Mbowe na genge lako, mnamtisha Amiri Jeshi Mkuu akitumia madaraka yake muanze tena kulalamika?

Mbowe na genge lako, mnamtisha Amiri Jeshi Mkuu akitumia madaraka yake muanze tena kulalamika?

Mpaka wewe umeibuka leo!!!!
Nimeamini UVCCM huwa mnaambiwa nini cha kufanya kwenye mitandao.
Poleni kwa kushikiwa akili.
Poleni kwa kuwa misukule.
Poleni kwa kutobarikiwa akili ya kujipatia kipato kwa jasho.
Poleni.
Sihitaji katiba mpya sijui nini, ninachohitaji ni maendeleo. Huyo Mbowe aache bla bla zake.
 
Hamna haja kupigania Katiba wakati rais kaishasema wazi kuwa watanzania wampe muda watapata katiba.

Ametaja muda specific? Ni vyema angetaja muda na sio kusema apewe muda ainue uchumi, wakati hakuna kipimo maalumu cha uchumi ausemao. Kwa mujibu wa serikali aliyokuwepo, tuko uchumi wa kati, je anataka mpaka uchumi uweje?
 
Sihitaji katiba mpya sijui nini, ninachohitaji ni maendeleo. Huyo Mbowe aache bla bla zake.

Kama ni maendeleo unahitaji, kwanini Nyerere alikuwa anamsupport Mandela na weusi wa Afrika kusini dhidi ya wazungu ambao walikuwa wanafanya maendeleo?
 
Wanaukumbi,

Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu asiyetambua umuhimu wa Katiba Mpya; tunapishana sehemu ndogo sana ‘timing’ na vipaumbele vya kitaifa kwa sasa viwe ni 1. Katiba Mpya au kupambana na 2. Janga la Corona na 3. Kuinua Uchumi na hali za wananchi masikini?

Sisi Watanzania tumechagua muhimu 2 na 3.

Mbowe na wafuasi wako mnachekesha sana hivi mnataka rais wetu afuate mnachotaka nyie kwa maslahi yenu?

Rais akitumia madaraka yake kama katiba unavyomtaka mtaanza tena kulia kuwa Tanzania hamna demokrasia.

Nakushauri Mbowe, zile pesa mlizorudishiwa na mahakama jengeni ofisi kwanza ondokeni Ufipa mlilpopanga vyumba viwili hamna Mtanzania anaweza kuwaamini wewe na kundi lako.

Kichwa cha bandiko kimekaa kichonganishi. Ni ile mitoto inayotishia kushtaki kwa mama kama vile inaonya, huku ikihakikisha mama anaisikia ili achukue hatua kali.

Hiiiiii bagosha!

Tuwatambue wazandiki hawa:


Mwanzo wa ngoma ni kuwafahamu wote kwa majina yao.
 
wananchi tunataka;

1. Maji safi na salama

2. elimu bora

3. barabara zenye kupitika

4. Umeme wa uhakika

5. pembejeo za kilimo na vitendea kazi.

Mbowe na chama chake ndio wanataka Mpya katiba.
wasubiri mpaka 2040.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hakukuwa na katiba mpya, je kipi kilifanya hayo yasipatikane?
 
Siwapangii lakini policy ya JF inapinga masuala ya ubaguzi wa kidini/ukabila na hatespeech. Ssa mtu anakuja na mada eti Mbowe anampinga Samia kisa ni Muislam!! Seriously? Kwani JPM alikua Muislam pia?

Udini haupaswi kushabikiwa
Unaweza kuonyesha sehemu ambayo mleta mada ameandika kua;

"Mbowe anampiga Samia kisa Muislamu?"

Au unaendeshwa tu na hisia zako binafsi?

Mimi naona wewe ndio unaleta udini kwenye hii thread.
 
Kuna kiila dalili kuwa hawa wanasiasa wabovu, walevi na waongo wameanza kumpanda kichwani mama.

Hivyo nakuomba mama yetu kipenzi chetu usiwajibu chochote wewe wakalie kimya tu ila warudishie mbabe wao Sabaya.

Sabaya aliwaweza kabisa, walikuwa hawana uwezo hata wa kukohoa mbele yake kuanzia chairman wa kudumu hadi mfagia ofisi wote waliufyata.

