Mbowe na siasa zake za "I am the only negro incharge in here"

Wakikuelewa usiache kutuletea mrejesho. Haijulikani wanataka au hawataki nini na wala kuwa wanamsemea nani.
CDM ilizidi kulala usingizini,

Naziona HOJA na siasa zenye nguvu sana za Ukombozi zitakazoanzishwa na viongozi wa Dini,

Ni hatari, lakini ndo jambo litatokea ikiwa CCMMM na CDM zitaendelea kuweka mbele kujikinai na kiburi ambacho wanapewa na wananchi wengi wasio na vyama.

Wengine tumejaaliwa macho yaonayo mbele na mbali sana.

Tusubiri.
 
Hebu fikirieni hili suala:
Umma wa Tanzania umeanza kuamka, unakataa udalali wa rasilimali zao, unaanza polepole kukataa chapa waliyopigwa kwa muda mrefu kimkakati ya uoga, unaanza kuchukua hatua ya kupeleka Struggle katika hatua ya pili ya matendo badala ya maneno. Cha kusikitisha anatokea kiongozi mmoja wa Taasisi muhimu ya wananchi, ambaye kwa nafasi yake, na mizizi ya taasisi yake angeweza kusaidia pakubwa kuwatoa wananchi kutoka katika kongwa hili la kutochukua hatua yoyote ya kuiadabisha serikali yao kutokana na madudu makubwa inayofanya yeye anarudi nyuma, na matokeo yake kuisaidia CCM kuzima cheche ambazo zingesaidia kutengeneza moto mkubwa wa mabadiliko huko mbele. Ni ajabu sana!

1. Mbowe na siasa zake za ki "Uncle Tom"
Kipindi cha utumwa huko Marekani na Jim Crow, walikuwepo wamarekani weusi ambao kwa kuwa wao walikuwa na vijinafasinafasi katika mfumo wa Marekani, walikuwa wakipenda kujitapa kwa kauli za "I am the only negro working as an engineer here", "I am the first black clerk in here". Leo hii Huwezi kushangaa kumsikia Mbowe akijitapa na kauli yake maarufu ya siasa za nchi hii ni ya Farasi wawili, CCM na Chadema. Na hii Mentality ndiyo inayomsukuma kutaka alambwe miguu pale wananchi wanapotaka kusogeza struggle kwenda next level, Ili kuitia kibano serikali ya CCM katika suala la bandari na katiba mpya. Ndiyo maana Juzi huko Zanzibar, huku akisimama kwa kujitapa mbele ya wazee wa chama anahoji eti Chadema haikushirikishwa katika maandalizi ya mikutano na maandamano ya kuibana serikali ya CCM katika suala la katiba mpya na Bandari. Yaani anataka apigiwe magoti na wananchi kwenye struggle za kuitia kibano serikali, yeye nani, na kwa nini?!.

2. Mbowe amesaliti struggle za Watanzania kupeleka struggle next level
Sijui kama Mbowe na chawa wake ndani ya Chadema wanatambua athari za walichokifanya dhidi ya struggle za Watanzania katika kujikomboa kutoka katika minyororo ya Siasa chafu na uongozi mbovu wa CCM. Badala ya kuweka ego ya Kiuenyekiti, na ego ya uchama mbele, Mbowe alipaswa aangalie picha pana ya movement ya wananchi ya kutaka kuitia kibano Serikali ya CCM zaidi katika suala la bandari. Infact struggle hii inacompliment kabisa jitihada za chama cha Chadema za kudai katiba mpya. Badala ya Mbowe kuwapiga Rungu Sauti ya Watanzania, kama kweli angekuwa anahitaji mabadiliko ya kweli nchini, alipaswa aweke ego yake pembeni na kuwasaidia kadri inavyowezekana. Hii ingesolidify movement ya mabadiliko kutoka pande zote za kijamii na kisiasa za kuleta mabadiliko nchini. Lakini cha ajabu at the critical hour, Mwenyekiti kama kawaida yake ANABADILI GIA angani.

