Mbowe na siasa zake za "I am the only negro incharge in here"

Mazingira ya kisiasa na utamaduni wa kisiasa yametofautiana sana kati ya Kenya na Tz.
 
MBOWE ni msaliti hilo halitaki elimu ya PHD.
Ni manyumbu tu ndio kawashika akili.
Alituletea aliyemwita fisadi mkuu aje agombee Urais kupitia UKAWA. yaani Umoja wa Katiba ya Wananchi.

Wakati huyo Lowasa hakuwa hata na mpango na hiyo katiba ya wananchi. Alipokatwa CCM akakimbilia UKAWA kwa vipande vya pesa akanunua ugombea urais usiopingwa wala kushindanishwa.

Bila aibu leo manyumbu wake mnamtukana Dr Slaa eti ni msaliti
wakati msaliti wa kweli ni Mbowe.
 
Mbowe na Chama chake wanafanya siasa za kujiandaa kushika dola.

Siasa ambazo ACT-Wazalendo imefanikiwa kulinganisha Chadema.
 
Hahahaha hahaha
Mkuu nimecheka si kwa sababu ninacheka ujumbe wako, la hasha. Bali umeongea point kubwa, ngumu na yenye mantiki kubwa. Umeongea kwa lugha ya mwalimu anayewahamasisha wanafunzi wake kabla ya kuingia kwenye final exams, umeongea kama kocha wa basketball anayewahamasisha wachezaji ktk last quarter.

CHADEMA kina mamluki wengi ndo maana unaona wengi waliokuwemo humo wakarudi zizini wamepewa nafasi kubwa ndani ya chama na serikali. Ninaowona kuwa serious ni Lissu, Boniface Jacob, Lema, Masese na Erythrocyte kwa nafasi ya juu huko.


Institutionally CHADEMA inapaswa kwa sasa kuziba ombwe la mkwamo huu wa kisiasa na kiuongozi kwa kuja na mikakati inayojenga ari, uthubutu na uzalendo kwa wananchi kuikataa dhambi (CCM) kivitendo.

Upo sahihi
 
Kila zama na mambo yake, kwa mika 20 Mbowe amafanikiwa kuijenga Chadema kama taasisi imara, na hiyo itabaki kuwa legacy yake.

Sasa baada ya ukuaji na kujiimarisha chama kinahitaji kufanya kazi yake muhimu ya kushika dola, na kwa hakika Mbowe hana speed hiyo.

Kabla ya kuwekwa mahabusu kulikuwa na vuguvugu kubwa kuhusu katiba mpya, nq nilitegemea kungekuwa na nguvu ile ile pengine zaidi baada ya kesi yake kuisha, ila ni tofauti, baada ya kutoka speed yote ikazima mpaka leo.

Mbowe anapunguza speed ya mabadiliko, na hilo ndio furaha ya chama tawala.
 
Mazingira ya kisiasa na utamaduni wa kisiasa yametofautiana sana kati ya Kenya na Tz.

Labda kama una maana Kenya hawana adui wala rafiki wa kudumu. Pia Kenya vigogo huhamasisha na kushiriki maandamano.

Kauli za mazingira tofauti ni potofu.
 
Wanasiasa wengi Afrika, ni wezi, wanafanya primitive accumulation of wealthy, kwao siasa is a "means to an end" Kupiga pesa, kupata influence, na power,
 
Sina hakika kama unaelewa mantiki ya hiki ulichokiandika hapa...

Unasema kuwa Freeman Mbowe na CHADEMA ni wasaliti kwake kwa sababu ya Edward Lowassa wa 2015...

Well. Kama anatambua hilo, anatafuta kitu gani tena huko? Amesahau kitu gani tena huko CHADEMA kiasi cha kuanza kulilia msaada wao kwenye harakati zake za kisiasa na hao wenzake?

Je, umeweza sasa kuona kuwa hoja yako hii haina connectivity ya kimantiki kabisa?

Na jibu ni moja tu kuwa, likey Dr Wlbroad Slaa hana nia njema na CHADEMA na ndiyo maana watetezi wake mnajichanganya bila hata kujua...

Na huu sasa ndio unyumbu halisi..!!
 
Dr Slaa hajaitafuta CHADEMA na wala hajaonba kurudi CHADEMA.
Wazalendo wa kweli Dr Slaa, Adv Mwabukusi, Mdude nk baada ya kuona inchi inaingizwa kwenye mikataba ya kilaghai huku vyama vya siasa vikiwa kimya ndipo waka form hicho kinachoitwa Sauti ya Watanzania.
Lengo ni kuunganisha nguvu za vyama vyote na hata taasisi zote kuungana kudai katiba mpya nakupinga uuzwaji wa bandari.

Mbowe Kagoma kushirikiana na sauti ya watanzania kupinga uuzwaji wa bandari wala kudai katiba mpya.
Anadai hakushirikishwa!
Buliaga alienda kufanya nini?

Hadi hapo bado huoni usaliti wa Mbowe?
Huoni km anamaslahi binafsi ktkt hili na sio maslahi ya kitaifa?
 
Bado hujui usemalo..!
Well and good. Mpaka hapo hakuna shida. Ni haki yao kabisa
Lengo ni kuunganisha nguvu za vyama vyote na hata taasisi zote kuungana kudai katiba mpya nakupinga uuzwaji wa bandari.
Wameshaunganisha vingapi? Ni kipi na kipi kwa majina?
Mbowe Kagoma kushirikiana na sauti ya watanzania kupinga uuzwaji wa bandari wala kudai katiba mpya.
Anadai hakushirikishwa!
Ooh, kumbe ni Mbowe ndiye kagoma na sio CHADEMA? Sasa kama kweli hakushirikishwa, shida yako ni nini? Si urudi kwake Tena ili umshirikishe vizuri aone kama anaweza kushirikiana nawe au la?
Hadi hapo bado huoni usaliti wa Mbowe?
Unaelewa hata maana ya maneno "Usaliti" na "msaliti" kweli wewe? Kukataa kuridhia ombi lako yawezekana vipi iwe ni usaliti?
Huoni km anamaslahi binafsi ktkt hili na sio maslahi ya kitaifa?
Kwani akiwa na maslahi binafsi Kuna shida gani? Wewe huna maslahi yako binafsi?

Fikiri kwanza unapojenga hoja ndipo useme au uandike. Hapa unaoendelea kujichanganya tu Kwa sababu hakuna mantiki ya Kila unachoandika!!
 
Basi sawa,
Wewe humuamini Dr Slaa
Mimi simuamini Mbowe
 
Basi sawa,
Wewe humuamini Dr Slaa
Mimi simuamini Mbowe
Haa haa 🥺

Umenena vyema. Lakini mimi niko tofauti kidogo na nitakushangaza kwa kusema..

Nyakati zingine naweza nisimwaamini yeyote na pia wakati mwingine naweza kumwaamini yeyote. Waswahili husema......inategemea....

Na actually, hii ndiyo sifa anayopaswa kuwa nayo binadamu yeyote aliye perfect..

Wa kumwaamini kwa 100% siku zote ni mmoja tu. Ni Mungu muumba pekee..!!

Kwa heri na Asante kwa kushiriki mjadala..
 
Mkuu nazungumzia ktkt huu mjadala ulio hapa jamvini.
Wewe humuamini Dr Slaa
Mimi simuamini Mbowe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…