Mbowe: Rais, wanaopinga ushiriki wa Taifa kwenye vita ya Corona wanawaza uchaguzi na huruma yako ktk uteuzi. Ukweli lawama zote zitakuangukia wewe

Mbowe: Rais, wanaopinga ushiriki wa Taifa kwenye vita ya Corona wanawaza uchaguzi na huruma yako ktk uteuzi. Ukweli lawama zote zitakuangukia wewe

Na hapa ndio kuna tatizo. Viongozi wanatuambia hali ni shwari na wagonjwa wamepungua huko mahospitalini. Hii ni habari nzuri lakini shida inakuja hamna takwimu rasmi ya idadi ya waliopona, waliofariki na rate ya maambukizi imepungua au imeongezeka kwa kiasi gani.
Kwa kweli wametuacha dilemma, halafu wafanya mambo kimya kimya sasa hivi nasikia wanataka kufungua mashule.

Hapo ndio unashindwa hata kuelewa.
 
Raia wa aina yako ndio laana ya nchi hii. Unaambiwa kuna tume inachunguza. Imemaliza kazi yake halafu unakuja kumshutumu mtu anayetaka tu kufahamu mambo yaliyojulikana! Unadhani utawahi kuhoji matumizi ya kodi unayolipa??

Umeambiwa vipimo ni feki. Ripoti ya tume ingeonesha ukweli au uongo wa hilo na tukajua kipi kinaendelea baada ya hapo. Toka tangazo la vipimo feki hata takwimu hakuna kwa sababu maabara ilifungwa kwa maelezo ya Ummy kuwa inafanyiwa ukarabati na wakati huo huo uchunguzi. Kweli kuhoji hili nalo ni jambo baya??

Raia wa hovyo sana wewe!!
Pole kamanda, umekurupuka kujibu bila kuelewa swali. Kuna baadhi ya watu wanatabia wa kujitungia maswali yao wanapoona maswali waliyopewa hawawezi kuyajibu, nafikiri wewe ni mmoja wapo?
 
Kukariri kubaya sana! Jifunzeni kujikubali,.....Kwani WaTanzania tumezuiwa kutumia Akili zetu kupambana na corona....kwani mpaka tutumie njia za mabeberu?? Hii ni vita...kila mtu na mbinu zake.
 
Mbowe mbona hatupi takwimu za Corona za ukoo wake wa Mbowe za idadi ya waliopimwa,waliougua,waliopona, waliofariki na rate ya maambukizi imepungua au imeongezeka kwa kiasi gani ? Hizo hazihitaji serikali ni yeye tu kuzitoa
Tunaziomba ili tuone jinsi hili janga lilivyo kubwa kwenye ukoo wake

Ukoo wake unaficha? mbona hatupi hizo takwimu hata siku moja tunaomba awe anatupa takwimu za kila siku
Mbowe ni wizara ya afya? Kwamba ana vipimo na utaalamu kuhusu Covid_19?
Ni sheria ipi inasema kwamba mwenye wajibu wa kukusanya takwimu za hili gonjwa ni mwananchi wa kawaida au mwanasiasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi tutakapo kufa kwa hayo maelfu wewe utafaidi nini?? Autuseme weye hutakufa? Zidi kuombea wenzio vifo ila na weye utakufa tu. Kumbuka hata kama upo nchi za nje, hakuna mahali corona haijafika hivyo usijione salama sana huko. Tunataka kusikia habari njema tena hizi za kufa kufa tu zimetuchosha.
We jamaa unafikiri kwa kutumia nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo sio RAIA kuwa na nani Bali ni kuwa wako sahihi na wanakoelekezwa? Rais anasema ugonjwa unaisha, lakini madereva wetu kwa idadi kubwa wakifika mipakani wanagundulika wagonjwa kwa nini?
Na hao wote wanatoka kwenye jamii huku mitaani ambako hatupimwi!
US embassy wameonya RAIA wao kuwa hali ya Dar inatisha, nchi jirani wanafunga mipaka bado hatuamini, lakini tunamuamini Magufuli tokea huko mafichoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli hatupimwi,je Rais asinge sema mwanae aliugua ungejua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Akizungumza na taifa Leo hii, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema na kiongozi wa upinzani bungeni Mheshimiwa Freeman Mbowe amemfafanua vizuri Spika wa Bunge kuwa ni MTU wa aina gani.
Akizungumza kwa upole mkubwa, unyenyekevu na weledi wa hali ya juu ameeleza vituko na udhalilishaji ufanywao na Ndugai kama vile gubu la ukewenza.
Hakika Mbowe utulivu usio na chuki umewashangaza wengi kwani utadhani hakuna jambo baya hata moja kesha wahi kutendewa yeye na chama chake.
Tupende tukatae, Mbowe ni kiongozi. Tena kiongozi adimu kupata kutokea katika zama hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asiyejua thamani ya maisha yake, ama ni kichaa au amechanganyikiwa. Mbowe anawaona WaTz ni watu wa aina hiyo. Yawezekana ndicho kilichomsukums kutoa amri kwa Wabunge wa CHAMA CHAKE wajifungie kwa siku 14 ati kujiridhisha hawana maambukizi. Walipomaliza hicho kifungo wamerudi bungeni kuungana na wabunge ambao hawakujifungia na kama wana maambukizi, kifungo chao kitakuwa hakina maana. Mh. Spika amekuwa akirejea maamuzi ya hovyo hayo, kuwakumbusha. Mbowe, badala ya kujibu hoja za Spika, anatumia nguvu sana kuzungumzia badala ya kujikita na hoja zenye maslahi mapana ya kitaifa.