3. Jeuri ya Nyomi mikutanoni na kudhani Chadema haihitaji Sauti za mitandaoni
Inavyoelekea, wingi wa watu katika mikutano ya Chadema umeanza kuwapa kiburi viongozi wa Chadema na kudhani kuwa nyomi hilo linamaanisha kushinda chaguzi na labda eti hiyo ndiyo force pekee inayoweza kuipeleka Chadema mbele. Nataka nimwambie Mwenyekiti Mbowe na Chawa wake ndani ya Chama kuwa kudhani hivyo ni very naive, Maana hata kama hilo nyomi lote litaichagua Chadema, kama hakuna katiba mpya, tume huru ya uchaguzi ni kazi bure. Ndiyo maana ni ujinga mtupu kubeza cheche za struggle ambazo zitazaa moto wa mabadiliko ya kisiasa na kijamii nchini yatakayoisaidia hata Chadema yenyewe. Na mtu yeyote anayedharau kundi la wananchi ambalo liko "Enlightened" basi huyo hajielewi.

Na labda tu nimwambie Mbowe, kuwa pengine Nyomi la mikutano linamtia kiburi na kuamini kuwa Hakuna haja ya kuwaengage Watanzania wa mitandaoni. Asubiri aone kama CCM nao watapita katika kata hizohizo anazopita leo watu walewale waliojitokeza kumsikiliza kama hawatakwenda kuwasikiliza CCM pia. Ni Ujinga kudharau movement ya kundi dogo wenye uelewa ktk society

4. Akili za kuwaza ubunge, wingi wa ruzuku na kuendelea kuwa Mwenyekiti
Siyo siri, viongozi wengi ndani ya Chadema ya leo wanawaza ubunge tu mwaka 2025. Ni wachache sana miongoni mwao wanaowaza beyond ubunge. Na hii sauti ya waota ubunge ndani ya chama ni kubwa zaidi kuliko wale ambao Genuinely kabisa wanawaza mabadiliko ya kweli ya kimfumo nchini. Ukisikiliza kauli za viongozi wengi wa Chadema wako more worried na uchaguzi mkuu ujao, na ndiyo maana sasa wanazungumza habari za mabadiliko ya katiba kuelekea uchaguzi. Hoja zilezile ambazo miaka mitatu iliyopita walikuwa wakiwatukana ACT kwazo, ndiyo hizohizo leo wanazileta kwetu kama eti ni maono ya hekima ya chama. Kama hekima zinapatika ndani ya miaka mitatu, basi maana yake huko nyuma hakuwa na hekima anyway.

5. Mbowe kama Gatekeeper
It seems Mbowe, hayuko tayari kwa massive action nchini. Yaani anadhani kuwa CCM itatuleta mabadiliko kwa kuombwa, kwa kujitungia sheria za kujidhibiti yenyewe, kwa kuombwa kuleta katiba ya kujimaliza yenyewe. Na CCM kwa kutambua udhaifu wa Mwenyekiti katika mambo makuu matatu, Mosi anautaka uenyekiti tena, Pili ni muoga wa kupush hard na Tatu ana maslahi nchini ambayo wanaweza kumblackmail nayo basi wako Comfortable kuwa Mwamba ataruka na chopa, ataongea rousy speeches lakini itakapokuja muda ambao Watu wanataka kuraise up, basi Mwenyekiti atatumia machinery ya chama chake kujiweka pembeni na kuwaacha wanaotaka kuraise wakiwa marginalized. Ni jukumu la Wanachadema kukifanyia review chama chao waone kuwa The same Old Mwenyekiti ana kipya au sasa ni time ya Change ili kupush mabadiliko ya kweli nchini.

