Mbowe: Ole Sabaya tumshamsamehe kabisa watu wa Hai. Maisha lazima yaendelee

Mimi ni mwanaCCM ila Sabaya hapana. Mbowe hapa kateleza sana. Sabaya ana maovu mengi ambayo hayakufika kwenye media au mahakamani. Huyo kijana kavuruga sana maisha ya watu wengi wilayani Hai. Alikuwa mnyama. Msamaha ungekuwa halali kama angekuwa gerezani. Sabaya alikuwa mhalifu 100%.
Sabaya ana tofauti gani na Makonda?
 
Hapana. Mbowe ni mwanasiasa bora kuliko Lissu. Lissu anaangalia short term goals. Ni mtu ambae ana ongozwa na emotions wakati Mbowe ni strategic na cold blooded. Lissu angeshika madaraka badala ya Mbowe, Chadema ingeishia kuwa kama DP ya marehemu Mtikila. Watu mnataka kutuaminisha kuwa CCM na serikali yake ziliikumbatia Chadema ya Mbowe wakati ukweli ni kuwa Chadema ya Mbowe ilishughulikiwa kuliko chama kingine chochote cha siasa by far. Viongozi wake ( wakiwemo Lissu na Heche) walipitia moto mkali lakini kiongozi wao hakuteteleka. Mnasahau reaction yake Lissu alipopigwa risasi? Walipofungwa Heche alisema kuwa alikataa kutoka jela mpaka baada ya wenzake wote kutoka. Sasa tuangalie hali ilivyo wakati wa Lissu. Ni Lissu peke yake aliyeko ndani. Wengine wote ( wakina Rupia n.k.) wanaishia mahabusu halafu wanaachiwa. Hivi toka wameruhusiwa kufanya siasa ni kitu gani cha maana zaidi ya kufanya presa? Wamefanya mikutano ya hadhara mingapi? Wametangaza maandamano mangapi?

Ni viongozi wachache sana wa Chadema, Bawacha na Bavicha tunaowasikia wakipinga yanayoendelea wakiwa ndani ya nchi ukilinganisha na wakati wa Mbowe. Wakati ule wakina Ruge, Husna, Kiwanga, Mnyika, Heche, Halima, yule kijana wa Iringa, Rose Mayemba ( mahabusu kulikuwa kwake) n.k. walikuwa hawapoi. Rose Mayemba wa sasa sio wa wakati wa Mbowe.

Yote hayo lakini bado mnadiriki kusema Mbowe akiwachelewesha?

Amandla...
Sikubaliani na wewe unaposema Lissu anaangalia short term goals.Either huwa haumusikilizi Lissu,au huwa unachagua kusikiliza yanayokufurahisha tu
 
Hiyo unayoona ni nguvu ya Mbowe ndio ulipokuwa udhaifu wa cdm. Kiongozi aliyejiugeuza kuwa ndio taasisi huoni tatizo. Hao unaowataja walifanya maandamano na mikutano chama kikiwa kimezuiwa kufanya siasa? Au walikuwa wanafanya mikutano na maandamano kila baada ya wiki 2?

Chama ndio kimefunguliwa kufanya siasa wiki 1 iliyopita, hata ofisi hawajafanya usafi na kujipanga waingie vipi kwa umma, unasema wamefanya maandamano mara ngapi?! Yaani Mbowe aliyekaa miaka 20+, unatolea mfano na uongozi uliokaa miezi minne na chama kikazuiwa kufanya siasa, tena kwa hila za huyo huyo Mbowe kwenye project yake ya kuikwamisha cdm?
 
Mimi ni mwanaCCM ila Sabaya hapana. Mbowe hapa kateleza sana. Sabaya ana maovu mengi ambayo hayakufika kwenye media au mahakamani. Huyo kijana kavuruga sana maisha ya watu wengi wilayani Hai. Alikuwa mnyama. Msamaha ungekuwa halali kama angekuwa gerezani. Sabaya alikuwa mhalifu 100%.
Hajamsamehe bali ametoa lugha za kisiasa. Amesema hivyo ili aonekane ni mwanasiasa mvumilivu, lakini ukweli hata asingemsamehe hana cha kumfanya. Ilitakiwa awe na madaraka tupime msamaha wake.

Huyo kashindwa na Lisu juzi kasusa hadi leo, na kibaya zaidi team yake ikahama chama tena kwa lengo la kumaliza cdm.
 
Mbowe aliichelewesha chadema kufikia malengo! Safu yake ya takataka kama Yericko Nyerere ulikuwa ni uchafu ulijificha kwenye kivuli cha upinzani kumbe ni njaa ya pesa
Sijui kama umeelewa Mbowe alivyosema "kuna maisha nje ya siasa"

Kuna wakati naona kabisa mindset zenu ndio zinarudisha nyuma harakati za mageuzi ya kisiasa nchi hii. Mpo kama mawe hayasogei mpaka yapigwe teke.

