Mbowe: Ole Sabaya tumshamsamehe kabisa watu wa Hai. Maisha lazima yaendelee

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amemwombea msamaha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, akiwataka wananchi wa Hai kumsamehe huku akisisitiza kuwa hakuna binadamu asiye na dhambi.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Aprili 23, 2026, walipokutana katika mazishi ya mama wa Mbunge wa Jimbo la Hai (CCM), Saashisha Mafuwe, yaliyofanyika katika makaburi ya familia yaliyopo Kijiji cha Uduru, Kata ya Machame Kaskazini.

Mwaka 2021, Sabaya alishtakiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, utakatishaji fedha, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa pamoja na uhujumu uchumi, alipokuwa mkuu wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika mazishi hayo, Mbowe amesema:

"Nilipofika hapa nilimkuta Sabaya akizungumza. Sabaya ni mdogo wangu na rafiki yangu. Kama mnavyojua, misiba hutufanya tuwe wamoja, tunyenyekee na mara nyingine hujenga hata urafiki uliokuwa na mashaka.”

"Ndugu yangu Sabaya pole kwa kuwa sijakuona siku nyingi, nilipokuja hapa nilikuta unaelezea kidogo katika maeneo fulani... sasa na mimi vilevile ni Graduate (mhitimu) na mimi nimepitia hivyo hivyo kwa taratibu tofauti, sasa ndugu zangu mnaweza mkajiweka kwenye nafasi yangu, ninachojaribu kukifikisha kwenu ni kuwatia moyo familia na kuwaambia ndugu zangu, waombolezaji wote, kuna maisha nje ya siasa."

Mimi ni mwanaCCM ila Sabaya hapana. Mbowe hapa kateleza sana. Sabaya ana maovu mengi ambayo hayakufika kwenye media au mahakamani. Huyo kijana kavuruga sana maisha ya watu wengi wilayani Hai. Alikuwa mnyama. Msamaha ungekuwa halali kama angekuwa gerezani. Sabaya alikuwa mhalifu 100%.
 
Sabaya hawezi kuwa na maovu mengi kuliko samia
 
Mbowe kaenda kwenye msiba wa mtu aliyemuibia uchaguzi na kamuombea msamaha muovu Sabaya! Mbowe hakufaa kuwa kwenye siasa bali uchungaji au biashara zake, ameichelewesha sana CHADEMA.
Kabla ya Mbowe kushika uongozi Chadema ilikuwa wapi?

Mbowe ni mkristu na imani yake inamtaka amsamehe kila aliyemkosea. Lakini kusamehe sio kusahau. Na kusamehe kwake hakuna uzito wa kisheria au hata kisiasa. Ameongea msibani na sio kwenye mkutano wa chama.

Amandla...
 
20260418_112815.jpg
 
Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amemwombea msamaha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, akiwataka wananchi wa Hai kumsamehe huku akisisitiza kuwa hakuna binadamu asiye na dhambi.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Aprili 23, 2026, walipokutana katika mazishi ya mama wa Mbunge wa Jimbo la Hai (CCM), Saashisha Mafuwe, yaliyofanyika katika makaburi ya familia yaliyopo Kijiji cha Uduru, Kata ya Machame Kaskazini.

Mwaka 2021, Sabaya alishtakiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, utakatishaji fedha, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa pamoja na uhujumu uchumi, alipokuwa mkuu wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika mazishi hayo, Mbowe amesema:

"Nilipofika hapa nilimkuta Sabaya akizungumza. Sabaya ni mdogo wangu na rafiki yangu. Kama mnavyojua, misiba hutufanya tuwe wamoja, tunyenyekee na mara nyingine hujenga hata urafiki uliokuwa na mashaka.”

"Ndugu yangu Sabaya pole kwa kuwa sijakuona siku nyingi, nilipokuja hapa nilikuta unaelezea kidogo katika maeneo fulani... sasa na mimi vilevile ni Graduate (mhitimu) na mimi nimepitia hivyo hivyo kwa taratibu tofauti, sasa ndugu zangu mnaweza mkajiweka kwenye nafasi yangu, ninachojaribu kukifikisha kwenu ni kuwatia moyo familia na kuwaambia ndugu zangu, waombolezaji wote, kuna maisha nje ya siasa."

View attachment 3578224
 
Wakati mwingine kumsamehe aliyekuumiza kunamuumiza kuliko kulipa kisasi. Mbowe ametupa madongo mengi. Amedai haki. Amewaambia wenye madaraka wasijisahau. Amemtumia Sabaya kutoa ujumbe kuwa malipo ni hapa hapa duniani. Na amefanya yote hayo huku akitabasamu. Kisu kimeingia kuliko kama angemfokea au kumbeza.