6. Mwisho
Hapa nataka nitoe tahadhari kwa viongozi wa Chadema ambao wameanza kuwa arrogant kwa kudhani Chadema is too big, na hawahitaji kuchangamana na watanzania wengine hasa wa mitandaoni.

Iko hivi, ni sisi wananchi wa Mitandaoni tuliopiga presha mpaka Mbowe akaachiwa. Ni sisi wananchi wengine wengi tu tusio na vyama lakini tuliokuwa tukiichangia Chadema katika operesheni zake. Ni sisi ambao tumeipa moral support, kwa kauli na matendo Na infact ni sisi ndiyo tunaolipa kodi ambayo leo hii Chadema wanapata ruzuku. Hii arrogance ya kijinga ambayo kwa bahati mbaya naona mnayo kuwa Walioko mitandaoni hawana dili, itakuja kuwatokea puani pale sentiment zitakapoanza kuwa negative kwenu na chama chenu. Kama mnabisha kaiulizeni ACT kwa nini haitoboi Tanganyika. Kawaulizeni negative content inawaathiri vipi!. Sasa msitufikishe huko.

Kama kweli Chadema ni chama cha wananchi, basi hiyo Taasisi ifanye kazi ya wananchi. Tungeshukuru sana kama Ingeshirikiana na Sauti ya Watanzani kuibana CCM zaidi, Kuitia kibado zaidi CCM kwenye suala la bandari na katiba. Kinyume cha hapo ni kuipa life support CCM na huo ni usaliti.

Nawasilisha!
Umesema ukweli ila hawa Nyumbu ni wagumu sana kuelewa wala kujitambua!
 
Usichokijua ni kuwa watu hao wanaomsaport Mdude, Mwabukusi na Slaa ndo wanaisapot CDM.
Inaweza kuonekana hivyo machoni.

Lakini ndani huwezi kujua mpaka tu uwe umejaliwa karama ya kuona Kwa macho ya ndani..

Sisi tunaona kwa macho ya rohoni kuwa hakuna kitu hapo..!!!!
Suluhu ni kuungana, Si kuanzisha chama kipya.
Waende wakajiunge CHADEMA.

Na kumbuka, ili kufanya harakati za kisiasa Tanzania, basi ni sharti u - comply na sheria za nchi zinazoongoza shughuli za kisiasa..

Au la, fanya mambo yako kama mwanaharakati huru. Na hapo walipo, ndipo mahali pao...

Ni makosa kuiingiza CHADEMA kwenye harakati zao kwa position yao na inapowakatalia kushiriki pamoja nao waelewe na si kuwanalaumu wenzao..
Chama kipya kitapunguza nguvu ya UMOJA wa watz na nguvu ya CDM kama main opposition party.
Sio kweli...
Mpaka sasa kuna legally registered political parties zaidi ya 20. Kipi kimeipunguzia kasi CHADEMA hata kukitoa kwenye position yake?
Narudia HOJA za Mbowe hazikuwa na mashiko.
Kwanza kumbuka hizo sio hoja za Freeman Mbowe. Hizo ni hoja na ni msimamo wa CHADEMA kama taasisi uliotolewa na Mwenyekiti wao..

Na hoja hizo zina mashiko na impact kuliko udhaniavyo. Na huyu ndiye kiongozi hasa...

Na kila mtu mwenye akili anaweza kuthibitisha sasa kuwa, kumbe CHADEMA kina akili na kina viongozi wanaoona hatari iliyo mbele yao na kuikwepa kirahisi. Ndiyo maana kipo na kitaongoza nchi hii kama chama tawala muda si kitambo...

Siasa za Tanzania zinahitaji umakini na sio mihemko na pupa. Dr Wlbroad Slaa na wenzake wako emotional sana. Mikakati yao ni very fragile and predictable..

Nakuhakikishia kitu komoja kuwa, hawatafanikiwa na wanaweza kuzimwa kirahisi sana unless wamerudi kwenye drawing board na kwa hekima na heshima wawavute wenzao na kupanga mikakati Kwa utaratibu wa pamoja step by step..!
 
