Mwamba tumeshamzoea na Speeches zake nzuri nzuri za hamasa. Ni kweli kipaji cha kuzungumza anacho, anavutia kusikiliza. Lakini utamu wa speeches zake hautupi katiba mpya, tume huru ya uchaguzi wala kuzuia bandari zetu kwenda kwa mwarabu. Tunataka chama kiunge mkono next level ya struggle ambayo ni mass action,
Miaka 20 ya kukaa kwenye uwenyekiti wewe unaongea tu, unaongea tu, unaongea tu. Sasa leo wananchi wanataka kuraise stake juu, beef up the ante, kubonyeza kitufe cha kuongeza joto kwa CCM, na katika kuwezesha hilo tunahitaji kushirikiana na Taasisi ya Chadema ambayo na sisi kuna jasho letu humo wewe unakuja na blahblah za oooh, hamkunishirikisha, ooooh sisi siyo pressure group, kama siyo pressure nyie ni nani, ni kundi la wacheza singeli na vigodoro au kitu gani?
Hii naivety ya Mwenyekiti ya namna ya kudeal na CCM inaturudisha nyuma sana.