Amandla...
 
Kabla ya Mbowe kushika uongozi Chadema ilikuwa wapi?

Mbowe ni mkristu na imani yake inamtaka amsamehe kila aliyemkosea. Lakini kusamehe sio kusahau. Na kusamehe kwake hakuna uzito wa kisheria au hata kisiasa. Ameongea msibani na sio kwenye mkutano wa chama.

Amandla...
Ndio maana nikasema hakufaa kuwa kiongozi wa CHADEMA, anafit zaidi kwenye dini au biashara kuliko siasa hasa za Tanzania chini ya CCM. Siasa za Tanzania zinawahitaji zaidi watu kama Lissu, Maalim Seif, Kambona n.k Appeasers kama Mbowe na Zitto wanachelewesha mabadiliko, kwa bahati mbaya hawa ndio wamekuwa wengi zaidi katika siasa za upinzani nchini.
 
Mbowe kaenda kwenye msiba wa mtu aliyemuibia uchaguzi na kamuombea msamaha muovu Sabaya! Mbowe hakufaa kuwa kwenye siasa bali uchungaji au biashara zake, ameichelewesha sana CHADEMA.
Kazi kweli kweli.
 
Ndio maana nikasema hakufaa kuwa kiongozi wa CHADEMA, anafit zaidi kwenye dini au biashara kuliko siasa hasa za Tanzania chini ya CCM. Siasa za Tanzania zinawahitaji zaidi watu kama Lissu, Maalim Seif, Kambona n.k Appeasers kama Mbowe na Zitto wanachelewesha mabadiliko, kwa bahati mbaya Hawa ndio wamekuwa wengi zaidi.
Hapana. Mbowe ni mwanasiasa bora kuliko Lissu. Lissu anaangalia short term goals. Ni mtu ambae ana ongozwa na emotions wakati Mbowe ni strategic na cold blooded. Lissu angeshika madaraka badala ya Mbowe, Chadema ingeishia kuwa kama DP ya marehemu Mtikila. Watu mnataka kutuaminisha kuwa CCM na serikali yake ziliikumbatia Chadema ya Mbowe wakati ukweli ni kuwa Chadema ya Mbowe ilishughulikiwa kuliko chama kingine chochote cha siasa by far. Viongozi wake ( wakiwemo Lissu na Heche) walipitia moto mkali lakini kiongozi wao hakuteteleka. Mnasahau reaction yake Lissu alipopigwa risasi? Walipofungwa Heche alisema kuwa alikataa kutoka jela mpaka baada ya wenzake wote kutoka. Sasa tuangalie hali ilivyo wakati wa Lissu. Ni Lissu peke yake aliyeko ndani. Wengine wote ( wakina Rupia n.k.) wanaishia mahabusu halafu wanaachiwa. Hivi toka wameruhusiwa kufanya siasa ni kitu gani cha maana zaidi ya kufanya presa? Wamefanya mikutano ya hadhara mingapi? Wametangaza maandamano mangapi?

Ni viongozi wachache sana wa Chadema, Bawacha na Bavicha tunaowasikia wakipinga yanayoendelea wakiwa ndani ya nchi ukilinganisha na wakati wa Mbowe. Wakati ule wakina Ruge, Husna, Kiwanga, Mnyika, Heche, Halima, yule kijana wa Iringa, Rose Mayemba ( mahabusu kulikuwa kwake) n.k. walikuwa hawapoi. Rose Mayemba wa sasa sio wa wakati wa Mbowe.

Yote hayo lakini bado mnadiriki kusema Mbowe akiwachelewesha?

Amandla...
 
Baada ya ukimya mwingi sana...... hatimaye amesema neno leo, lakini hii inaonyesha pia kwa ukimua huo kwa mwenyekiti aliye mshinda (Lisu)..... nikama bado anakinyongo na kitendo cha kushindwa.
Hatuwezi kiwasamehe watu wote walioanzisha utekaji, uuaji na unyang'anyi. Miingoni mwao ni Makonda na Ole Sabaya. Hapa Mbowe au hayuko serious au ameongea kwa tafsida (satire)
 
Sabaya hayuko jela na Bashite ni Waziri katika wizara muhimu kwenye serikali ya mama yenu, msamaha gani zaidi ya huu wanaohitaji??
 
