You have to keep an open mind! Ushahidi kwamba ameua mtu yeyote uko wapi? Kumtuhumu mtu bila ushahidi wowote ni chuki binafsi na uonevu.
Critics wengi wa serikali huuawa bila maagizo yoyote ya viongozi wakuu. Kuna mashabiki ambao hawaoni shida kumuondoa mtu ambaye wanadhani ni headache kwa kiongozi wanayempenda wao. Mashabiki wa aina ya wafuasi wa Trump, kwa mfano, hawahitaji maagizo yoyote kutoka kwa Trump kumfyekelea mbali mtu ambaye wanamuona ni tishio kwa kiongozi wao. Hawa ni wahalifu wanaoamini kimakosa kwamba matendo yao yana maslahi kwa taifa!
Hata mimi nikijianika mahali nikawa mkosoaji mkali sana wa Lissu au Mbowe, kila uchao, ninaweza kutekwa na kuuawa na wafuasi wao hata bila wao wenyewe kutoa maagizo yoyote. Hii ndiyo kasoro kubwa inayoambatana na ushabiki.