Walikuwa hawana hata muda wa kudai mikutano wala sijui katiba, wao walibali siku nzima kulia tu. Hawa wanasiasa walevi usije ukawaendekeza hata kidogo hawanaga shukrani.

Ukitaka kuona hizi kelele zao zinaisha wakabidhi Ole sabaya, tena mpe wizara ya mambo ya ndani. Hutaona tena wala kusikia kelele yoyote, wanamuogopa sana sabaya. Walilia kila aina ya kilio.

Mwenyekiti wa kudumu alikimbia kwao usiku usiku, hivyo wala usiwajibu hawa dawa yao ni huyo. Ila sabaya aliwakomesha aisee, hizi kelele mlizoana kuzipiga zisingekuwepo.

Uchumi kwanza.
Katiba hata vikoba wanayo
#kazi iendelee#
 
Kwamba nchi inaendeshwa kwa Rehema na Shukrani kwa Mwenyekiti wa CCM..

Long way to Freedom
 
Kuna kiila dalili kuwa hawa wanasiasa wabovu, walevi na waongo wameanza kumpanda kichwani mama. Hivyo nakuomba mama yetu kipenzi chetu usiwajibu chochote wewe wakalie kimya tu ila warudishie mbabe wao Sabaya...
Bhodogo...
 
Hakukuwa na katiba mpya, je kipi kilifanya hayo yasipatikane?
mabadiliko yatafanyika mwaka 2040 sio leo wala kesho, tuwe wavumilivu, tuchape kazi tuache kuwaza vyeo.

wanasiasa wanao dai mpya katiba wao wanacho waza ni madaraka na vyeo tu sio shida za wananchi.

sijawahi kumuona Mbowe anatatua shida za wananchi au anahamasisha maendeleo ya wananchi kama alivyo kuwa marehemu Ndesamburo, sana sana anahamasisha maandamano tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui huyu jamaa yupoje

Yeye ni kiki na kiki na yeye

Mama amewajibu kistaarabu kwamba mumpe muda tena amewaomba lakini kiburi kinakupanda

Sasa kama sio kichaa kwanini hamkutaka katiba wakati wa Magufuli?mbona hamkutoa pua zenu nje even kudai kuandamana


Ni kwasababu ni Samia si ndio?Huyu mama kaonyesha njia ya na amerudisha uhuru na haki tulioukosa kwa miaka 6

Muacheni ajenge uchumi kwanza nyie mnamvuruga kwa kutumiwa na watu wa nje

Kwanini mnapanda mama kichwani?kwanini hamkufanya hivyo wakati wa magufuli...mama kaamua kuwa mwema kwetu sisi na tunataka awe hivi hivi halafu kina mbowe mnataka mama abadilike

Dola haichezewi na hata mbowe unalijua hilo, katiba tumpe mama muda kwanza, mwenyewe katiba ya chama imekushinda umetawala chama kwa miaka 20 halafu hatusemi, mpe mama nafasi ashasema tumpe muda

Tunatakiwa tushukuru tuna rais anayesikiliza maoni na anayekosolewa akakubali lakini bado hamulioni hilo mnatakaje?

,Kwanini mnakubali kutumika kwa manufaa ya wazungu?

Mbowe tuli na utulizane maana vuguvugu umelitaka watanzania sisi tunataka maendeo kwanza katiba baadae


Hakuna mjinga atakayeandamana kwa sababu ya mbowe na genge lake mbowe ni mbinafsi na anatumika na wazungu kulivuruga taifa nani amsikilize mtu km yule?

Niandamane kwa sababu ya kina mbowe khaaaaa[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]labda km nitakua mgonjwa
 
Uzuri wa watanzania ni wazuri kusapoti katika kusema.

Lakini sio kusapoti ati kuandamana.

Siasa za tanzania sasa hivi na watanzania tulipofikisha na siasa ni kwamba ishu kama hii ya katiba mpya watakaokuwa na muamko wa kuandamana ni vyama pinzani.

Lakini kuna watanzania wengi ambao sio wanasiasa hawatoona umuhimu wa kuandamana.
 
Back
Top Bottom