina farao afe) bado yu hai. Huyo ndiye Mungu!
Kwani kufa ni adhabu? Mbona hamtaki kumaliza masomo ya shule za msingi kabla ya kujiunga na kumbi kama hizi?
 
Kwani kufa ni adhabu? Mbona hamtaki kumaliza masomo ya shule za msingi kabla ya kujiunga na kumbi kama hizi?
Kama kufa si adhabu mbona alimmiminia mwenzie risasi 16? Ona sasa kilichomfika!
 
Hayo mambo ya hadhi hebu weka pembeni kwanza. Subiri amalize!
 
kama mnakumbuka kipindi cha Bunge la Katiba Tundu Lissu alimtukana Hayati Mwalimu Nyerere sasa yupo tena Hayati Magufuli, naamini angekuwa na fedha anamdai pia angeenda kumshtaki hayati. Eti huyu alitaka kuwa Rais wa Tanzania shame on him
 
Ungekuwa ni wewe ulipigwa risasi ukanusurika kufa ungepangiwa cha kuongea? Ungekuwa ni wewe umefanyiwa uonevu unyanyasaji uovu kibao ikiwemo kubambikiwa kesi kibao kisha upangiwe cha kuongea ungekubali? Ebu jaribu na wewe upitie mateso kama aliyopitia Lisu ndipo utajua kuwa alichokiandika hapo juu hukuzingatia haki za binadamu zaidi ya kusaka uteuzi kwa njia haramu za kishetani.
 
kama mnakumbuka kipindi cha Bunge la Katiba Tundu Lissu alimtukana Hayati Mwalimu Nyerere sasa yupo tena Hayati Magufuli, naamini angekuwa na fedha anamdai pia angeenda kumshtaki hayati. Eti huyu alitaka kuwa Rais wa Tanzania shame on him
Aliyekuwa Rais Mbona hakutumia demokrasia kama mkapa na kikwete? Kutumia wasiojulikana kupiga watu risasi ndiyo kaleta tabu zote hizi , kuwatumia task force kupora mali za watu, kufunga biashara za watu, Account za watu kuwapora cash zao kuwatishia kuwabambikia kesi za utakatishaji fedha uhujumu uchumi , huyo ndiyo Rais bora?
 
Ukiona mtu anashabikia Unyama unyanyasaji mateso aliyofanyiwa Tundu na utawala wa marehemu ujue huyo mtu ni mnufaika kupitia huo mfumo mateso, wanufaika wote sasa hawana Amani hawajui mama anawaza nini juu yao
 
Huyo anaweza akarudi Tz wananchi wenye hasira Kali wakamuteka bila serikali kujua
Hakuna mwananchi mjinga kiasi hicho wananchi wenye Akili timamu wanajua machungu ya kunusurika kuuawa wanafahamu machungu ya kubambikiwa kesi, uonevu unyanyasaji uovu wote aliofanyiwa Tundu lisu
 
Natamani lisu aseme zaidi kwa upande ule wa (wasiojulikana)
Baada ya mch. Mtikila sasa yupo lisu, asiposema lisu kuna mzalendo gani mwingine anaweza sema na hata kujulikana wote waliokuwa (wasiojulikana)?

Ni kama kuna fukuto mioyoni, kuna vitu vingi watu wanatamani kuujua ukweli na kuona hatua stahiki zikichukuliwa.
 
Wewe ndiyo huna Akili hata za kuazima tu kwa polepole, Yaani ulitaka mtu apigwe risasi aporwe ubunge anyimwe haki zake abambikiwe kesi kibao kisha akae kimya? akae kimya ili iweje? Unyanyasaji unyama wote huo haujauona? Acha kujitoa fahamu kiasi hicho
 
Ulaya America wameendelea kwa kuambizana ukweli la cha ajabu Tanzania msema ukweli huwa Adui wa CCM na hata kupigwa risasi
 
Sasa walio mpiga risasi mbona Ni Ngozi nyeupe ili wachafue inchi kama walivyo fanya inchi Za kiarabu
Hii propaganda ni ya enzi zileee zamani sana wakati watanzania wamelala hawajaamka, sasa Tambua kuwa watanzania wana upeo mkubwa hizo propaganda zibakize huko huko kwa akina Le mutuz watu wenye IQ ndogo
 
mwendo ni ule ule kasi mpya ari mpya msitegemee mtelemko HAPA KAZI TU
Kazi kazi ni jambo jema lakini uonevu unyanyasaji mateso manyanyaso kwa wapinzani wakiiga vya marehemu lazima wataishia kufeli zaidi, warithi mazuri pekee yale mabaya waache azikwe nayo mwenyewe
 
Mimi nashauri aendelee hivyo hivyo kuropoka, atafanya nini zaidi ya hilo? Hebu mwacheni mbaba wa watu azidi kutema nyongo. Inapunguza machungu

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…