Mbowe: Ole Sabaya tumshamsamehe kabisa watu wa Hai. Maisha lazima yaendelee

Mbowe: Ole Sabaya tumshamsamehe kabisa watu wa Hai. Maisha lazima yaendelee

Nenda kawaulize wao.
FB_IMG_1748360197313.jpg
 
Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amemwombea msamaha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, akiwataka wananchi wa Hai kumsamehe huku akisisitiza kuwa hakuna binadamu asiye na dhambi.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Aprili 23, 2026, walipokutana katika mazishi ya mama wa Mbunge wa Jimbo la Hai (CCM), Saashisha Mafuwe, yaliyofanyika katika makaburi ya familia yaliyopo Kijiji cha Uduru, Kata ya Machame Kaskazini.

Mwaka 2021, Sabaya alishtakiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, utakatishaji fedha, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa pamoja na uhujumu uchumi, alipokuwa mkuu wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika mazishi hayo, Mbowe amesema:

"Nilipofika hapa nilimkuta Sabaya akizungumza. Sabaya ni mdogo wangu na rafiki yangu. Kama mnavyojua, misiba hutufanya tuwe wamoja, tunyenyekee na mara nyingine hujenga hata urafiki uliokuwa na mashaka.”

"Ndugu yangu Sabaya pole kwa kuwa sijakuona siku nyingi, nilipokuja hapa nilikuta unaelezea kidogo katika maeneo fulani... sasa na mimi vilevile ni Graduate (mhitimu) na mimi nimepitia hivyo hivyo kwa taratibu tofauti, sasa ndugu zangu mnaweza mkajiweka kwenye nafasi yangu, ninachojaribu kukifikisha kwenu ni kuwatia moyo familia na kuwaambia ndugu zangu, waombolezaji wote, kuna maisha nje ya siasa."


View attachment 3578224
Hizi njia za mkato, tena nje ya taratibu za uwajibikaji ndizo zinazoendelea kuvuruga taifa hili.

Mnafanya maovu yenu huko gizani; mnakuja huku kwenye mwanga na kutufanya wajinga?
 
Tutaona. Hivi majuzi tunasikia amekubali kuingia katika mazungumzo ya Maridhiano. Hivi karibuni tumemsikia Makamu wake akimmwagia sifa kiongozi wa Covid-19 waliyekuwa wakimuita msaliti. Sijui mtasema nini mtakapo muona amekaa Ikulu akinywa kahawa na Mkuu wa nchi. Yetu macho.

Amandla....

Weeeh... Hebu tuwekee audio/video au maandishi aliyosema hayo...
 
Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amemwombea msamaha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, akiwataka wananchi wa Hai kumsamehe huku akisisitiza kuwa hakuna binadamu asiye na dhambi.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Aprili 23, 2026, walipokutana katika mazishi ya mama wa Mbunge wa Jimbo la Hai (CCM), Saashisha Mafuwe, yaliyofanyika katika makaburi ya familia yaliyopo Kijiji cha Uduru, Kata ya Machame Kaskazini.

Mwaka 2021, Sabaya alishtakiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, utakatishaji fedha, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa pamoja na uhujumu uchumi, alipokuwa mkuu wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika mazishi hayo, Mbowe amesema:

"Nilipofika hapa nilimkuta Sabaya akizungumza. Sabaya ni mdogo wangu na rafiki yangu. Kama mnavyojua, misiba hutufanya tuwe wamoja, tunyenyekee na mara nyingine hujenga hata urafiki uliokuwa na mashaka.”

"Ndugu yangu Sabaya pole kwa kuwa sijakuona siku nyingi, nilipokuja hapa nilikuta unaelezea kidogo katika maeneo fulani... sasa na mimi vilevile ni Graduate (mhitimu) na mimi nimepitia hivyo hivyo kwa taratibu tofauti, sasa ndugu zangu mnaweza mkajiweka kwenye nafasi yangu, ninachojaribu kukifikisha kwenu ni kuwatia moyo familia na kuwaambia ndugu zangu, waombolezaji wote, kuna maisha nje ya siasa."


