Pre GE2025 Mbowe ndiye aliyepambania Uhai wa Lissu kwa Jasho na Damu Mpaka Kumvushia Nairobi Kenya lakini leo Lissu anampaka matope na kumuona hafai

Pre GE2025 Mbowe ndiye aliyepambania Uhai wa Lissu kwa Jasho na Damu Mpaka Kumvushia Nairobi Kenya lakini leo Lissu anampaka matope na kumuona hafai

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Tenda Wema nenda zako na wala usisubiri shukurani,ni bora Umfadhili Mbuzi kuliko Mwanadamu.Duniani hapa Watu wanaumizwa na Wameumizwa sana na watu wale wa karibu sana yaani wale ambao waliwasaidia kwa jasho na Damu lakini Mwisho wa siku wamegeuka na kubakia Maadui wakubwa sana.

Watu wengi sana wameingia matatizoni na kupata majuto mazito kutoka kwa watu waliowasaidia.watu wengi sana wameumizwa na wema wao .Wapo watu leo wanabubujikwa na machozi yasiyokata usiku na mchana kwa sababu ya majeraha na vidonda visivyopona vilivyo sababishwa na watu waliowasaidia na kujitoa na kujitolea kwao.

Mwamba wa kaskazini na Jabali la siasa za Upinzani hapa Nchini Mheshimiwa Freeman Mbowe leo anapakwa matope, kuchafuliwa, kuzushiwa uongo, kusemwa vibaya kusingiziwa kila aina ya uongo, kutukanwa, kubezwa kudharauliwa na hata kutupiwa kila aina ya shutuma kutoka kwa watu aliowakuza, kuwalea na kuwasaida kwa jasho na Damu.

Leo anaumizwa,kuzushiwa uongo na kuchafuliwa na watu walio ndani ya CHADEMA au ambao wapo nje ya CHADEMA lakini walipita mikononi mwake na yeye ndiye akawasaidia mpaka kupata Uongozi kama vile Ubunge japo walikuwa Makapuku na choka Mbaya na wasiofahamika kabisa kwa watanzania lakini Leo ndio wamegeuka kuwa maadui zake wenye kuongoza mashambulizi ya kumchafua, kumpaka matope na kumzushia kila aina ya uchafu.

Ni haohao aliowabeba na kuwasaida na kuwatambulisha mbele ya macho ya watanzania licha ya Umasikini wao, kuchoka kwao kimwili na kupoteza nuru hata ya macho kutokana na njaa zao lakini Leo ndio wapo mstari wa mbele kumrushia mishale ya kila aina kutaka kumuangamiza.

Kwa hakika inaumiza sana kibinadamu,inatia sana hasira, inaleta uchungu na kusononesha sana na kwa hakika kwa mtu mwenye akili Timamu na unayejitambua kamwe na katu huwezi hata kidogo kuwaamini watu wa aina hiyo wanaomshambulia Mbowe kwa sasa wakati unajua kuwa wamefika hapo walipofika na kutambulika hapa Nchini kupitia Mabega na mikono na Msaada wa Mbowe mwenyewe.

watu hao hawapaswi kuaminika wala kuwaamini popote pale wala kuwakaribisha chumbani kwako au hata kuwaonyesha funguo za nyumba yako zinapokaa. Haupaswi hata kuwaacha watoto wako kwao maana ipo siku utakuta wamefanyiwa ukatili na unyama usiomithirika.

Kama wewe mwenye akili Timamu unatambua mchango wa Mbowe kuwasaidia watu hao lakini Leo ndio wanamchafua Mbowe.je wewe ni nani mpaka ufikirie kuwa huwezi kusalitiwa na kuja kutukanwa na watu hao? Wewe ni nani mpaka ufikirie kuwa hao watu au huyo mtu hawezi kuja kukugeuka na kukusaliti?

Mbowe ndiye mtu aliyepambana kwa jasho na Damu kupambania uhai wa Lissu.ndiye aliyefanya juhudi zote kuhakikisha Lissu anapata ndege ya dharura itakayo msafirisha Lissu kutoka nje ya mipaka ya Tanzania ni Mbowe ndiye aliyeweka kambi Nairobi Kenya kusimamia matibabu ya lissu lakini leo Mbowe analipwa kwa mabaya, leo anaonekana hafai,leo anaonekana ni mtu wa hatari ,leo anaonekana hafai kwa lolote lile .Leo Mbowe anaambulia kejeli,dharau,matusi ,kuchafuliwa na kupakwa Matope ya kila aina.

