Duh!...!. Kiukweli hawa vilaza wa humu, ukiisha wajua, hawakupi taabu!. Unadhani mtu kuelimika ni mpaka uajiriwe na kuteuliwa kuwa fulani, hivyo vilaza hawa wa humu wanadhani mimi nafukuzia teuzi!.
Je, wajua Sio Kila Kumpongeza, ni Kujikomba/Kusaka Teuzi? Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
Kama kazi yako ni mvuvi wa samaki, na kila siku unavua samaki 2, mmoja unamuuza na mwingine ni kitoweo, ikatokea umeupenda uvuvi na unaweza kujikimu maisha yako kwa huo huo uvuvi, ukiamua kujiendeleza kielimu hadi kupata Ph.D, ukaendelea na uvuvi, usimkashifu mtu kama huyo kuendelea na uvuvi huku ana Ph.D kuwa usomi haujamsaidia kitu kwasababu tuu ni mvuvi!, kwasababu sio kila anayejiendeleza kielimu ni anajiendeleza ili aajiriwe!, wengine anajiendeleza kielimu just kuelimika na sio kusaka ajira au uteuzi!.
Mimi ni mtangazaji na always ni mtangazaji, no matter nimesomea nini kingine na nimehitimu elimu ngapi za makaratasi, naendelea na ile ile kazi yangu ya uvuvi wa samaki na naomba nikujulishe sijawahi kuomba kazi popote zaidi ya ile ya kutaka kuwatumikia wananchi na kuitumikia nchi yangu nikakataliwa na yale majinga fulani! ule ujinga fulani!, lakini sitafuti ajira yoyote popote na kwa yeyote!, na wala sisaki uteuzi wowote kuwa yoyote kwa yeyote!.
Ubarikiwe sana!.
P