Mnamtaka Mbowe atengeneze uadui na Sabaya milele!! Ili iweje, itasaidia nini zaidi ya kuifanya Chadema ionekane chama cha wajuaji?

Kuna wakati inalazimu kuiweka mihemko ya kisiasa pembeni, maisha mengine lazima yaendelee.
 
Viongozi wengi wa zamani wa CHADEMA ya Mbowe sasa hivi wako CCM au CHAUMA,
NI haki yao. Na hawakuanza kuhama leo.

Tumaini Makene na John Mrema waliuza akaunti zote za mitandao ya kijamii ya CHADEMA,
Ongea kama msomi. Angemuuzia nani hizo akaunti? Wao waliondoka lakini walioingia hawakuwa na passwords za ku access zile akaunti. Lakini kwa namna walivyomfanyia Mrema walishindwa kumuomba.
pia Mbowe alisema mambo mengi ya CHADEMA alikuwa akiyafanikisha kwa pesa zake na 'marafiki zake',
Kwani uongo? Hata Mkutano Mkuu wa mwaka jana bila milioni 250 alizotoa usingefanyika. Haya aliyasema Katibu Mkuu wa Chadema.
itachukua muda CHADEMA kujijenga kama taasisi inayotegemea wanachama zaidi katika baadhi ya mambo.
Sio uongo. Ndio maana Chadema ya sasa inapata shida kutoa taarifa za mapato na matumizi kama walivyo ahidi. Watanzania ni wachangaji wazuri wa tukio lakini sio kwenye mambo endelevu. Bahati mbaya hata uongozi wa sasa wanapenda mambo ya kifahari. Wote wanapenda ma Vieti. Tofauti ni kuwa Mbowe alikuwa ananunua mnadani, wao tutaona wananunua wapi.

Amandla...
 
Sikubaliani na wewe unaposema Lissu anaangalia short term goals.Either huwa haumusikilizi Lissu,au huwa unachagua kusikiliza yanayokufurahisha tu
Namsikiliza sana. Mtu yeyote mwenye kufikiri alijua hamna jinsi CCM wangekubali kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya kabla ya Uchaguzi. Na wasingekubali kuahirisha uchaguzi. Angekuwa mwenye mtazamo wa mbali ange focus kwenye uchaguzi wa 2030 na kujipanga kuhakikisha kuwa Katiba Mpya na mfumo mzima wa uchaguzi unafumuliwa kabla ya 2028. Njia ya kufanya hivyo ni kuingiza wabunge wake bungeni na kupata ruzuku ya kutosha kupiga kampeni nchi nzima. Wale walioenda Chaumma walitambua hilo lakini Lissu ali focus kwenye 2025. Na matokeo yake tumeyaona.

Amandla...
 
Baada madawa ya kulevya na upiga dili kurudi tena kwa kasi Hai ndiyo mnamsamehe?
 
Viongozi wengi wa zamani wa CHADEMA ya Mbowe sasa hivi wako CCM au CHAUMA, Tumaini Makene na John Mrema waliuza akaunti zote za mitandao ya kijamii ya CHADEMA, pia Mbowe alisema mambo mengi ya CHADEMA alikuwa akiyafanikisha kwa pesa zake na 'marafiki zake', itachukua muda CHADEMA kujijenga kama taasisi inayotegemea wanachama zaidi katika baadhi ya mambo.
Changia ToneTone japo kwa Tsh 2,000 siyo kulialia humu tu
 
Namsikiliza sana. Mtu yeyote mwenye kufikiri alijua hamna jinsi CCM wangekubali kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya kabla ya Uchaguzi. Na wasingekubali kuahirisha uchaguzi. Angekuwa mwenye mtazamo wa mbali ange focus kwenye uchaguzi wa 2030 na kujipanga kuhakikisha kuwa Katiba Mpya na mfumo mzima wa uchaguzi unafumuliwa kabla ya 2028. Njia ya kufanya hivyo ni kuingiza wabunge wake bungeni na kupata ruzuku ya kutosha kupiga kampeni nchi nzima. Wale walioenda Chaumma walitambua hilo lakini Lissu ali focus kwenye 2025. Na matokeo yake tumeyaona.

Amandla...
Chaumma na ACT ya Luhaga Mpina wamepata wabunge wangapi kwa kushiriki uchaguzi mkuu??

CHADEMA iliposhirikia uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 ilipata matokeo gani??