Hapana. Mbowe ni mwanasiasa bora kuliko Lissu. Lissu anaangalia short term goals. Ni mtu ambae ana ongozwa na emotions wakati Mbowe ni strategic na cold blooded. Lissu angeshika madaraka badala ya Mbowe, Chadema ingeishia kuwa kama DP ya marehemu Mtikila. Watu mnataka kutuaminisha kuwa CCM na serikali yake ziliikumbatia Chadema ya Mbowe wakati ukweli ni kuwa Chadema ya Mbowe ilishughulikiwa kuliko chama kingine chochote cha siasa by far. Viongozi wake ( wakiwemo Lissu na Heche) walipitia moto mkali lakini kiongozi wao hakuteteleka. Mnasahau reaction yake Lissu alipopigwa risasi? Walipofungwa Heche alisema kuwa alikataa kutoka jela mpaka baada ya wenzake wote kutoka. Sasa tuangalie hali ilivyo wakati wa Lissu. Ni Lissu peke yake aliyeko ndani. Wengine wote ( wakina Rupia n.k.) wanaishia mahabusu halafu wanaachiwa. Hivi toka wameruhusiwa kufanya siasa ni kitu gani cha maana zaidi ya kufanya presa? Wamefanya mikutano ya hadhara mingapi? Wametangaza maandamano mangapi?

Ni viongozi wachache sana wa Chadema, Bawacha na Bavicha tunaowasikia wakipinga yanayoendelea wakiwa ndani ya nchi ukilinganisha na wakati wa Mbowe. Wakati ule wakina Ruge, Husna, Kiwanga, Mnyika, Heche, Halima, yule kijana wa Iringa, Rose Mayemba ( mahabusu kulikuwa kwake) n.k. walikuwa hawapoi. Rose Mayemba wa sasa sio wa wakati wa Mbowe.

Yote hayo lakini bado mnadiriki kusema Mbowe akiwachelewesha?

Amandla...
Cheki hii tikiti Chadema Toka waachiwe huru na mahakama ata two weeks hawana ushauliza mikutano mingapi nyie ambao hamkufungiwa mmepiga mikutano mingapi😁
 
Hapana. Mbowe ni mwanasiasa bora kuliko Lissu. Lissu anaangalia short term goals. Ni mtu ambae ana ongozwa na emotions wakati Mbowe ni strategic na cold blooded. Lissu angeshika madaraka badala ya Mbowe, Chadema ingeishia kuwa kama DP ya marehemu Mtikila. Watu mnataka kutuaminisha kuwa CCM na serikali yake ziliikumbatia Chadema ya Mbowe wakati ukweli ni kuwa Chadema ya Mbowe ilishughulikiwa kuliko chama kingine chochote cha siasa by far. Viongozi wake ( wakiwemo Lissu na Heche) walipitia moto mkali lakini kiongozi wao hakuteteleka. Mnasahau reaction yake Lissu alipopigwa risasi? Walipofungwa Heche alisema kuwa alikataa kutoka jela mpaka baada ya wenzake wote kutoka. Sasa tuangalie hali ilivyo wakati wa Lissu. Ni Lissu peke yake aliyeko ndani. Wengine wote ( wakina Rupia n.k.) wanaishia mahabusu halafu wanaachiwa. Hivi toka wameruhusiwa kufanya siasa ni kitu gani cha maana zaidi ya kufanya presa? Wamefanya mikutano ya hadhara mingapi? Wametangaza maandamano mangapi?

Ni viongozi wachache sana wa Chadema, Bawacha na Bavicha tunaowasikia wakipinga yanayoendelea wakiwa ndani ya nchi ukilinganisha na wakati wa Mbowe. Wakati ule wakina Ruge, Husna, Kiwanga, Mnyika, Heche, Halima, yule kijana wa Iringa, Rose Mayemba ( mahabusu kulikuwa kwake) n.k. walikuwa hawapoi. Rose Mayemba wa sasa sio wa wakati wa Mbowe.

Yote hayo lakini bado mnadiriki kusema Mbowe akiwachelewesha?

Amandla...
Viongozi wengi wa zamani wa CHADEMA ya Mbowe sasa hivi wako CCM au CHAUMA, Tumaini Makene na John Mrema waliuza akaunti zote za mitandao ya kijamii ya CHADEMA, pia Mbowe alisema mambo mengi ya CHADEMA alikuwa akiyafanikisha kwa pesa zake na 'marafiki zake', itachukua muda CHADEMA kujijenga kama taasisi inayotegemea wanachama zaidi katika baadhi ya mambo.
 
Back
Top Bottom