Leo maadui zake wakubwa ni wale aliowasaidia na kuwapigania.

Kwa hakika ni bora Mfadhili Mbuzi tuuu kuliko Mwanadamu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Mbowe Hafai kuwa mwenyekiti kwa sasa haina maana hafai kuwa binadam!

Siasa ni kama mpira! Kubadilisha kocha haina maana yule kocha mnamchukia!
Yanga walimfukuza Gamondi pamoja na kwamba aliwafunga simba!

Kama hoja ni kumpeleka hospital basi chama kiteuwe dakitali kuwa mwenyekiti!
Wacheni kujitutumua tundu lissu kupona kwake ilikuwa ni mapenzi ya Mungu!

Kwasasa chadema inahitaji kocha mpya ambae ni tundu lissu!

Tumechoka michezo ya mbowe haituvushi hasa kwa aina hii ya siasa za sasa ambapo Ccm kutumia Dola
 
Mbowe Hafai kuwa mwenyekiti kwa sasa haina maana hafai kuwa binadam!

Siasa ni kama mpira! Kubadilisha kocha haina maana yule kocha mnamchukia!
Yanga walimfukuza Gamondi pamoja na kwamba aliwafunga simba!

Kama hoja ni kumpeleka hospital basi chama kiteuwe dakitali kuwa mwenyekiti!
Wacheni kujitutumua tundu lissu kupona kwake ilikuwa ni mapenzi ya Mungu!

Kwasasa chadema inahitaji kocha mpya ambae ni tundu lissu!

Tumechoka michezo ya mbowe haituvushi hasa kwa aina hii ya siasa za sasa ambapo Ccm kutumia Dola
Hakuna Mwenye akili Timamu anayeweza kubali kuona akatoa kura yake ya ndio kwa lissu na kumuacha Mbowe.
 
MWAKA 1961 TANGANYIKA IKIPATA UHURU.

BABA WA TAIFA ALIWATAJA MAADUI WAKUU WA TATU WA TAIFA.
1. UMASIKINI.
2. UJINGA.
3. MARADHI.

AKAMALIZA KWA KUSEMA "MAADUI HAWA NI MAADUI KWELI KWELI NA SI MAADUI WA DHIHAKA"
JK NYERERE
 
Kizza Besigye alikuwa daktari binafsi wa M7. Uswahiba wa Uhuru na Ruto ulikuwa haukamatiki. Raila na ODM wakati ule ngoma inogile!

Ghafla bin vuu akaja Gachagua ndiye akawa bafa mkinga shari ili kumlinda na kumwinua Ruto.

Trump na Mike Pence walikuwa ni rais na makamu wake same as Joe na Kamala same as urafiki wa ENL & JK.

Haji Manara ulikuwa humwambii kitu kuhusu Simba. Na MO daima alihuzunikia mkwanja wake aliouwekeza Msimbazi!

Wema alikuwa kipenzi halisi cha Diamond. Dar ilikuwa makao makuu ya nchi. Juliasi na Sokoine walikuwa wazalendo wa Azimio la Arusha.

Nasari alikuwa shabiki kindakindani wa CDM. Na Waitara hakuisha kukinanga chama tawala kabla ya kutimkia huko kama Msigwa hivi karibuni.

Dkt. Slaa aliwahi kugombea urais chini ya CDM. Zitto Kabwe na CDM, CDM na Zitto Kabwe enzi hizoo!

Airtel ilikuwa Zain, Zain ilikuwa Celtel na Tigo imegeuka kuwa Yas. Elon Musk alikuwa Democrat, lakini sasa hivi yeye ndiye almost usukani, tairi na injini ya serikali ya Marekani!

Hivi unaweza kuamini kwamba kuna wakati hapo zamani ambapo Wapalestina na Waisraeli walikuwa wakiishi kwa amani na utulivu?

Juzi Anko Joni alikuwa rais, leo Sa100 ndiye kinara wa kuapisha viongozi wateule.

Must I continue?
 
Wewe lini umewahi kuwa na akili? Sifa kubwa ya kuwa chawa ni kujitoa akili. Mpumbavu mkubwa wewe unadandia dandia wanaume kama changudoa sasa umeweka kambi kwa Mbowe unafikiri ndiyo atakutoa kimaisha? Utakufa masikini kwa ujinga wako.
Ungeacha wenye akili Timamu na wanaojitambua wajadili hoja.
 
Back
Top Bottom