Mbowe na siasa zake za "I am the only negro incharge in here"

Mbowe na siasa zake za "I am the only negro incharge in here"

Mbowe anadhani kuwapigisha ukunga wananchi mikutanoni kunaweza kuifanya CCM ilete katiba mpya.
Kitu pekee cha kuifanya CCM ilete katiba mpya ni mass action, na CHADEMA inayo nguvu za kusiaidia hilo. Ila viongozi wake akina Mbowe wao wanawaza ruzuku, nyomi, ubunge 2025, uenyekiti endelevu na wasirudishwe jela tena baasi.

Hizi siasa zetu zisipobadilika na kuwa za ngangari ngunguri hatutoboi. Unfortunately, Mbowe hayuko tayari kuraise up the stake na kuitia kibano kikali CCM na serikali yake!. Labda anaogopa kesi yake isije ikafufuliwa tena!
 
Huyu anaangaliwa kwa jicho la wasiwasi na wasaka ubunge wa mwaka 2025 ndani ya CHADEMA. Wanaona misimamo yake itamkasirisha "mama". Na hawataki hilo mama asije akawafanya kitu mbaya kama JPM alivyofanya mwaka 2020.
Kundi hili la wasaka ubunge linapay lip service tu ya katiba mpya, lakini haliko interested nayo kiviiile!.
Wao ubunge ni kitu number one!
Dhambi mbaya anayoifanya Mbowe ni kuonyesha kumtenga Lissu waziwazi.
 
Mbowe anadhani kuwapigisha ukunga wananchi mikutanoni kunaweza kuifanya CCM ilete katiba mpya.
Kitu pekee cha kuifanya CCM ilete katiba mpya ni mass action, na CHADEMA inayo nguvu za kusiaidia hilo. Ila viongozi wake akina Mbowe wao wanawaza ruzuku, nyomi, ubunge 2025, uenyekiti endelevu na wasirudishwe jela tena baasi.

Hizi siasa zetu zisipobadilika na kuwa za ngangari ngunguri hatutoboi. Unfortunately, Mbowe hayuko tayari kuraise up the stake na kuitia kibano kikali CCM na serikali yake!. Labda anaogopa kesi yake isije ikafufuliwa tena!
Uko sahihi sana.
Kila siku naimba kuwa Mbowe sasa ni kikwazo
 
Mbowe ningemdharau sana kama angeshiriki haya maandamano ya akina Slaa na Mdude, mtu yoyote mwenye akili aliyeona ile press conference yao ya kuipa serikali siku 30 angesema hawa watu ni vichaa
Shida mmeaminishwa na Mbowe kuwa mabadiliko ni kubembelezana na watawala kwa mnachoita maridhiano.Ukisilikiliza kauli ngumu kama za akina mdude lazima upagawe coz sio ulichoaminishwa na Mbowe. Tuseme kweli,siasa za Mbowe ndio CCM wanazitaka, ni siasa zisizowanyima usingizi na ndio maana wamewaacha wazunguke nchi nzima. SIASA za akina mdude ni mwiba kwa CCM ndio maana wanapambana kuzizima na ndio siasa zinazotakiwa nchi hii.Ukiona unapiga siasa na watawala wako kimya jua unapoteza muda tu.Piga siasa hadi kesho usikie watawala wametuma jeshi lao kuzima na hapo ndio utajua kweli sindano zimewaingia
 
Dhambi mbaya anayoifanya Mbowe ni kuonyesha kumtenga Lissu waziwazi.
Amekuwa na soft speech sana mwenyekiti sijui kipi kimemkuta? CCM wanahitaji nginjangija kama ya TL tofauti na hapo ni kupoteza muda tu.
 
Hayo ni mawazo yako.Usidhani watu wote hawana akili kama wewe.Mnafikiri kazi ya siasa kwenye hizi nchi nikama kwenda chooni kutoa haja.Wewe baki na mtazamo wako ila muda utakuja kukupa majibu ni nani yuko sahihi kati ya mbowe na wafuasi wake na wewe ambaye kauli zako zinaonyesha unatamani wakwame.
Shida ya Chadema na wafuasi wake ni ujuaji mwingi. Hamuwez itoa CCM madarakani kwa siasa za Mbowe na genge lake. Kama mnalengo la kupiga porojo sawa ila kama ni kuitoa CCM madarakani kwa siasa uchwara hizi msahau. CCM inajivunia uwepo wa siasa kama za Chadema
 
Chadema kimekuwa chama MFU kwa sababu ya mbowe na siasa zake za udini na ukabila
 
Hebu fikirieni hili suala:

Umma wa Tanzania umeanza kuamka, unakataa udalali wa rasilimali zao, unaanza polepole kukataa chapa waliyopigwa kwa muda mrefu, unaanza kuchukua hatua ya kupeleka Struggle katika hatua ya pili ya matendo badala ya maneno. Cha kusikitisha anatokea kiongozi mmoja wa Taasisi muhimu ya wananchi, ambaye kwa nafasi yake, na mizizi ya taasisi yake angeweza kusaidia pakubwa kuwatoa wananchi kutoka katika kongwa hili la kutochukua hatua yoyote ya kuiadabisha serikali yao kutokana na madudu makubwa inayofanya yeye anarudi nyuma, na matokeo yake kuisaidia CCM kuzima cheche ambazo zingesaidia kutengeneza moto mkubwa wa mabadiliko huko mbele. Ni ajabu sana!