View attachment 3578224
Mbowe ni wa ovyo, Sabaya ameua watu wengi, ameteka watu wasio na makosa ila kwa kuwa tu na itikadi tofauti na CCM, amefunga watu wasio na makosa. Raia wa Tanzania wana haki ya kufanya siasa kwa mujibu wa katiba, Huyu Mbowe ni mpumbavu, na kwa vile anapewa pesa na kitambi Samia analazimishwa awapende CCM na awachukie CHADEMA waliomshinda uongozi. Suala la kusamehewa Sabaya halikubaliki, Sabaya amesababisha familia zipoteze wapendwa wao, na ni makosa makubwa aliyoyafanya ambayo hayakubaliki, hao aliowapoteza atuambie wapi walipo au aonyeshe mahali alipowazika......Sabaya anapaswa awe jela maisha kwa mauaji. MBOWE ACHA KUHARIBU, MBONA HUMTETEI LISSU ASIYE NA KOSA, UNAWATETEA WALE WA UPANDE MWINGINE?
 
Nakuongeza kwenye ignore list yangu,

Amandla...
Wewe ndiye unayetakiwa kuwekwa kwenye hiyo list kwa sababu ya upumbavu wako. Mbowe yule ni mpiga deal na kwenye siasa alikuwa anatutapeli tu. Katika mambo ya hatari kwenye nchi ni kusamehe wahalifu kama Sabaya wakati walifanya uovu na mauaji. Anajitia kimbelembele, Sabaya kaomba msamaha? Sabaya aliwahi kuomba msamaha kwa watu aliowaumiza? Huyu jamaa yenu Mbowe sikuwahi kudahni ni mjinga kiasi hiki.
 
Hapana. Mbowe ni mwanasiasa bora kuliko Lissu. Lissu anaangalia short term goals. Ni mtu ambae ana ongozwa na emotions wakati Mbowe ni strategic na cold blooded. Lissu angeshika madaraka badala ya Mbowe, Chadema ingeishia kuwa kama DP ya marehemu Mtikila. Watu mnataka kutuaminisha kuwa CCM na serikali yake ziliikumbatia Chadema ya Mbowe wakati ukweli ni kuwa Chadema ya Mbowe ilishughulikiwa kuliko chama kingine chochote cha siasa by far. Viongozi wake ( wakiwemo Lissu na Heche) walipitia moto mkali lakini kiongozi wao hakuteteleka. Mnasahau reaction yake Lissu alipopigwa risasi? Walipofungwa Heche alisema kuwa alikataa kutoka jela mpaka baada ya wenzake wote kutoka. Sasa tuangalie hali ilivyo wakati wa Lissu. Ni Lissu peke yake aliyeko ndani. Wengine wote ( wakina Rupia n.k.) wanaishia mahabusu halafu wanaachiwa. Hivi toka wameruhusiwa kufanya siasa ni kitu gani cha maana zaidi ya kufanya presa? Wamefanya mikutano ya hadhara mingapi? Wametangaza maandamano mangapi?

Ni viongozi wachache sana wa Chadema, Bawacha na Bavicha tunaowasikia wakipinga yanayoendelea wakiwa ndani ya nchi ukilinganisha na wakati wa Mbowe. Wakati ule wakina Ruge, Husna, Kiwanga, Mnyika, Heche, Halima, yule kijana wa Iringa, Rose Mayemba ( mahabusu kulikuwa kwake) n.k. walikuwa hawapoi. Rose Mayemba wa sasa sio wa wakati wa Mbowe.

Yote hayo lakini bado mnadiriki kusema Mbowe akiwachelewesha?

Amandla...
Mwamba umetengeneza hoja nzuri sana
 
Ndio maana nikasema hakufaa kuwa kiongozi wa CHADEMA, anafit zaidi kwenye dini au biashara kuliko siasa hasa za Tanzania chini ya CCM. Siasa za Tanzania zinawahitaji zaidi watu kama Lissu, Maalim Seif, Kambona n.k Appeasers kama Mbowe na Zitto wanachelewesha mabadiliko, kwa bahati mbaya hawa ndio wamekuwa wengi zaidi katika siasa za upinzani nchini.