Usichokijua ni kuwa watu hao wanaomsaport Mdude, Mwabukusi na Slaa ndo wanaisapot CDM.

Suluhu ni kuungana, Si kuanzisha chama kipya.

Chama kipya kitapunguza nguvu ya UMOJA wa watz na nguvu ya CDM kama main opposition party.

Kila kundi likianziaha chama chake Bado adui hatowezekanika ndo sababu ya Slaa kuomba support ya CDM.

Narudia HOJA za Mbowe hazikuwa na mashiko.

..ila hoja za Mwabukusi kwamba vyama vya upinzani ni magenge maslahi ya ubunge na ruzuku ina mashiko!?
 
Huu sio uchochezi, huoni mikutano ya Lissu hapewi umuhimu?
Mbowe anatmia chopa Lissu magari.
Mbowe mkutano unapambwa lkn Lissu majukwaa mabovu.

Japo Lissu anajaza watu kwa mvuto wake wa kujenga hoja.
Funguka
Mbowe anajaza watu Kwa chopa
 
Naimani kubwa na viongozi wa chadema.

Wapumbavu/vigeugeu kama slaa wafie mbele ka magufuri.

Wanataka kutumia chadema kama platform ili waonekane na wao kama wapigania haki za wananchi.

Waache usenge
 
Nililazimika kukwambia tuwe tunapiga hatua. Andiko lako ni kama umefika duniani sasa tokea sayari nyingine.

Kwa andiko lako hujui kuna mtafaruku, kuwa hakuna hata usuluhishi unaohitajika.

"Kwamba unadhani kumbe wanaoandika hawa ni wendawazimu."

Sawa endeleeni kukaza shingo ila hoja haipigwi rungu.

Wapi umeona Mwabukusi na wanaharakati wanataka kuongea na chadema ambayo hata tumekubaliana si mtu, ya mtu na hayupo mwenye hati miliki peke yake humo?

Haya si ni maajabu yenyewe ya Mussa?

..kwani mikutano ya Chadema ya operation 255 katiba mpya ina tatizo gani?

..badala ya kuwapa moyo kwanini mnawakatisha tamaa waandaaji wa mikutano hiyo?

..adui yetu ni Ccm sio Chadema.
 
Hebu fikirieni hili suala:
Umma wa Tanzania umeanza kuamka, unakataa udalali wa rasilimali zao, unaanza polepole kukataa chapa waliyopigwa kwa muda mrefu kimkakati ya uoga, unaanza kuchukua hatua ya kupeleka Struggle katika hatua ya pili ya matendo badala ya maneno. Cha kusikitisha anatokea kiongozi mmoja wa Taasisi muhimu ya wananchi, ambaye kwa nafasi yake, na mizizi ya taasisi yake angeweza kusaidia pakubwa kuwatoa wananchi kutoka katika kongwa hili la kutochukua hatua yoyote ya kuiadabisha serikali yao kutokana na madudu makubwa inayofanya yeye anarudi nyuma, na matokeo yake kuisaidia CCM kuzima cheche ambazo zingesaidia kutengeneza moto mkubwa wa mabadiliko huko mbele. Ni ajabu sana!

1. Mbowe na siasa zake za ki "Uncle Tom"
Kipindi cha utumwa huko Marekani na Jim Crow, walikuwepo wamarekani weusi ambao kwa kuwa wao walikuwa na vijinafasinafasi katika mfumo wa Marekani, walikuwa wakipenda kujitapa kwa kauli za "I am the only negro working as an engineer here", "I am the first black clerk in here". Leo hii Huwezi kushangaa kumsikia Mbowe akijitapa na kauli yake maarufu ya siasa za nchi hii ni ya Farasi wawili, CCM na Chadema. Na hii Mentality ndiyo inayomsukuma kutaka alambwe miguu pale wananchi wanapotaka kusogeza struggle kwenda next level, Ili kuitia kibano serikali ya CCM katika suala la bandari na katiba mpya. Ndiyo maana Juzi huko Zanzibar, huku akisimama kwa kujitapa mbele ya wazee wa chama anahoji eti Chadema haikushirikishwa katika maandalizi ya mikutano na maandamano ya kuibana serikali ya CCM katika suala la katiba mpya na Bandari. Yaani anataka apigiwe magoti na wananchi kwenye struggle za kuitia kibano serikali, yeye nani, na kwa nini?!.

