Mbowe ndiye anayewafanya Wajinga na siyo Spika Tulia au CCM!

Yes ..Peace was NEVER an option.
 
Hizo sheria zitaenda kuangaliwa mahakamani.

Anachotaka mwanzilishi wa huu uzi ni Mheshimiwa Rais kuingilia mhimili huru wa mahakama in favour of CHADEMA.

Does anything justify this barbarism?
Kabla ya kwenda mahakamani, kuna jambo Tulia analotakiwa kulifanya kwa nafasi yake, kuwafukuza kina Mdee kwasababu uwepo wao bungeni mpaka sasa ni kinyume cha sheria.

Badala ya kutimiza jukumu lake hili, anakimbilia kuiachia mahakama iamue, hizi ndio delaying tactics zenyewe, hapa Tuloa anaonesha vile hazijui taratibu za mhimili anaouongoza.
 
Ulivyo sema ndio ukweli, japo si kweli rais hajui nini kina endelea. Hao wabunge ni karata ya serikali ili kupata ruzuku toka wafadhili. Aliyo yasema spika ndio msimamo wa serikali. Na kesi haita isha mpaka uchaguzi ujao.
 
Nafasi ya kusikilizwa walipewa wakakimbia hawakuonekana, na hata juzi kwenye Baraza Kuu wamepewa tena nafasi nyingine ya kusikilizwa, wote wakanyama kimya.
 
Awamu ya 5 haikuwajali sana hawa manjagu wetu wanaotumika kuutangazia umma kuwa tuna Demokrasia. Badala yake iliamua kuwatesa na hapa ndipo ushamba wa awamu ile na kuitwa waporipori ulipoanzia.

Mwachini DJ ale kwa urefu wa kamba yake after all yuko smart sana kucheza na akili za misukule.
 
🗣️ Eti Mbowe, kweli huna maslahi ya uwepo wa kina Mdee huko Bungeni?
 

Samia hawezi kuingilia mhimili wa mahakama, maana hapo siyo Spika bali ngoma inachezwa mahakamani. Nawashauri CHADEMA watafute agenda nyingine lakini hawa 19 watawatesa sana! Kama waliandaa majina mengine kupeleka bungeni hiyo wasubiri hadi uchaguzi wa 2025. Kwa kifupi ni kuwa wanapolalia wao wenzao waliamkia huko juzi. Hapo ni kumwaga ugali kwa mboga!
 
Hawezi kuwafukuza wakati bado ni wanachama wa CHADEMA.

Mahakama pekee ndio ina uwezo, kwa sasa, kuamua uanachama wao.

Kama mahakama itajiridhisha mchakato wa kuwaondolea uanachama ulikuwa halali, wataondoka Bungeni mara moja.

Kama mahakama itajiridhisha mchakato wa kuwaondolea uanachama ulikuwa haramu wataendelea na uanachama na Ubunge wao.

Bunge likiwaondoa sasa hivi litaleta mgongano kama mahakama itaamua vinginevyo.

Ndio maana watabakia kuwa Wabunge mpaka mahakama itakapothibitisha vinginevyo.
 
Mbowe alifuata nini Ikulu tena peke yake na yakiwa yamebaki masaa machache kikao kilichowafukuza kina Mdee kufanyika?!

Ni kweli Mbowe hana maslahi ya uwepo wa kina Mdee huko Bungeni?!
Huna namba yake ya simu ukamuuliza? Unadhani sisi tutakuwa na majibu kweli?
 
Hivi Chadema mnaumia nini na riziki za watu?

Kama ni chama si mmeishawavua uanachama?

Sasa mnaacha shughuli zenu ili tu muendeleze ligi na wanawake 19?

Yetu macho!
 

Bungeni walipelekwa na chama chao na ndiyo msingi wa kesi. Sasa tumwachie Jaji ndiye atakayeamua kama walipelekwa na chama au walijipeleka wenyewe, na kesi itatolewa hukumu 2025.
 
Tanzania imecheza pata potea kuruhusu mihimili muhimu ya nchi kuongozwa na wakina mama katika zama hizi. Sina maana ya kuwa mimi ni mbaguzi wa kijinsia, ila namaanisha wanamke wa Kitanzania licha ya usomi wao, ama kuaminika kwao kushika nafasi nyeti za uongozi, halikuwa jambo lenye afya kuwaruhusu kuongoza taasisi nyeti za urais na bunge.

Tutajitoa ufahamu na kuwamwagia sifa kemkem, lakini ukweli unabakia kuwa bado maamuzi yao mengi yanakosa busara ni yenye ukakasi mwingi. Bado wanatawaliwa na munkari na mihemuko ya kike zaidi.

Pasipokuwa hata na sababu yoyote ile ya maana, wanawake wenye madaraka hupenda kuleta mapambano yasiyokuwa na tija ama kupiga chini maamuzi ama matamko ya wanaume.
 
nasema sis bawacha mkit wetu ni mdee.full stop

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe hata hujui unachoandika kwa huo mstari wako wa kwanza tu niliousoma.
 
Bungeni walipelekwa na chama chao na ndiyo msingi wa kesi. Sasa tumwachie Jaji ndiye atakayeamua kama walipelekwa na chama au walijipeleka wenyewe, na kesi itatolewa hukumu 2025.
Una ushahidi gani walipelekwa na chama chao?
 
Mmejifanya wajuaji sasa Ngoja tuone!

Chama kimejaa uhuni, Kimejaa matusi , Chama kimejaa ujanja ujanja!

Haitawezekana tena !!!!!!!
 
Msitupigie kelele, tuko bize na calculations za ongezeko la 23.3% ili tujue ki.a mmoja anapata nini!
 
Kwa hiyo mbowe ndo anavunja katiba ya nchi, tumia akili kidogo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…