1. Mbowe na siasa zake za ki "Uncle Tom".
Kipindi cha utumwa huko Marekani na Jim Crow, walikuwepo wamarekani weusi ambao kwa kuwa wao walikuwa na vijinafasinafasi katika mfumo wa Marekani, walikuwa wakipenda kujitapa kwa kauli za "I am the only negro working as an engineer here", "I am the first black clerk in here". Leo hii Huwezi kushangaa kumsikia Mbowe akijitapa na kauli yake maarufu ya siasa za nchi hii ni ya Farasi wawili, CCM na Chadema. Na hii Mentality ndiyo inayomsukuma kutaka alambwe miguu pale wananchi wanapotaka kusogeza struggle kwenda next level, Ili kuitia kibano serikali ya CCM katika suala la bandari na katiba mpya. Ndiyo maana Juzi huko Zanzibar, huku akisimama kwa kujitapa mbele ya wazee wa chama anahoji eti Chadema haikushirikishwa katika maandalizi ya mikutano na maandamano ya kuibana serikali ya CCM katika suala la katiba mpya na Bandari. Yaani anataka apigiwe magoti na wananchi kwenye struggle za kuitia kibano serikali, yeye nani?!

2. Mbowe amesaliti struggle za Watanzania kupeleka struggle next level
Sijui kama Mbowe na chawa wake ndani ya Chadema wanatambua athari za walichokifanya dhidi ya struggle za Watanzania katika kujikomboa kutoka katika minyororo ya Siasa chafu na uongozi mbovu wa CCM. Badala ya kuweka ego ya Kiuenyekiti, na ego ya uchama mbele, Mbowe alipaswa aangalie picha pana ya movement ya wananchi ya kutaka kuitia kibano Serikali ya CCM zaidi katika suala la bandari. Infact struggle hii inacompliment kabisa jitihada za chama cha Chadema za kudai katiba mpya. Badala ya Mbowe kuwapiga Rungu Sauti ya Watanzania, kama kweli angekuwa anahitaji mabadiliko ya kweli nchini, alipaswa aweke ego yake pembeni na kuwasaidia kadri inavyowezekana. Hii ingesolidify movement ya mabadiliko kutoka pande zote za kijamii na kisiasa za kuleta mabadiliko nchini. Lakini cha ajabu at the critical hour, Mwenyekiti kama kawaida yake ANABADILI GIA angani.

3. Jeuri ya Nyomi mikutanoni na kudhani Chadema haihitaji Sauti za mitandaoni

Inavyoelekea, wingi wa watu katika mikutano ya Chadema umeanza kuwapa kiburi viongozi wa Chadema na kudhani kuwa nyomi hilo linamaanisha kushinda chaguzi na labda eti hiyo ndiyo force pekee inayoweza kuipeleka Chadema mbele. Nataka nimwambie Mwenyekiti Mbowe na Chawa wake ndani ya Chama kuwa kudhani hivyo ni very naive, Maana hata kama hilo nyomi lote litaichagua Chadema, kama hakuna katiba mpya, tume huru ya uchaguzi ni kazi bure. Ndiyo maana ni ujinga mtupu kubeza cheche za struggle ambazo zitazaa moto wa mabadiliko ya kisiasa na kijamii nchini yatakayoisaidia hata Chadema yenyewe. Na mtu yeyote anayedharau kundi la wananchi ambalo liko "Enlightened" basi huyo hajielewi.
Na labda tu nimwambie Mbowe, kuwa pengine Nyomi la mikutano linamtia kiburi na kuamini kuwa Hakuna haja ya kuwaengage Watanzania wa mitandaoni. Asu biri aone kama CCM nao watapita katika kaya hizohizo anazopita leo watu walewale waliojitokeza kumsikiliza hawatakwenda kuwasikiliza CCM. Ni Ujinga kudharau movement ya kundi dogo wenye uelewa ktk society

