Pre GE2025 Mbowe ndiye aliyepambania Uhai wa Lissu kwa Jasho na Damu Mpaka Kumvushia Nairobi Kenya lakini leo Lissu anampaka matope na kumuona hafai

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Narudia kusema kuwa CHADEMA inahitaji mtu mwenye akili Timamu na anayejitambua kuendelea kuiongoza.hivyo ni Mbowe ndiye atakayeendelea kuiongoza CHADEMA
wewe utakuwa kilaza au chawa, maana hao ndio aina ya watu walio mzunguka Mbowe.
Lisu hataki machawa.
 
Hivi ccm kutetea viongozi wa chadema imeanza lini?
 
Ushawahi kukataliwa kimapenzi!? ulikuwa hufai kuwa nae kwenye mapenzi lakini sio hufai kabisa apana! ila haukukizi vigezo kuwa kwenye ile nafasi! hivyo hivyo Kwa mbowe ni mwema na mzuri kiutu lakini kwenye maendeleo ya chama huenda ikawa hatoshi! Kwa kusema hatoshi haimaanishi hafai tuelewane ivo msiendeshwe na mihemko yenu hili jambo halihitaji ushabiki tunataka mtu wa kutuvusha hapa tulipo
 
Mtu uliyemfanyia wema sio vizuri umkandamize kisiasa eti kwa kuwa ulimsaidia. Lissu ana haki ya kuhoji.
 
Kwahiyo chama kilipomteua Lisu kugombea uraisi alikuwa hana akili timamu!?
Yaani wamwamini nafas ya urais halafu asifae kwenye uenyekiti wa chama!
Hivi unaakili sawasawa kweli wewe Nyerere?
Kwani hujamsikia mwenyekiti wa Chadema wa Shinyanga?
 
Lissu ni mnafiki tu.
Mbowe ndiyo mnafiki mkubwa katekeleza wajibu wake eti kawatuma chawa mje na masimango, ebu kuweni na Akili kidogo hiki ni kipindi cha uchaguzi kila mgombea ana haki ya kuanika mapungufu ya chama ili akipewa dhamani aweke kila kitu sana
 
Watetezi wa mbowe licha ya kula pesa za mbowe kuweni na Akili kidogo mtambue kuwa huu ni uchaguzi kila mgombea lazima ana haki ya kuongea mapungufu ya chama, msiwapangie wagombea vya kuongea kisa Mbowe alitimiza wajibu wake, kampeni haiendi kwa kufagilia mbowe kijinga jinga
 
Kwa hiyo akimpamhania ndio anakuwa amenunua yaki za Lisu kiasi kuwa Lusu haruhusiwi kusema chochote dhidi ya mpambaniaji hata kama kiovu kweli?
 
aliyetaka kuuondoa uhai huo ni nani? sio mboe huyohuyo?
Zito alipewa sumu, wangwe aliuawa , heche anaugua na sasa Lisu anaishi kwa wasiwasi kila anayewania Uenyekiti huwa Adui wa mbowe na kile kikundi chake wanufaika wa ufisadi na Udikiteta wa mbowe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…