Mbowe tafadhali tembelea kituo cha Karantini Horohoro Tanga na ikikupendeza wachangie chakula



Hi thread yako utarudi tu siku moja uanze kusema yaliopita si ndwele. Baada ya kigeu geu Wako a.k.a jiwe kutangaza lockdown.
 
Huku mbunge ni nani? Meya/ mwenyekiti wa halmashauri ni nani na wa wachama gani.

DC ni kutoka chama gani? DED ni chama gani na ameteuliwa na nani?

Watendaji kata na wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji ni wa chama gani?

Rais ni wa chama gani...


Vile maendeleo hayana vyama, mh lusinde ama msukuma tusaidieni kutatua changamoto maana chedema,nccr,caf,act wote wameshindwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja ya nani anakusanya kodi inapendwa sana na upinzani kuliko kuhoji matumizi ya fedha za ruzuku na mfuko wa jimbo, kulikoni?

Chama changu pendwa CCM kina hati chafu, hiyo tunayoiita SACCOS ina hati safi!!

Mbowe ni genious, ni kiongozi, ni baba kwelikweli...ningeweza kukushawishi Mbowe ningekuleta CCM. Ila hili haliwezekani, huko upinzani ulipo panakufaa kutufungua macho
 
Hivi hiyo style ya lockdown si itasababisha maambukizi kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa waliopo hapo karantini?
 
Hoja ya nani anakusanya kodi inapendwa sana na upinzani kuliko kuhoji matumizi ya fedha za ruzuku na mfuko wa jimbo, kulikoni?
Ruzuku na mfuko wa Jimbo Sawa kabisa lakini huko wanapolia ni Jimbo la ccm au ulitaka mfuko wa Jimbo la Hai na Ruzuku ya Chadema ndio ikawasaidie huko, wakati chama Cha mapinduzi kinapata Ruzuku zaidi na kina vitega uchumi vingi!!..
 
Duh

Kuwalipisha 140K kwa wiki 2 ni wizi! Nikiamua kugonga wali nyama kwa wiki 2 mfululizo gharama zitakuwa hivi:-
1. Mchele kwa siku 1/2 kilo, kwa siku 14 = 7kg@Sh 2000 =14,000

2. Nyama kwa siku 1/4 kilo, kwa siku 14 =3.5kgx7000= 24,500
3. Nyanya + vitunguu kwa siku = Sh 1000x14= 14000
4. Mkaa kiroba kimoja =10K
5. Mafuta ya kupikia +chumvi =5000

Total=67,500

140, 000 - 67500 =72500

Yaani Serikali ya CCM mnataka kuibia Wananchi Maskini Sh. 72,500 kwa kisingizio cha karantine?! Yaani wakati wenzenu wanaangalia wawasaidie vp wananchi wao maskini ktk kipindi hiki kigumu, nyie ndo kwanza mnataka kuwapiga!!

Hivi nyie jamaa mmerogwa na nani nyie watu?!
 
Mbowe ana hamu tena ya karantini?
 
Kwanini usianze wewe kuwachangia? Mbowe mwenyewe anangoja michango na ruzuku za chadema aendeshe mambo yake.
 
Ingelikuwa vyema endapo ungeliwaambia wanaJF hao wanaolalamika ni raia wa nchi gani.
Yani watu watoke Kenya halafu waingie Tanganyika kwa njia za panya kukwepa Karantini walikuwa wanategemea nini? Wanataka watusambazie ugonjwa kwa haraka?.
Lazima wanyooshwe wakitaka warudi kwao Kenya.
 
Taarifa yako imekaa kinafiki, we mtoa mada umeanza mazoe yakijinga yakumuona Mbowe kama demu wako.
Hii taarifa yako ndiyo haswa ya kinafiki. Mbowe ni kiongozi wa upinzani na kiongozi wa nchi mtarajiwa. Anayo haki yakufanya hivyo, na zaidi ya hayo kama kiongozi wa upinzani na kiongozi mtarajiwa, ni mtu wa wananchi wote na sip wako au wa chadema tuu, wananchi wanayo hali ya kutikuza na kumshutumu akoseapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka kumhitaji Mbowe kuchangia vyakula, ina maana hatuna Serikali? Serikali ipo kwaajili ya nini kama siyo kutoa huduma wakati wa majanga kama haya?

Hawa wananchi katika maisha yao, karibia kila siku waliichangia Serikali, na Serikali ilikusanya michango yao kwa jina la kodi, leo Serikali inashindwa kurudisha sehemu ya fedha iliyokusanya toka kwao?

Serikali ni kama Shirika kubwa la bima. Inachukua michango toka kwetuwanachama wake ili itoe huduma kwetu wachangiaji zinapohitajika. Leo huduma tunayoihitaji ni ulinzi wa uhai na afya zetu. Isikwepe wajibu. Huyo Mbowe huwa anachukua michango toka kwa nani?

Hili pia, kama Taifa, ni funzo kwetu. Kila kidogo kinachopatikana, tunakimbilia kutumia mpaka senti ya mwisho bila ya kufikiria kuwa kuna milipuko ya magonjwa, majanga ya kiasili kama mafuriko na matetemeko, ukame unaoweza kusababisha upungufu wa chakula, n.k.
 
Hoja ya nani anakusanya kodi inapendwa sana na upinzani kuliko kuhoji matumizi ya fedha za ruzuku na mfuko wa jimbo, kulikoni?

Fedha za mfuko wa jimbo ni 35m@month, unahoji nini kama wananchi wa eneo husika wanamahitaji ya 5b? Kama uko kwenye jimbo lolote la upinzani, nenda kwenye halmashauri husika utapewa matumizi ya mfuko wa jimbo husika. Una jingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…