2. Mbowe amesaliti struggle za Watanzania kupeleka struggle next level
Sijui kama Mbowe na chawa wake ndani ya Chadema wanatambua athari za walichokifanya dhidi ya struggle za Watanzania katika kujikomboa kutoka katika minyororo ya Siasa chafu na uongozi mbovu wa CCM. Badala ya kuweka ego ya Kiuenyekiti, na ego ya uchama mbele, Mbowe alipaswa aangalie picha pana ya movement ya wananchi ya kutaka kuitia kibano Serikali ya CCM zaidi katika suala la bandari. Infact struggle hii inacompliment kabisa jitihada za chama cha Chadema za kudai katiba mpya. Badala ya Mbowe kuwapiga Rungu Sauti ya Watanzania, kama kweli angekuwa anahitaji mabadiliko ya kweli nchini, alipaswa aweke ego yake pembeni na kuwasaidia kadri inavyowezekana. Hii ingesolidify movement ya mabadiliko kutoka pande zote za kijamii na kisiasa za kuleta mabadiliko nchini. Lakini cha ajabu at the critical hour, Mwenyekiti kama kawaida yake ANABADILI GIA angani.

3. Jeuri ya Nyomi mikutanoni na kudhani Chadema haihitaji Sauti za mitandaoni
Inavyoelekea, wingi wa watu katika mikutano ya Chadema umeanza kuwapa kiburi viongozi wa Chadema na kudhani kuwa nyomi hilo linamaanisha kushinda chaguzi na labda eti hiyo ndiyo force pekee inayoweza kuipeleka Chadema mbele. Nataka nimwambie Mwenyekiti Mbowe na Chawa wake ndani ya Chama kuwa kudhani hivyo ni very naive, Maana hata kama hilo nyomi lote litaichagua Chadema, kama hakuna katiba mpya, tume huru ya uchaguzi ni kazi bure. Ndiyo maana ni ujinga mtupu kubeza cheche za struggle ambazo zitazaa moto wa mabadiliko ya kisiasa na kijamii nchini yatakayoisaidia hata Chadema yenyewe. Na mtu yeyote anayedharau kundi la wananchi ambalo liko "Enlightened" basi huyo hajielewi.

Na labda tu nimwambie Mbowe, kuwa pengine Nyomi la mikutano linamtia kiburi na kuamini kuwa Hakuna haja ya kuwaengage Watanzania wa mitandaoni. Asubiri aone kama CCM nao watapita katika kata hizohizo anazopita leo watu walewale waliojitokeza kumsikiliza kama hawatakwenda kuwasikiliza CCM pia. Ni Ujinga kudharau movement ya kundi dogo wenye uelewa ktk society

4. Akili za kuwaza ubunge, wingi wa ruzuku na kuendelea kuwa Mwenyekiti
Siyo siri, viongozi wengi ndani ya Chadema ya leo wanawaza ubunge tu mwaka 2025. Ni wachache sana miongoni mwao wanaowaza beyond ubunge. Na hii sauti ya waota ubunge ndani ya chama ni kubwa zaidi kuliko wale ambao Genuinely kabisa wanawaza mabadiliko ya kweli ya kimfumo nchini. Ukisikiliza kauli za viongozi wengi wa Chadema wako more worried na uchaguzi mkuu ujao, na ndiyo maana sasa wanazungumza habari za mabadiliko ya katiba kuelekea uchaguzi. Hoja zilezile ambazo miaka mitatu iliyopita walikuwa wakiwatukana ACT kwazo, ndiyo hizohizo leo wanazileta kwetu kama eti ni maono ya hekima ya chama. Kama hekima zinapatika ndani ya miaka mitatu, basi maana yake huko nyuma hakuwa na hekima anyway.

