Mbowe: Mtu yeyote anayepuuza siasa atatawaliwa na wajinga

Mbowe: Mtu yeyote anayepuuza siasa atatawaliwa na wajinga

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kauli hii Muhimu imetolewa na Mwamba wa siasa za Tanzania Mh. Freeman Mbowe huko Ikungi Mkoani Singida.

Akihutubia Maelfu ya wananchi wa Ikungi, katika Mkutano unaodhaniwa kuvunja rekodi ya mahudhurio ya watu kwa mikutano ya hadhara iliyowahi kufanyika Mkoa wa Singida tangu mkoa huo uanzishwe, Mbowe amesema kwamba, wewe ukijifanya mjanja kwa kudhan kwamba siasa haikuhusu, basi jiandae kwa Tozo, mfumuko wa bei, ugumu wa maisha na taabu zote za dunia.

Mbowe amewakumbusha Watanzania kwamba SIASA NI MAISHA, hakuna yeyote aliye hai anayeweza kujitenga nayo.
 
Ni mwanasiasa uchwara awezaye kutoa kauli ya kwamba wewe ukijifanya mjanja kwa kudhan kwamba siasa haikuhusu, basi jiandae kwa Tozo, mfumuko wa bei, ugumu wa maisha na taabu zote za dunia na wewe unayeitetea ni mtu wa kujipendekeza.

Ukiweza kujibu maswali yafuatayo kwa moyo wa dhati na Uzalendo (kwa maana kuwa msingi wa mwanasiasa yeyote ni uzalendo - kujitoa kwa hali na mali kuendeleza jami - TAIFA), ili hoja zako ziwe na matinki

1) Je, huyo Mbowe akiingia madarakani ataendesha nchi kwa fedha gani?
2) Je, biashara ambazo amekuwa akifanya mtaji amepata wapi?
3) Je, faida katika biashara zake amewapunguzia wangapi umaskini?
 
Ni mwanasiasa uchwara awezaye kutoa kauli ya kwaMmbs wewe ukijifanya mjanja kwa kudhan kwamba siasa haikuhusu , basi jiandae kwa Tozo , mfumuko wa bei , ugumu wa maisha na taabu zote za dunia na wewe unayeitetea ni mtu wa kujipendekeza...
Weee jamaa siku nyingine ficha ujinga wako bhana...

(1) Ataendesha nchi kwa rasimali hizo hizo lkn kwa manufaa ya nchi tofauti na ccm wanaoiba na kuficha ughaibuni

(2) Mhe mbowe hela kaikuta na anaiendeleza . Hivyo hata nchi ataiendeleza kwa ufanisi kama afanyavyo kwenye biashara zake

(3) ameajiri vijana wengi tu hata ww ukitaka sema uajiriwe .. , mm sijaajiriwa lkn niko zangu ifwenkenya nachimba zangu madini ya dhahabu na nalima mpunga bonde la kamsamba
 
Weee jamaa siku nyingine ficha ujinga wako bhana...

(1) Ataendesha nchi kwa rasimali hizo hizo lkn kwa manufaa ya nchi tofauti na ccm wanaoiba na kuficha ughaibuni...
Ningekujibu ila umesukumwa na hisia za kisiasa hadi kunitukana.

Lakini, moja ambalo itapendeza kurejea, ni kuhusu kujihusisha kwake katika siasa amefanikisha yapi, katika majimbo ambayo CHADEMA ilitawala, kwa kutumia rasmali za nchi? Usisahau kwamba hata ofisi za chama hazijajengwa, japo alikuwa akilipwa mabilioni ya ruzuku na michango ya lazima ya Wabunge, mbali ya wanachama wa kawaida km ada!!!
 
Back
Top Bottom