Kama CCM hawakutaka na hawakuleta katiba mpya kabla ya 2025 ni kinakufanya uamink wataleta katiba mpya au tume huru ya uchaguzi kabla ya 2030?
 
Chadema ilipata mbunge mmoja katika uchaguzi wa 2020. Huyo mmoja tu alilisumbua sana bunge la CCM. Kura walizopata katika uchaguzi ule (ingawa walipunjwa) ziliwapa ruzuku ambayo baada ya kukubali kuipokea iliwawezesha kununua jengo walilofanya Makao Makuu yao, kukarabati makao yao ya zamani na kuendesha shughuli za chama chao.

Chaumma na Act ya Semu zina wabunge na zinapata ruzuku ambazo wanatumia kujitayarisha kwa ajili ya chaguzi za 2029 na 2030. Sigrada kila kukicha yuko jimboni mwake akipigania watu wake. Na akitoka kule anaendeleza mapambano Bungeni. Ado Shaibu hivyo hivyo. Wakati huo Chadema platform waliyokuwa nayo ni presa. Wanashindwa hata kufanya sherehe zao

CCM wataleta Katiba Mpya kabla ya 2028 kama ambavyo walileta Tume Huru ya Uchaguzi. Kazi kubwa inayovikabili vyama vya upinzani ni kuishinikiza CCM wapitishe Katiba Mpya kweli na sio ya kiini macho kama walivyofanya kwenye Tume ya Uchaguzi. Ili kufanikisha hilo wanahitaji kuwa kila mahali (bungeni, miatandaoni na kwenye vitongoji) na kushirikiana kama walivyofanya wakati wa Ukawa. Shida ni kuwa ni wachache sana watakuwa tayari kushirikiana na Chadema ya sasa ambayo imetukana karibu vyama vingine vyote vya upinzani.

Akili yako imeharibiwa na siasa za kupenda na kufikiria ruzuku tu, kila ukiongea ni ruzuku tu, CHADEMA wala haina hata shida ya ruzuku bali uwanja sawa na uhuru wa kufanya siasa.

Mbunge mmoja wa CHADEMA waliyepewa na Magufuli 2020 wala hakuwa na chochote cha maana bungeni, 90% ya raia hata hawakuwa wanajua kama CHADEMA wana mbunge bungeni zaidi ya wale COVID-19 waliokuwa kwenye mgogoro nao.
 
Hapana. Mbowe ni mwanasiasa bora kuliko Lissu. Lissu anaangalia short term goals. Ni mtu ambae ana ongozwa na emotions wakati Mbowe ni strategic na cold blooded. Lissu angeshika madaraka badala ya Mbowe, Chadema ingeishia kuwa kama DP ya marehemu Mtikila. Watu mnataka kutuaminisha kuwa CCM na serikali yake ziliikumbatia Chadema ya Mbowe wakati ukweli ni kuwa Chadema ya Mbowe ilishughulikiwa kuliko chama kingine chochote cha siasa by far. Viongozi wake ( wakiwemo Lissu na Heche) walipitia moto mkali lakini kiongozi wao hakuteteleka. Mnasahau reaction yake Lissu alipopigwa risasi? Walipofungwa Heche alisema kuwa alikataa kutoka jela mpaka baada ya wenzake wote kutoka. Sasa tuangalie hali ilivyo wakati wa Lissu. Ni Lissu peke yake aliyeko ndani. Wengine wote ( wakina Rupia n.k.) wanaishia mahabusu halafu wanaachiwa. Hivi toka wameruhusiwa kufanya siasa ni kitu gani cha maana zaidi ya kufanya presa? Wamefanya mikutano ya hadhara mingapi? Wametangaza maandamano mangapi?

Ni viongozi wachache sana wa Chadema, Bawacha na Bavicha tunaowasikia wakipinga yanayoendelea wakiwa ndani ya nchi ukilinganisha na wakati wa Mbowe. Wakati ule wakina Ruge, Husna, Kiwanga, Mnyika, Heche, Halima, yule kijana wa Iringa, Rose Mayemba ( mahabusu kulikuwa kwake) n.k. walikuwa hawapoi. Rose Mayemba wa sasa sio wa wakati wa Mbowe.

Yote hayo lakini bado mnadiriki kusema Mbowe akiwachelewesha?

Amandla...

Lissu ni Mwanasiasa asiyeyumba. Mwenye Misimamo na Kujielewa. Mbowe anaangalia kwenye siasa anafaidika vipi na nini pia.
 
Tanzania kuna Tume huru ya uchaguzi?!
Inawezekana hii ni ID nyingine ya Yericko.
 