5. Mbowe kama Gatekeeper
It seems Mbowe, hayuko tayari kwa massive action nchini. Yaani anadhani kuwa CCM itatuleta mabadiliko kwa kuombwa, kwa kujitungia sheria za kujidhibiti yenyewe, kwa kuombwa kuleta katiba ya kujimaliza yenyewe. Na CCM kwa kutambua udhaifu wa Mwenyekiti katika mambo makuu matatu, Mosi anautaka uenyekiti tena, Pili ni muoga wa kupush hard na Tatu ana maslahi nchini ambayo wanaweza kumblackmail nayo basi wako Comfortable kuwa Mwamba ataruka na chopa, ataongea rousy speeches lakini itakapokuja muda ambao Watu wanataka kuraise up, basi Mwenyekiti atatumia machinery ya chama chake kujiweka pembeni na kuwaacha wanaotaka kuraise wakiwa marginalized. Ni jukumu la Wanachadema kukifanyia review chama chao waone kuwa The same Old Mwenyekiti ana kipya au sasa ni time ya Change ili kupush mabadiliko ya kweli nchini.

6. Mwisho
Hapa nataka nitoe tahadhari kwa viongozi wa Chadema ambao wameanza kuwa arrogant kwa kudhani Chadema is too big, na hawahitaji kuchangamana na watanzania wengine hasa wa mitandaoni.

Iko hivi, ni sisi wananchi wa Mitandaoni tuliopiga presha mpaka Mbowe akaachiwa. Ni sisi wananchi wengine wengi tu tusio na vyama lakini tuliokuwa tukiichangia Chadema katika operesheni zake. Ni sisi ambao tumeipa moral support, kwa kauli na matendo Na infact ni sisi ndiyo tunaolipa kodi ambayo leo hii Chadema wanapata ruzuku. Hii arrogance ya kijinga ambayo kwa bahati mbaya naona mnayo kuwa Walioko mitandaoni hawana dili, itakuja kuwatokea puani pale sentiment zitakapoanza kuwa negative kwenu na chama chenu. Kama mnabisha kaiulizeni ACT kwa nini haitoboi Tanganyika. Kawaulizeni negative content inawaathiri vipi!. Sasa msitufikishe huko.

Kama kweli Chadema ni chama cha wananchi, basi hiyo Taasisi ifanye kazi ya wananchi. Tungeshukuru sana kama Ingeshirikiana na Sauti ya Watanzani kuibana CCM zaidi, Kuitia kibado zaidi CCM kwenye suala la bandari na katiba. Kinyume cha hapo ni kuipa life support CCM na huo ni usaliti.

Nawasilisha!
Achana na Chadema hangaika na ccm yako.
 
..kwani mikutano ya Chadema ya operation 255 katiba mpya ina tatizo gani?

..badala ya kuwapa moyo kwanini mnawakatisha tamaa waandaaji wa mikutano hiyo?

..adui yetu ni Ccm sio Chadema.

Kwani mikutano ya kina Mwabukusi ilikuwa na tatizo gani ku merit response hii?

View: https://m.youtube.com/watch?v=63aDMuscAFU

Wewe unaona ni sawa bin sawia?

Bado wapi umeona tatizo na +255 na awaye yote au hata hili la kukatisha tamaa unalosema?
 