4. Akili za kuwaza ubunge, wingi wa ruzuku na kuendelea kuwa Mwenyekiti.

Siyo siri, viongozi wengi ndani ya Chadema ya leo wanawaza ubunge tu mwaka 2025. Ni wachache sana miongoni mwao wanaowaza beyond ubunge. Na hii sauti ya waota ubunge ndani ya chama ni kubwa zaidi kuliko wale ambao Genuinely kabisa wanawaza mabadiliko ya kweli ya kimfumo nchini. Ukisikiliza kauli za viongozi wengi wa Chadema wako more worried na uchaguzi mkuu ujao, na ndiyo maana sasa wanazungumza habari za mabadiliko ya katiba kuelekea uchaguzi. Hoja zilezile ambazo miaka mitatu iliyopita walikuwa wakiwatukana ACT kwazo, ndiyo hizohizo leo wanazileta kwetu kama eti ni maono ya hekima ya chama. Kama hekima zinapatika ndani ya miaka mitatu, basi maana yake huko nyuma hakuwa na hekima anyway.

5. Mbowe kama Gatekeeper.

It seems Mbowe, hayuko tayari kwa massive action nchini. Yaani anadhani kuwa CCM itatuleta mabadiliko kwa kuombwa, kwa kujitungia sheria za kujidhibiti yenyewe, kwa kuombwa kuleta katiba ya kujimaliza yenyewe. Na CCM kwa kutambua udhaifu wa Mwenyekiti katika mambo makuu matatu, Mosi anautaka uenyekiti tena, Pili ni muoga wa kupush hard na Tatu ana maslahi nchini ambayo wanaweza kumblackmail nayo basi wako Comfortable kuwa Mwamba ataruka na chopa, ataongea rousy speeches lakini itakapokuja muda ambao Watu wanataka kuraise up, basi Mwenyekiti atatumia machinery ya chama chake kujiweka pembeni na kuwaacha wanaotaka kuraise wakiwa marginalized. Ni jukumu la Wanachadema kukifanyia review chama chao waone kuwa The same Old Mwenyekiti ana kipya au sasa ni time ya Change ili kupush mabadiliko ya kweli nchini.

6. Mwisho.
Hapa nataka nitoe tahadhari kwa viongozi wa Chadema ambao wameanza kuwa arrogant kwa kudhani Chadema is too big, na hawahitaji kuchangamana na watanzania wengine hasa wa mitandaoni.

Iko hivi, ni sisi wananchi wa Mitandaoni tuliopiga presha mpaka Mbowe akaachiwa. Ni sisi wananchi wengine wengi tu tusio na vyama lakini tuliokuwa tukiichangia Chadema katika operesheni zake. Ni sisi ambao tumeipa moral support, kwa kauli na matendo Na infact ni sisi ndiyo tunaolipa kodi ambayo leo hii Chadema wanapata ruzuku. Hii arrogance ya kijinga ambayo kwa bahati mbaya naona mnayo kuwa Walioko mitandaoni hawana dili, itakuja kuwatokea puani pale sentiment zitakapoanza kuwa negative kwenu na chama chenu. Kama mnabisha kaiulizeni ACT kwa nini haitoboi Tanganyika. Kawaulizeni negative content inawaathiri vipi!. Sasa msitufikishe huko.
Kama kweli Chadema ni chama cha wananchi, basi hiyo Taasisi ifanye kazi ya wananchi. Tunheshukuru kama Ingeshirikiana na Sauti ya Watanzani kuibana CCM zaidi, Kuitia kibado zaidi CCM kwenye suala la bandari na katiba. Kinyume cha hapo ni kuipa life support CCM na huo ni usaliti.

Nawasilisha!
zitto junior JokaKuu Tindo Nguruvi3 Uzima Tele Pascal Mayalla brazaj Kalamu The Boy Wonder ....
 
..suala la maandamano halipaswi kuharakishwa.

..wacha mikutano ifanyike kuelimisha wananchi, na wakishahamasika ndio maandamano yafanyike.
Kama ndiyo hivyo kulikuwa na sababu gani ya kubeza wengine kwa kuwaita ni pressure group? Kwanini kama viongozi wasingefanya mawasiliano na wakashauriana?
 
Wanaharakati huru wanaruhusiwa kufanya harakati zao za upatikanaji wa katiba mpya na kuzuia kuuzwa kwa bandari.
Wasitegemee mgongongo wa chama chochote cha siasa kuanzia sisiem hadi vyama vya upinzani.
Ccm wana rasimu yao wanayoiita katiba mbadala, wananchi wana rasimu ya Warioba inayohujumiwa.
Wanaharakati waje na ya kwao.
Kutegemea kuungwa mkono na upinzani mfano wa chadema ni sawa ila wakubali hilo sii jukwaa moja kwani kwa njia hiyo ccm wanaweza kueneza propaganda kuwa hii ni katiba ya chadema.
Kila kundi lipambane kutokea angle yao na ikifika mahali fulani ndipo nguvu ziunganishwe.
Kundi moja kutaka huruma za kundi jingine ni kuhujumu au kukwamisha dhamira njema ya upatikanaji katiba mpya.
Wanaharakati huru achaneni na mbowe na chadema, lakini katika masuala ya msingi ndipo iunganishwe nguvu.
Hili la kutuhumiana limeshaipa nguvu ccm kuhujumu harakati kwa kuzingatia kigezo cha kwamba watu hawa wanegawanyika na hivyo kuwatwanga ni rahisi maana hawana lugha moja.
 
