Pre GE2025 Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Safi sana
 
Watu tumewabembeleza walete katiba mpya wanatuona wajinga . Sheria wametunga wao hawazifuwati halafu bila aibu wanasema tii sheria bila suluti . Yaani mtu anaishi kwasababu ya sheria na katiba halafu haziheshimu. Hapo utasema tuna viongozi au vibaka?
 
Wacha tuendelee kutazama
Usikute mpaka sasa yeye mwenyewe hajui kuwa sio yeye!. Kuna vitu vingine wengine wanaambiwa kabla mhusika hajajua!.
Mfano angalia tarehe ya bandiko hili Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli wakati huo mwenyewe alikuwa hajui.

Hata hapa Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...
Hata hivyo niliisha muanda kisaikolojia kabla Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! huyo mwanamke anaweza kuwa ni Dr. Tulia!.
P
 
Ipo wazi maza anajua anachukiwa na raia, sasa kampeni ikianzishwa itaungwa mkono sana, ninachoona Mbowe anaweza kutulizwa kama sio kulambishwa asali basi atakamatwa.
 
Hiyo jumatatu haifiki.. Mbowe atadakwa kwa uchochezi.
 
Sijui kama mkuu 'Rabbon' ataisoma hii.
Hili ndilo jibu nililokuwa nikitafuta tokea juzi, naye (Rabbon' akawa ananizungusha mbuyu!.

Kwa taarifa hii hapa, ni wazi kabisa kwamba hiyo kazi ya "Kikosi Kazi" imepangwa toka juu kabisa. Huu ni mbango ulio andaliwa kwa maksudi, kama maandalizi ya kuelekea kwenye chaguzi zinazo fuata.
Hapa hakuna cha bahati mbaya, wala nani hajui.
 
Nadhani hiyo ni wrong approach ambayo itasababisha ccm wote waungane kumtetea m/kiti wao. Nice approach ni kumgombanisha sa100 na wanaccm wenzake.
Kwa nini wewe unafikiri CCM wote wanakubali upuuzi huu unaofanywa na vongozi wao?

Okoteza visababu vyako uchwara; lakini Samia hafai kuendelea kuwa kiongozi wa nchi hii.
 
Unawezaje kumtoa Mtu anayelindwa na Jeshi 24/7 ?
Unajidhalilisha sana kwa ujinga kama huu.

Hao viongozi ambao huondolewa madarakani huwa hawana jeshi?

Juzi juzi, yule mama wa Bangladesh alifurumishwa, hakuwa na jeshi?
Akina Omar Bongo huko Gabon, hawakuwa na jeshi?

Nchi inapo kuwa na wajinga wa namna hii ndipo huwa furaha kuu ya viongozi wabovu.

Sikiliza, wewe si lazima ushiriki. Kaa pembeni, subiri wenye uchungu na nchi hii wakufanyie kazi. Kwenye nchi yoyote ile, watu wa aina yako hawakosekani.
 
Huu ujinga ulioandika ndio wanaoutumia kuteka na kuua watu wakiamini watanzania watatulia tu. Usisubiri yakukute ndio ujie umuhimu wa kuchukua hatua kama hizi.
Sasa ndugu yangu, kuna vitu vinahitaji suluhisho la busara! Huwezi kutumia bad methods ukitegemea kupata matokeo chanya. πŸ™πŸ™πŸ™βœ
 
"Samia must go" ,na sio CCM must go!!.

Mbowe mjanja sana anakula huku na kule.
Mbowe mjinga tu ka copy and paste ya Kenya ya Ruto must go

Hana ubunifu wowote
Anadhani environment ya Kenya na ya Tanzania ziko sawa na anadhani watu w Kenya na Tanzania wanafanana

Tanzania haambulii kiti vijana wa Kenya na Tanzania tofauti sana
 
Ataondoka Mbowe na Chadema kabla ya SSH.

Mnaalikwa kujiunga kufanya usafi Kwa tarehe tajwa hapo chini πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://x.com/MzalendoDaily/status/1833893018245451992?t=XyYVwRmVBJCV3OMYzwbTPA&s=19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…