Hizo confrontation politics ambazo wanataka Mbowe aende nazo dhidi ya misisiyemu watakaoumia ni cdm wala siyo misisiyemu.Kibaya zaidi watz majority hawaziwezi siasa za hivyo kwa sababu ya uoga wa police na vizimba vya mahakama
 
Ngoja chawa wake waje wakupopowe na mawe. Miongoni mwa viumbe vya ajabu duniani basi ni Wafuasi wa Mbowe au Chadema kwa ujumla. Wao wanaamini wako sahihi muda wote na wengine hawako sahihi. Wao wanaamini kila anayewakosoa ni CCM au ACT.Hii nchi kungekua na upinzani wa maana swala la Bandari na saizi umeme yalitosha kuitoa ccm madarakani au hata kuipa adabu tu CCM.Mbowe na genge lake wanawaza ubunge tu na sio kuleta mabadiliko yoyote Tanzania. Siasa zao ni za kujipendekeza kwa watawala angalau 2025 wawalegezee kwenye Ubunge. Wanafanya SIASA za kuogopa kuikwaza CCM wasije wapiga pini huko mbele.Hiki sio chama cha siasa bali genge la wahuni.
Suala ni kuanzisha chama chako tu . Ofisi za msajili ziko hapo kwa Ajili ya kazi hiyo wala idadi haina limit no room for lamentations
 
Mbowe ningemdharau sana kama angeshiriki haya maandamano ya akina Slaa na Mdude, mtu yoyote mwenye akili aliyeona ile press conference yao ya kuipa serikali siku 30 angesema hawa watu ni vichaa
Kwanza Chadema kama taasisi haiwezi kuburuzwa na kuingizwa mzobemzobe kwenye movement ambayo wamehusishwa kwetu final stage tu . Waache akina slaa waendelee
 
..nyinyi ambao sio chawa wa Mbowe mmefanya nini? Mbona inaonekana hamna mbadala wa mtu, na hata ideas?
Wanakuambia kwamba Mbowe wanaanza naye vizur kisha anawabutua dakika za mwisho
 
Mtego wa Kitengo tumeuvuka salama Mungu mkubwa.

✌️✌️✌️
 
Kwani mikutano ya kina Mwabukusi ilikuwa na tatizo gani ku merit response hii?

View: https://m.youtube.com/watch?v=63aDMuscAFU

Wewe unaona ni sawa bin sawia?

Bado wapi umeona tatizo na +255 na awaye yote au hata hili la kukatisha tamaa unalosema?

..response hiyo ni baada ya Adv.Mwabukusi kudai vyama vya upinzani ni magenge ya kusaka ubunge na ruzuku na havitetei maslahi na agenda za wananchi. Na Mbowe ametumia DIPLOMASIA na busara kuwajibu Sauti ya Watanzania.
 
..suala la maandamano halipaswi kuharakishwa.

..wacha mikutano ifanyike kuelimisha wananchi, na wakishahamasika ndio maandamano yafanyike.
Miaka 30 mikutano inafanyika bado Wananchi awajahamasika?
 
..response hiyo ni baada ya Adv.Mwabukusi kudai vyama vya upinzani ni magenge ya kusaka ubunge na ruzuku na havitetei maslahi na agenda za wananchi. Na Mbowe ametumia DIPLOMASIA na busara kuwajibu Sauti ya Watanzania.

Si ulisema hakuna mgogoro unakuzwa na watu? Tena ukasema suluhu ni kupoteza muda? Sasa haya ya uliyoandika hapa ya Nini Tena?
 
Ngombe wewe Mbowe anafungwa magereza miezi 8 kuna kima aliandamana ili Mbowe achiwe?
Hakuna mwenye akili TIMAMU aandamane kwa ajili ya maslai binafsi ya mtu flani.Angekua anapigania maslai ya wananchi Mbowe asingekaa ndani hata nusu dk
 
Matarajio yetu kwa Mwamba Mbowe yako pale pale.

Huko Maria Space Bundi waliohongwa ili watengeneze mgogoro ndani CHADEMA tunawajua.

People's Power ✌️✌️✌️
 
Back
Top Bottom