Nimshangaa anavyojitapa kukwamisha jitihada za wananchi kuitia kibano serikali ya CCM kwenye ishu ya katiba mpya na bandari.

Badala awaone Sauti ya watanzania kama natural allies, yeye anaweka mbele ego yake tu ya uwenyekiti mbele.

OK sawa, wewe ni mwenyekiti so what?
Kuna jambo wengi hawawezi kulifafanua
The guy anatuchezea akili na vile wadanganyika wameruhusu basi safari ya ukombozi ni ndoto
Mkulu anafanya teuzi nje ya nchi, anavunja Katiba left right n center anatembea kila siku kwa shughuli hazieleweki opposition wapo kimya
Inafikirisha sana
 
Kama ndiyo hivyo kulikuwa na sababu gani ya kubeza wengine kwa kuwaita ni pressure group? Kwanini kama viongozi wasingefanya mawasiliano na wakashauriana?

..Kama Mbowe alisema hivyo basi atakuwa amekosea.

..Labda alikuwa anajibu kauli ya Adv.Mwabukusi kwamba vyama vya siasa ni magenge ya ubunge na ruzuku.

..Sasa ukiacha hiyo minyukano ambayo haina maana, hali ya mahudhurio na hamasa ktk mikutano ya hadhara haionyeshi kwamba huu ni wakati sahihi wa kuitisha maandamano.

..Tujifunze toka kule walikoitisha maandamano na wakafanikiwa. Je, hali yetu ya kisiasa inalingana nao?
 
..suala la maandamano halipaswi kuharakishwa.

..wacha mikutano ifanyike kuelimisha wananchi, na wakishahamasika ndio maandamano yafanyike.
Mnaelimisha nini ambacho wananchi hawajui?Mnatofauti gani na CCM wanaosema swala la katiba wananchi wapewe elimu kwanza?
 
Mnaelimisha nini ambacho wananchi hawajui?Mnatofauti gani na CCM wanaosema swala la katiba wananchi wapewe elimu kwanza?

..maandamano ni zao la mikutano mikubwa yenye hamasa ya hadhara.
 
..maandamano ni zao la mikutano mikubwa yenye hamasa ya hadhara.
Huko walikopita wameacha hamasa gani?Operation wanazofanya akina Mbowe ni utapeli na uhujumu kodi za wananchi. Wananchi wamechoka na ccm na hakuna asiyejua ubaya wa ccm saizi.Kinachotakiwa ni mass action tu na sio kuendelea kuleta porojo. Swala l bandari halikuhitaji porojo zaidi ya Mbowe kuitisha maandamano nchi nzima. Huko Kenya mbona hatusikii porojo za kutoa elimu wanapokua na jambo lao?Bei ya unga imepanda,Odinga ye ni kuwaingiza wafuasi wake barabarani. Hakuna porojo kama za akina Mbowe huku
 
..kama hali ya hamasa imefika hapo basi yeyote yule anaweza kuitisha maandamano hakuna haja ya kumlalamikia au kumkoromea Mbowe au Chadema.
 
..suala la maandamano halipaswi kuharakishwa.

..wacha mikutano ifanyike kuelimisha wananchi, na wakishahamasika ndio maandamano yafanyike.

Hii hoja ya wacha wananchi waelimishwe kwanza ndiyo hoja hiyo hiyo Samia anaitumia kwenye katiba mpya kuwa "wacha wananchi waelimishwe kwanza".

Sikia elimu haina mwisho!. Ila kuendelea na mfumo huu wa sasa hata kwa mwaka mmoja mbele ni mzigo!. Thats why cheche zozote za kupeleka struggle to the next level lazima zisaidiwe, zilelewe, ziungwe mkono na ziwezeshwe. Siyo kurudia the same old politics ambazo Mbowe kazifanya kwa miaka zaidi ya 20 sasa na tuko palepale!.
Insanity is doing the same thing over and over again expecting different results!
 
..kama Mbowe anaonekana hafai basi wajitokeze wengine wenye uwezo na mbinu mpya.

..kwanini nguvu kubwa inaelekeza kumlaumu Mbowe kuliko kudai katiba mpya?

..Nadhani tumepoteza muelekeo hivi karibuni.
 
Back
Top Bottom