Akili yako imeharibiwa na siasa za kupenda na kufikiria ruzuku tu, kila ukiongea ni ruzuku tu, CHADEMA wala haina hata shida ya ruzuku bali uwanja sawa na uhuru wa kufanya siasa.

Mbunge mmoja wa CHADEMA waliyepewa na Magufuli 2020 wala hakuwa na chochote cha maana bungeni, 90% ya raia hata hawakuwa wanajua kama CHADEMA wana mbunge bungeni zaidi ya wale COVID-19 waliokuwa kwenye mgogoro nao.
Chama chochote cha siasa kinahitaji fedha ili kuweza kuendesha shughuli zake. Ruzuku ni sehemu ya hizo pesa. Kwa vile Chadema haitakuwa na ruzuku kwa miaka mitano ijayo ni nafasi nzuri kuionyesha jamii namna watakavyoongoza juhudi za kupata huo uwanja sawa na uhuru wa kufanya siasa katika hali waliyokuwa nayo. 2029 sio mbali.

Ndivyo alivyosema Lissu akisahau kuwa yule mbunge mmoja alikihakikishia Chadema ushindi na kura za kutosha katika jimbo lake la uchaguzi. Kuthibitisha hilo, mbunge aliyemrithi wa jimbo hilo anatoka upinzani. Sio lazima utambuliwe na 90% ili uwe na impact. Aidan alikuwa na impact kuliko wabunge wengi wa CCM.

Amandla...
 
Lissu ni Mwanasiasa asiyeyumba. Mwenye Misimamo na Kujielewa. Mbowe anaangalia kwenye siasa anafaidika vipi na nini pia.
Tutaona. Hivi majuzi tunasikia amekubali kuingia katika mazungumzo ya Maridhiano. Hivi karibuni tumemsikia Makamu wake akimmwagia sifa kiongozi wa Covid-19 waliyekuwa wakimuita msaliti. Sijui mtasema nini mtakapo muona amekaa Ikulu akinywa kahawa na Mkuu wa nchi. Yetu macho.

Amandla....
 
Sijui kama umeelewa Mbowe alivyosema "kuna maisha nje ya siasa"

Kuna wakati naona kabisa mindset zenu ndio zinarudisha nyuma harakati za mageuzi ya kisiasa nchi hii. Mpo kama mawe hayasogei mpaka yapigwe teke.

Mnamtaka Mbowe atengeneze uadui na Sabaya milele!! Ili iweje, itasaidia nini zaidi ya kuifanya Chadema ionekane chama cha wajuaji?

Kuna wakati inalazimu kuiweka mihemko ya kisiasa pembeni, maisha mengine lazima yaendelee.
Nimwsema ya Yeriko Nyerere. Not. Ya Sabaya...nimechomekea tu
 
Hapana. Mbowe ni mwanasiasa bora kuliko Lissu. Lissu anaangalia short term goals. Ni mtu ambae ana ongozwa na emotions wakati Mbowe ni strategic na cold blooded. Lissu angeshika madaraka badala ya Mbowe, Chadema ingeishia kuwa kama DP ya marehemu Mtikila. Watu mnataka kutuaminisha kuwa CCM na serikali yake ziliikumbatia Chadema ya Mbowe wakati ukweli ni kuwa Chadema ya Mbowe ilishughulikiwa kuliko chama kingine chochote cha siasa by far. Viongozi wake ( wakiwemo Lissu na Heche) walipitia moto mkali lakini kiongozi wao hakuteteleka. Mnasahau reaction yake Lissu alipopigwa risasi? Walipofungwa Heche alisema kuwa alikataa kutoka jela mpaka baada ya wenzake wote kutoka. Sasa tuangalie hali ilivyo wakati wa Lissu. Ni Lissu peke yake aliyeko ndani. Wengine wote ( wakina Rupia n.k.) wanaishia mahabusu halafu wanaachiwa. Hivi toka wameruhusiwa kufanya siasa ni kitu gani cha maana zaidi ya kufanya presa? Wamefanya mikutano ya hadhara mingapi? Wametangaza maandamano mangapi?

Ni viongozi wachache sana wa Chadema, Bawacha na Bavicha tunaowasikia wakipinga yanayoendelea wakiwa ndani ya nchi ukilinganisha na wakati wa Mbowe. Wakati ule wakina Ruge, Husna, Kiwanga, Mnyika, Heche, Halima, yule kijana wa Iringa, Rose Mayemba ( mahabusu kulikuwa kwake) n.k. walikuwa hawapoi. Rose Mayemba wa sasa sio wa wakati wa Mbowe.

Yote hayo lakini bado mnadiriki kusema Mbowe akiwachelewesha?

Amandla...
Upumbavu mtupu!
FB_IMG_1748360197313.jpg
 
Back
Top Bottom