Mbowe na Wenzake 3 wakutwa na kesi ya kujibu. Kesi imeahirishwa hadi Machi 04, 2022 watuhumiwa kuanza kujitetea

Kanawe miguu ulale hapo kwenye banda la mbuzi
 
Toka lini mahakama za kitanzania zikawa huru,huyu jaji anahukumu mfukoni tufanye mambo mengiine,wameshaamua kumfungaa,wao waseme wanamfunga miaka mingapi ,tusipotezewe muda na comedian waliojificha kwenye kimvuli cah ujaji tujadili mgao wa umeme,bei za vifaa vya ujenzi kupanda,bei za mafuta kupanda ,katiba mpya na mengneyo
 
Dah...nimechoka kabisaa Mungu tu sasa aingilie kati aisee vinginevyo Mbowe tunamkosaa😴😴😴😴
 
Hakuna kitu unaweza kuficha kwa MUNGU ndiyo maana nimekwambia KWA HAKI HATAHUKUMU MATAIFA. Hata kwenye hii Kesi AMELITIZAMA WAZO LENU TOKEA MBALI NA NIA ZENU. Tumia akili ya kawaida kwanini Urio aliyemtafutia gaidi mbowe watu wa kufanya Ugaidi alafu kesi isimuhusu kuwa mshitakiwa?

Kwanini awaingize vijana wa watu ambao hawakuwa hata na wazo mfano mmoja alikuwa anajipondea kokoto alishe familia yake. Alafu wajinga wanamuona Urio Ni shujaa.

Alitakiwa baada ya kujua Nia mbaya ya Ugaidi ya mbowe wangedili na mbowe bila Urio kuwaingia wasiokuwa hata na nia mbaya.

Hii kesi ina Ushetani mwingi sana kwa wenye uwezo wa kufikiri. Kama ule Ushetani uliokuwa wa kumuua Lisu mwisho wa siku shetani kashindwa kumchunguza shetani mwezake.
 
Itakuwa upunguani kumuita mtu anayekushtaki akutetee, ataibomoa kesi yako na kwa mzaha wako wa kufikiri utamdhalilisha kwenye doc mteja wako akaishia jela.
Dah! Kwaiyo wewe unaijua hiikesi kuliko kibatala na jopo lake??? Kwikwikwiiii...
 
Kwahiyo usipo ajiriwa kwa vigezo ulivyotaja basi tafsiri yake ni umeajiriwa kwa ugaidi?
Muwe mnatumia akili kutetea ujinga wenu ebooo

Kwani umeambiwa ile ni kesi ya mikataba ya ajira?
 
Dah! Kwaiyo wewe unaijua hiikesi kuliko kibatala na jopo lake??? Kwikwikwiiii...
Ninyi wanawafanyia uanasheria wa ki comedy, kifutuhi futuhi, ili mfurahie kwenye space ya maria muendelee kuwachangia, lakini kisheria hakuna sanachokifanya TRIAL WITHIN TRIAL ambayo ilikuwa sehemu muhimu walishindwa na hivyo caution statement zikapokelewa, na sasa Kwenye PRIMA FACIE nako wameshindwa sasa huo ubora wao kisheria uko wapi?

Mawakili wa serikali wanajua wanachokifanya, ni fact gani wanatakiwa ku prove na sio kupoteza muda wa mahakama kwa pumba, ndio maana mashahidi hao maswali yale ya kijinga walikuwa wanajibu sijui

Hivi unajua kuwa akina kibatala sasa hivi hawana nafasi ya cross examination lakini nafasi yao ni EXAMINATION IN CHIEF na RE EXAMINATION IN CHIEF

Unajua effect yake kisheria? Kama watamwita shahidi wa upande wa jamhuri wao watamwongoza kwenye ushahidi bila kuwa na leading questions na baadaye wakili wa serikali atakuwa na nafasi nzuri sana ya kuibomoa kesi yao kupitia cross examination ambapo watakuwa wanajenga nyumba mboja.

Na mahakama haiwezi kuchukua procedure za hostile witness ili awe cross examined kwa sababu from the beginning msimamo unsjulikana yupo upande gani
 
Ni muhimu sana mahakama kutenda haki na ionekane kwamba imetendeka.
Mahakamani siyo sehemu ya kamari kama fikra za wengi zilivyo.
Hukumu za kesi zinatolewa kutokana na kusikiliza mashahidi na kuchambua vielelezo kwa akili ya kawaida pamoja na mtazamo wa kisheria.
Narudia "Akili ya kawaida (common sense) inazidi hata shahada.
Maamuzi madogo au hukumu za kesi kama hii, lazima zielezewe vizuri kwa wananchi ili wajenge Imani na mahakama vinginevyo tutajenga kizazi kinachofikiria kuwa hata maamuzi ya mahakama ni kama kamari.
 
Mbowe aache dharau aliambiwa muda tu, sasa hivi anatia huruma sana, aache dharau si aliambiwa, hii case itampiga ndani
 
Hii kesi mkuu Inaufadhili wa sukuma gang ,kundi hatar kabisa linahitaj mashahid majina yao na anwani ili wakanunue kesi ,ila wajue huu si uchaguz ya kwamba wataiba kura ,kitu kipo mezani.

Naona mawakili wameshupaza kabisa shingo wanataka anuani za mashahidi,,, ili iweje...? kwani watakapokuwa wanawauliza maswali si watawauliza anuani zao...??

Ni jambo lina msingi sana kwa upande wa mashtaka???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…