Tujiulize, Mitaani kuna ombaomba, ambao hawavai barakoa wala kutakasa mikono yao, je, wamekufa wangapi? Maeneo ya wakazi wengi maisha yaendelea, wamekufa wangapi?

Ni kweli COVID-19 ipo na ni gonjwa la hatari. Kupambana na gonjwa hili si jukumu la Serikali peke yake, kama ambavyo Mbowe anataka jamii iamini, ila ni la kila mmoja wetu:

Mkuu wa kaya aweke mazingira salama ya kujikinga dhidi ya maambukizi, kwa familia yake, kabla na baada ya maambukizi.

Mwajiri naye aweke mazingira ya kinga dhidi ya wafanyakazi na wateja wake.

Wanafamilia, wafanyakazi na wateja wazingatie kanuni na taratibu, za kujikinga dhidi ya maambukizi, zilizowekwa kwenye maeneo yao.

JIKINGE UMKINGE JIRANI

JILINDE UWALINDE UWAPENDAO
 
Magufuli kusikia tu Mhe, Mbowe ataongea leo., Limekurupuka huko lilikojifisha ili mradi tu. linajiongeresha kanisani huko.
Tofauti ni kwamba Mbowe ameongea maneno yale yale ambayo hata mtoto wa drs la saba angeongea ila Magu babalao ameongea maneno mapya yanayohitajika hapa duniani.
 
Bado namtafakari anayeiongoza hii nchi. Hivi hizi aibu tunazificha wapi lakini? Anakejeli vipimo waavyofanyiwa madereva kwa kusema wanaendesha magari maelfu ya Kilometa, mbona hawaanguki kwenye usukani! Kabisa, Rais wa nchi? Kwamba hajui kuhusu contamination njiani? Tulipatikana!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tukubali madereva wanapata maambukizi njiani, je, mna takwimu za maambukizi au vifo kwenye maeneo ya vituo vya magari hayo?

Mtasema ni wajibu wa Serikali kutoa takwimu wakati taarifa za vifo zinaweza kupatikana kwenye mashina ya chama, kama yapo maeneo hayo, maana kifo cha binadamu hakifichiki.

Kwa kuwa hamjui kama hamjui, kila asemalo Mbowe ni neno takatifu kama la Biblia au Korani.
 
Utaratibu gn ndugu saiv kariakoo hata barakoa watu hawavai wanajua corona imeisha lakini wakati huohuo katika mpk wa zambia na holili madereva wengi toka tanzania wanatest +ve huoni kuna kitu hakiko sawa ila kinafanywa kionekane ni normal
Dah.. Braza....unahakika hivyo vipimo havijachakachuliwa kwa sababu maalum... sometimes tutumie akili kidogo tu [emoji41]

Sent using Beretta ARX 160
 
Tatizo sio RAIA kuwa na nani Bali ni kuwa wako sahihi na wanakoelekezwa? Rais anasema ugonjwa unaisha, lakini madereva wetu kwa idadi kubwa wakifika mipakani wanagundulika wagonjwa kwa nini?
Na hao wote wanatoka kwenye jamii huku mitaani ambako hatupimwi!
US embassy wameonya RAIA wao kuwa hali ya Dar inatisha, nchi jirani wanafunga mipaka bado hatuamini, lakini tunamuamini Magufuli tokea huko mafichoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
Narudia mara kwa mara, tunapenda kusikia takwimu za maambukizi na vifo kutokana na COVID-19 kutoka Serikalini, lakini humu JF, kama wewe, husemi idadi ya walioambukizwa au vifo nyumbani kwako, jirani, mtaani, rafiki au ndugu zako? Hayo maambukizi na vifo viko wapi?
 
Mbowe amejivua nguo leo

Watu Tunakaribia kuishinda corona yeye analeta habari za classmates na spika

Huyu Mbowe bure kabisa
FB_IMG_1589397986327.jpg
 
Huo uwongo wadanganye ufipa

Rais Magufuli ni nahodha bora ametuvusha salama kwenye corona
 
Tukubali madereva wanapata maambukizi njiani, je, mna takwimu za maambukizi au vifo kwenye maeneo ya vituo vya magari hayo?

Mtasema ni wajibu wa Serikali kutoa takwimu wakati taarifa za vifo zinaweza kupatikana kwenye mashina ya chama, kama yapo maeneo hayo, maana kifo cha binadamu hakifichiki.

Kwa kuwa hamjui kama hamjui, kila asemalo Mbowe ni neno takatifu kama la Biblia au Korani.
Kama sayansi ya instruments imemshinda ni yeye tu!!

Hivi unawezaje kusema kifaa kinatoa majibu positive tu, Je kifaa akiwezi kutoa jibu negative?

Kwangu kichwa sio mfuko wa kubebea meno, kwangu awe Mbowe,lissu,mnyika,n.k pia na Rais siwezi kuwa mjinga mbele yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom