Pre GE2025 Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'

Pre GE2025 Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe akiwa kwenye mkutano wa waandishi uliohudhuriwa na wanachama wa CHADEMA asema wataanza na kampeni ya Samia Must Go ikiwa hakutakuwa na uwajibikaji kwenye matukio ya utekaji.

Mbowe pia ametoa rai kwa viongozi wa CHADEMA siku 12 kuanzia sasa kuja Dar kwaajili ya kupeana mikakati muhimu kwa hatua zaidi.

Soma Pia:

=====

"Kisiasa, n ani vyema mkasikia bunge la Tanzania, mwaka jana (2023) katika mabadiliko ya sheria ya usalama wa taifa ilipeleka usimamizi ya idara ya usalama wa taifa moja kwa moja Ikulu kusimamiwa na Rais, na sheria ile ilitoa kwa mara ya kwanza haki ya watu wa usalama wa taifa kukamata watu, kuwaweka kizuizini, bila kueleza mahali popote wala bila kushtakiwa.

"Sheria hii ilivyopitishwa Rais aliipitisha na akajimilikisha mamlaka ya usalama wa taifa. Sasa mimi kwa niaba ya CHADEMA na vikao na vikao vyangu, tuna declare mtu wa kwanza kuwajibishwa katika masuala hay ani Rais Samia Suluhu Hassan.

"Na sisi tunasema tunaanza moja kwa moja kampeni inayoitwa ‘Samia Must Go’, hiyo ndiyo rai yetu. Sasa basi, kwasababu bado tuna msiba, tumekubaliana kwamba tuna msiba kwasababu kuna viongozi wetu hatujui wako wapi. Kwahiyo sisi kama chama hatujamaliza msiba. Tutaendelea na msiba wetu kitaifa na bender azote za chama zitapeperushwa nusu mlingoti hadi tujue watu wetu wako wapi, wako hai au mauti

"Lingine, kuanzia siku ya Jumatatu, tar 23/9/2024 mkumbuke nilitangaza tar 21 tunategemea tuone hatua za watu kuwajibika zimeanza. Kama hawatachukuliana hatua wenyewe kwa wenyewe, sisi kuanzia tarehe 23 jiji lote la Dar es Salaam, kila kata kila mtaa.. ndugu zangu tumekuwa tunafanya utani mara nyingi, lakini kwa wakati huu hatuna utani.

"Kuanzia jumatatu sisi tutaingia barabarani kudai tunachoona ni uhai wa watu wetu waliopotenzwa unless serikali imechukua hatua za haraka na za makusudi kuwarejesha, watu kujiuzulu na watu wote kuwajibika kwa mujibu wa tamko letu la leo." -
Amesema Mbowe katika mkutano kwenye ofisi za CHADEMA, Mikocheni leo 11/9/2024

Safi sana
 
Ofcoz amegoma kuondoka, kuachia ngazi...

Lakini hebu kamuulize iwapo huyo William Rutto huwa analala hata usingizi kwa kashkash anazopewa na vijana GEN-Z...

Utamhurumia sana maana kuna wakati anajibizana na watoto wadogo huku wakimrushia kila aina ya matusi na hana cha kuwafanya maana ni majasiri, hawaogopi risasi wala bunduki wala mabomu ya machozi na wako tayari kufa...

Kwa kashkash hizo tuu ilimlazimu kunyoosha mikono juu na kufanya mabadiliko makubwa ktk serikali yake ikiwemo kuvunja baraza lote la mawaziri pamoja na reforms zingine muhimu ingalau kuridhisha madai ya vijana waandamanaji....

Unataka mama yenu Samia afikishwe huko?

Ofcoz, anaweza kugoma KUONDOKA au kutii amri ya umma ya "SAMIA MUST GO" lakini cha moto atakiona...

Mwambieni aombe HEKIMA kwa Mungu wake ili apate akili na ufahamu kutumia fursa ndogo aliyonayo kufanya the needful otherwise atabeba mimba ya stress na uzee wake huo muda si mrefu...!!
Watu tumewabembeleza walete katiba mpya wanatuona wajinga . Sheria wametunga wao hawazifuwati halafu bila aibu wanasema tii sheria bila suluti . Yaani mtu anaishi kwasababu ya sheria na katiba halafu haziheshimu. Hapo utasema tuna viongozi au vibaka?
 
Wacha tuendelee kutazama
Usikute mpaka sasa yeye mwenyewe hajui kuwa sio yeye!. Kuna vitu vingine wengine wanaambiwa kabla mhusika hajajua!.
Mfano angalia tarehe ya bandiko hili Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli wakati huo mwenyewe alikuwa hajui.

Hata hapa Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...
Hata hivyo niliisha muanda kisaikolojia kabla Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! huyo mwanamke anaweza kuwa ni Dr. Tulia!.
P
 
Ipo wazi maza anajua anachukiwa na raia, sasa kampeni ikianzishwa itaungwa mkono sana, ninachoona Mbowe anaweza kutulizwa kama sio kulambishwa asali basi atakamatwa.
 
Hiyo jumatatu haifiki.. Mbowe atadakwa kwa uchochezi.
 
"Kisiasa, n ani vyema mkasikia bunge la Tanzania, mwaka jana (2023) katika mabadiliko ya sheria ya usalama wa taifa ilipeleka usimamizi ya idara ya usalama wa taifa moja kwa moja Ikulu kusimamiwa na Rais, na sheria ile ilitoa kwa mara ya kwanza haki ya watu wa usalama wa taifa kukamata watu, kuwaweka kizuizini, bila kueleza mahali popote wala bila kushtakiwa.
Sijui kama mkuu 'Rabbon' ataisoma hii.
Hili ndilo jibu nililokuwa nikitafuta tokea juzi, naye (Rabbon' akawa ananizungusha mbuyu!.

Kwa taarifa hii hapa, ni wazi kabisa kwamba hiyo kazi ya "Kikosi Kazi" imepangwa toka juu kabisa. Huu ni mbango ulio andaliwa kwa maksudi, kama maandalizi ya kuelekea kwenye chaguzi zinazo fuata.
Hapa hakuna cha bahati mbaya, wala nani hajui.
 
Nadhani hiyo ni wrong approach ambayo itasababisha ccm wote waungane kumtetea m/kiti wao. Nice approach ni kumgombanisha sa100 na wanaccm wenzake.
Kwa nini wewe unafikiri CCM wote wanakubali upuuzi huu unaofanywa na vongozi wao?

Okoteza visababu vyako uchwara; lakini Samia hafai kuendelea kuwa kiongozi wa nchi hii.
 
Unawezaje kumtoa Mtu anayelindwa na Jeshi 24/7 ?
Unajidhalilisha sana kwa ujinga kama huu.

Hao viongozi ambao huondolewa madarakani huwa hawana jeshi?

Juzi juzi, yule mama wa Bangladesh alifurumishwa, hakuwa na jeshi?
Akina Omar Bongo huko Gabon, hawakuwa na jeshi?

Nchi inapo kuwa na wajinga wa namna hii ndipo huwa furaha kuu ya viongozi wabovu.

Sikiliza, wewe si lazima ushiriki. Kaa pembeni, subiri wenye uchungu na nchi hii wakufanyie kazi. Kwenye nchi yoyote ile, watu wa aina yako hawakosekani.
 
Huu ujinga ulioandika ndio wanaoutumia kuteka na kuua watu wakiamini watanzania watatulia tu. Usisubiri yakukute ndio ujie umuhimu wa kuchukua hatua kama hizi.
Sasa ndugu yangu, kuna vitu vinahitaji suluhisho la busara! Huwezi kutumia bad methods ukitegemea kupata matokeo chanya. 🙏🙏🙏✍
 
"Samia must go" ,na sio CCM must go!!.

Mbowe mjanja sana anakula huku na kule.
Mbowe mjinga tu ka copy and paste ya Kenya ya Ruto must go

Hana ubunifu wowote
Anadhani environment ya Kenya na ya Tanzania ziko sawa na anadhani watu w Kenya na Tanzania wanafanana

Tanzania haambulii kiti vijana wa Kenya na Tanzania tofauti sana
 
Mbowe akiwa kwenye mkutano wa waandishi uliohudhuriwa na wanachama wa CHADEMA asema wataanza na kampeni ya Samia Must Go ikiwa hakutakuwa na uwajibikaji kwenye matukio ya utekaji.

Mbowe pia ametoa rai kwa viongozi wa CHADEMA siku 12 kuanzia sasa kuja Dar kwaajili ya kupeana mikakati muhimu kwa hatua zaidi.

Soma Pia:

=====

"Kisiasa, n ani vyema mkasikia bunge la Tanzania, mwaka jana (2023) katika mabadiliko ya sheria ya usalama wa taifa ilipeleka usimamizi ya idara ya usalama wa taifa moja kwa moja Ikulu kusimamiwa na Rais, na sheria ile ilitoa kwa mara ya kwanza haki ya watu wa usalama wa taifa kukamata watu, kuwaweka kizuizini, bila kueleza mahali popote wala bila kushtakiwa.

"Sheria hii ilivyopitishwa Rais aliipitisha na akajimilikisha mamlaka ya usalama wa taifa. Sasa mimi kwa niaba ya CHADEMA na vikao na vikao vyangu, tuna declare mtu wa kwanza kuwajibishwa katika masuala hay ani Rais Samia Suluhu Hassan.

"Na sisi tunasema tunaanza moja kwa moja kampeni inayoitwa ‘Samia Must Go’, hiyo ndiyo rai yetu. Sasa basi, kwasababu bado tuna msiba, tumekubaliana kwamba tuna msiba kwasababu kuna viongozi wetu hatujui wako wapi. Kwahiyo sisi kama chama hatujamaliza msiba. Tutaendelea na msiba wetu kitaifa na bender azote za chama zitapeperushwa nusu mlingoti hadi tujue watu wetu wako wapi, wako hai au mauti

"Lingine, kuanzia siku ya Jumatatu, tar 23/9/2024 mkumbuke nilitangaza tar 21 tunategemea tuone hatua za watu kuwajibika zimeanza. Kama hawatachukuliana hatua wenyewe kwa wenyewe, sisi kuanzia tarehe 23 jiji lote la Dar es Salaam, kila kata kila mtaa.. ndugu zangu tumekuwa tunafanya utani mara nyingi, lakini kwa wakati huu hatuna utani.

"Kuanzia jumatatu sisi tutaingia barabarani kudai tunachoona ni uhai wa watu wetu waliopotenzwa unless serikali imechukua hatua za haraka na za makusudi kuwarejesha, watu kujiuzulu na watu wote kuwajibika kwa mujibu wa tamko letu la leo." -
Amesema Mbowe katika mkutano kwenye ofisi za CHADEMA, Mikocheni leo 11/9/2024

Ataondoka Mbowe na Chadema kabla ya SSH.

Mnaalikwa kujiunga kufanya usafi Kwa tarehe tajwa hapo chini 👇👇

View: https://x.com/MzalendoDaily/status/1833893018245451992?t=XyYVwRmVBJCV3OMYzwbTPA&s=19
 
Back
Top Bottom