Mkuu Mbowe Alifaa kwa wakati wake, na TAL Anafaa kwa wakati wake wa sasa.
 
Hajamsamehe bali ametoa lugha za kisiasa. Amesema hivyo ili aonekane ni mwanasiasa mvumilivu, lakini ukweli hata asingemsamehe hana cha kumfanya. Ilitakiwa awe na madaraka tupime msamaha wake.

Huyo kashindwa na Lisu juzi kasusa hadi leo, na kibaya zaidi team yake ikahama chama tena kwa lengo la kumaliza cdm.
.

Anataka tumuone kama Mandela, sisi sio wajinga bhana
 
Mbowe ni wa ovyo, Sabaya ameua watu wengi, ameteka watu wasio na makosa ila kwa kuwa tu na itikadi tofauti na CCM, amefunga watu wasio na makosa. Raia wa Tanzania wana haki ya kufanya siasa kwa mujibu wa katiba, Huyu Mbowe ni mpumbavu, na kwa vile anapewa pesa na kitambi Samia analazimishwa awapende CCM na awachukie CHADEMA waliomshinda uongozi. Suala la kusamehewa Sabaya halikubaliki, Sabaya amesababisha familia zipoteze wapendwa wao, na ni makosa makubwa aliyoyafanya ambayo hayakubaliki, hao aliowapoteza atuambie wapi walipo au aonyeshe mahali alipowazika......Sabaya anapaswa awe jela maisha kwa mauaji. MBOWE ACHA KUHARIBU, MBONA HUMTETEI LISSU ASIYE NA KOSA, UNAWATETEA WALE WA UPANDE MWINGINE?

Mbaya zaidi mwenyewe sabaya hajaomba msamaha na kukiri kuna watu amewaumiza, Analazimisha uma umuone kama amebadirika.

Yaani umebadirika wakati huna madaraka, Sisis ni wanjinga au?

Eti hata tembea yangu imebadirka 🤣
 
Mkuu Mbowe Alifaa kwa wakati wake, na TAL Anafaa kwa wakati wake wa sasa.
Mbowe ni mtu soft, anayependa dini zaidi na kulinda maslahi yake ya biashara na ukaribu na watawala (huenda labda kwa sababu ya historia yake, baba yake kuwa rafiki wa Nyerere na serikali na baba mkwe wake kuwa gavana wa BoT vimechangia).Hii hulka yake ni wazi imeleta mgogoro wa maslahi katika harakati zake za siasa. Aliziweza siasa vizuri wakati wa JK kwa sababu JK alikuwa akipenda zaidi siasa za hadaa za kuwapanga watu kwa mazungumzo kuliko nguvu, ilitakiwa amuachie Lissu uongozi mara tu baada ya uchaguzi wa 2015.
 
Hawa CCM wa mama wanaojidai ni nyutro wanakera sana.
Eti yule mama fisadi anateuliwa kuwa mshauri wake alafu hawa machawa wanapata nguvu gani ya kumtetea huyu mama, hakuna kazi ngumu kama kumtetea huyu mama
 
Mbowe ni mtu soft, anayependa dini zaidi na kulinda maslahi yake ya biashara na ukaribu na watawala (huenda labda kwa sababu ya historia yake, baba yake kuwa rafiki wa Nyerere na serikali na baba mkwe wake kuwa gavana wa BoT vimechangia).Hii hulka yake ni wazi imeleta mgogoro wa maslahi katika harakati zake za siasa. Aliziweza siasa vizuri wakati wa JK kwa sababu JK alikuwa akipenda zaidi siasa za hadaa za kuwapanga watu kwa mazungumzo kuliko nguvu, ilitakiwa amuachie Lissu uongozi mara tu baada ya uchaguzi wa 2015.
Mbowe ni kiongozi mzuri mwenye vision na mipango kuliko Lissu Hilo liko wazi sema kwa aina ya siasa za sasa hivi zinamuhitaji Lissu kuliko Mbowe ndio sababu wanachama wakamchagua Lissu kuwa mwenyekiti wao
 
Back
Top Bottom