Pre GE2025 Mbowe: Nikiona chama changu kinaenda kuzamishwa, Kamanda naingia mzigoni

Pre GE2025 Mbowe: Nikiona chama changu kinaenda kuzamishwa, Kamanda naingia mzigoni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe akirudi na lipumba wa cuf karudi, hawa wote waliwahi kugombea urais wakaangukia pua, sasa uchaguzi ujao wataambulia nini kama si kuipa ccm ushindi mnono?
 
CHADEMA kilikuwepo na itaendelea kuwepo bila yeye, tunachotaka ni Chama Imara ambacho hata Kiongozi akifa hakitetereki.
Mbowe amesema kwamba: "Nikiona chama changu kinazama, nitaingia mzigoni".
Tafsiri yake: Bila yeye (Mbowe) hakuna Chadema imara. Hicho Ni chama cha Mbowe; kwa hiyo, si chama kama taasisi Bali ni chama cha kutegemea nguvu ya mtu. Hii Ni hatari Sana.

Tanbihi: mpaka hapo siwapingi wanaosema Chadema Ni Saccoss ya mtu, wengine wanasema Ni Saccoss ya wachaga.
 
IPO HIVI. TUNACHOOGOPA NI MWENYEKITI MTEULE KUAMUA KUUNGA JUHUDI KAMA MSIGWA.
MBOYE PAMOJA NA MAPUNGUFU YOTE NA KUFUNGWA JELA HAJAWAHI KUSALITI CDM KWA MIAKA 30
Kwa hiyo huyu Mzee Mbowe ataishi milele na milele?
 
Hili ndio tatizo la upinzani nchi hii , kuna watu wapuuzi ni undercover humo , wanatumika kuharibu juhudi za mageuzi ya kisiasa nchi hii
ni wapuuzi, wanadhani wananchi hawajui double standard zao
 
Mbowe amesema kwamba: "Nikiona chama changu kinazama, nitaingia mzigoni".
Tafsiri yake: Bila yeye (Mbowe) hakuna Chadema imara. Hicho Ni chama cha Mbowe; kwa hiyo, si chama kama taasisi Bali ni chama cha kutegemea nguvu ya mtu. Hii Ni hatari Sana.

Tanbihi: mpaka hapo siwapingi wanaosema Chadema Ni Saccoss ya mtu, wengine wanasema Ni Saccoss ya wachaga.
Hapana tupo wachagga tunaojielewa ila sio wamachema hovyo kabisa
 
ametoa kauli mbaya sana hivi ingetokea mwana ccm mstaafu atamke kuwa akiona chama chake kinazama ataingia mzigoni ataeleweka vipi? Huo ni uhaini

Mwenyekiti anaye maliza muda wake, Freeman Mbowe amesema ya kwamba iwapo ataona chama chake Cha CHADEMA kinataka kuzamishwa basi ataingia mzigoni. Kwa maana nyingine atagombea uenyekiti wa CHADEMA. Je nani anataka kugombea uenyekiti akizamishe chama.

Kwa kauli hii ya Mbowe Ina maana atagombea uenyekiti. Nadhani Mbowe anafikiri yeye tu ndio mwenye uwezo wa kuisimamisha CHADEMA. Wengine wataizamisha
Mboye aache utani , eti chama changu . Kumbe CHADEMA ni mali yake? Vijana wengi wameumizwa kwa kipigo kupitia mali ya mtu binafsi? Niliwaamini sana chadema kumbe nilikuwa sijui kilichoko nyuma ya pazia
 
Mwenyekiti anaye maliza muda wake, Freeman Mbowe amesema ya kwamba iwapo ataona chama chake Cha CHADEMA kinataka kuzamishwa basi ataingia mzigoni. Kwa maana nyingine atagombea uenyekiti wa CHADEMA. Je nani anataka kugombea uenyekiti akizamishe chama.

Kwa kauli hii ya Mbowe Ina maana atagombea uenyekiti. Nadhani Mbowe anafikiri yeye tu ndio mwenye uwezo wa kuisimamisha CHADEMA. Wengine wataizamisha
Umeshaambiwa chama chake unauliza nini tena?
 
inasikitisha kwa kweli. Act wazalendo wajiandae kupata wabunge wawili watatu pahala pa chadema, chadema ndio basi tena kama mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti
Itafika mahala sisi wananchi tujipiganie bila kutegemea Wanasiasa!
 
ametoa kauli mbaya sana hivi ingetokea mwana ccm mstaafu atamke kuwa akiona chama chake kinazama ataingia mzigoni ataeleweka vipi? Huo ni uhaini
Sasa hivi watakaobaki na CHADEMA ni wale ambao wana Maslahi nayo, Sikiliza Speech ya Boniphace Jacob mbele ya Mbowe, Hapo ndipo utaona sura halisi ya CHADEMA, Kisha mtazame tena Kigaila!
 
Mwenyekiti anaye maliza muda wake, Freeman Mbowe amesema ya kwamba iwapo ataona chama chake Cha CHADEMA kinataka kuzamishwa basi ataingia mzigoni. Kwa maana nyingine atagombea uenyekiti wa CHADEMA. Je nani anataka kugombea uenyekiti akizamishe chama.

Kwa kauli hii ya Mbowe Ina maana atagombea uenyekiti. Nadhani Mbowe anafikiri yeye tu ndio mwenye uwezo wa kuisimamisha CHADEMA. Wengine wataizamisha
Kwa mawazo haya, Kenneth Kaunda, (Zambia ) Jomo Kenyatta (Kenya) Julius Nyerere (Tanzania), nk,, wangesema sisi ndio waasisi tumeleta uhuru hatutaki mwingine atuharibie nchi. Walikaa kando na nchi zao zinasonga. Pia anaharibu kusema chama chake kwani anatembeza nacho mfukoni kama leso au pochi ? Chama kinatakiwa kuwa cha wanachama.
 
Mbowe anatakiwa atumie tu busara amwachie Lissu uenyekiti na yeye awepo kwenye kamati kuu ili kama kutakuwa na namna ya mtu kukihujumu chama ashughulikiwe. Chama tunachokinadi kama cha demokrasia maana yake kila mtu ana nafasi sawa ya kushinda na kishindana kama vipi wote waombe na kuwe na free anda fair election atakayeshindwa basi aridhike ila siyo kuanza kumchafua Lissu kisa tu anagombea uenyekiti.
 
Back
Top Bottom