Nina stick hapo kwa wanachama wa Chadema vichwa ngumu sababu kuna mifano mingi wanayoonesha walivyo wagumu, wapo wanaopinga hata Mbowe kwenda ikulu juzi, walitaka asuse, hawa kwangu ni vichwa ngumu tu, hakuna politics bila mazungumzo.
Kuhusu idea ya Lissu kuongea na watz baada ya kuonana na Samia, na Mbowe kugoma kuongea mpaka wakae chamani kwao, kwangu naona hata Mbowe angeweza kufanya alichofanya Lissu tofauti na unavyofikiria.
Zaidi naona matukio ya Mbowe na Lissu kukutana na Samia yanafanana, labda ajenda moja tu ya Mbowe kuachiwa huru ndio inabadilika, nyingine zote zinabaki pale pale.
Mbowe angemaliza kuongea na Samia angeweza atoke pale aje aseme nimemwambia tunataka Katiba Mpya, Tume Huru, na mikutano ya siasa, lakini hakufanya hivyo, hii kwangu ni move tofauti kwenye same scenario kama ya Lissu.
Ila kama kuna motive behind iliyomfanya Lissu aongee vile na Samia aka react kwa kumuachia Mbowe na akawaudhi wahafidhina ndani ya chama chao hiyo siijui.