Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,903
- 1,360
Lisu anaandika yaliyo moyoni mwake, mimi nimemuelewa kuwa hataki unafiki. Ningeshangaa sana kama Lisu angemsifia JPM na kwa kweli angekuwa mnafiki wa hali ya juu.
Wapo watu humu wanajifanya kumlilia JPM hadharani lakini ungeweza kufungua mioyo yao ungeona unafiki mtupu; nadhani ndiyo maana serikali iliamua kutangaza kwa nguvu zote kuwa kipindi hiki watu wasifanye sherehe yoyote. Kwa utamaduni wetu hatukupaswa kuambiwa hili kwani kwenye majonzi huwa hatufanyi sherehe lakini hadi serikali inaamua kutangaza hivyo basi iliona kuwa kuna watu watafanya sherehe na hao hao kabla ya msiba walikuwa mbele kusifia.
Ni suala la muda tu yote yataisha