PostGE2025 Mbowe: Taifa lina maumivu makubwa. Nisiposema haya nitakuwa mnafiki au 'Mswahili'

PostGE2025 Mbowe: Taifa lina maumivu makubwa. Nisiposema haya nitakuwa mnafiki au 'Mswahili'

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema kuwa taifa bado lina maumivu makubwa, akibainisha kuwa wapo watu walioko magerezani ambao wanastahili kula matunda ya nchi yao pamoja na Watanzania wenzao.

Ameyasema hayo leo wakati wa msiba wa Mzee Mtei unaofanyika Tengeru, mkoani Arusha.
 
Mbowe anaibukia kwenye msiba kuyasema haya wakati yakiwepo kwa zaidi ya mwaka?.....

Tukisema anaunga mkono maridhiano yanayopigiwa debe na CCM na yule mzee wa hovyo tutakuwa tumekosea na kustahili kupotezwa au kupewa kesi ya uhaini? 🤔
 
Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema kuwa taifa bado lina maumivu makubwa, akibainisha kuwa wapo watu walioko magerezani ambao wanastahili kula matunda ya nchi yao pamoja na Watanzania wenzao.

Ameyasema hayo leo wakati wa msiba wa Mzee Mtei unaofanyika Tengeru, mkoani Arusha.
Nawasihi wana Jfs mkomment kwa akili
 
Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema kuwa taifa bado lina maumivu makubwa, akibainisha kuwa wapo watu walioko magerezani ambao wanastahili kula matunda ya nchi yao pamoja na Watanzania wenzao.

Ameyasema hayo leo wakati wa msiba wa Mzee Mtei unaofanyika Tengeru, mkoani Arusha.
Mzee wa magloves kwenye ubora wake 🙌🏿🙌🏿
 
Mbowe anaibukia kwenye msiba kuyasema haya wakati yakiwepo kwa zaidi ya mwaka?.....

Tukisema anaunga mkono maridhiano yanayopigiwa debe na CCM na yule mzee wa hovyo tutakuwa tumekosea na kustahili kupotezwa au kupewa kesi ya uhaini? [emoji848]
Hata ufanyeje, binadamu hata ridhika!
 
Mswahili kibongo bongo tunatumia kama ni mtu magumashi ajanyooka kona kona nyingi.

Halihusiani kabisa neno kiswahili.

Ndiyo nakwambia hivyo mnavyotumia ni makosa. Na ninategemea wahuni wakiwa kijiweni waseme hivyo, lakini si Mbowe kwenye msiba wa Mtei.

Mbowe should know better.


Hakuna namna ya kutolihusisha neno Mswahili na Kiswahili.

Koswahiki ni lugha ya Mswahili.

Mswahili ni mtu wa Pwani ya Afrika ya Mashariki.

Kuna utamaduni mkubwa na wenye mambo mengi mazuri kwa Waswahili.

Mpaka hiyo lugha aliyotumia Mbowe ni ya Waswahili. Mbowe ni Mchaga wa Machame lakini hakutumia Kichaga hapo kuongea, katumia Kiswahili.

Mbowe amejionesha kuwa ni mtu mjinga sana mwenye mawazo ya kizamani ya ubaguzi wa kikabila na kiutamaduni. Ameweka kasumba ya kuwaweka Waswahili wote kwenye kapu moja, kwamba Uswahiki ni sawa na unafiki.

Ametia doa msiba wa Mzee Mtei, baba mkwe wake, sehemu ambapo alitegemewa kuongea kwa heshima, kaongea kama mubuni yupo kijiweni tu.

Unafiki ni tabia ya mtu, kuna Wachaga wanafiki, kuna Waingereza wanafiki, kuna Wachina wanafiki.

Mbowe amejionesha kuwa liicha ya kukaa mjini siku nyingi na kuwa mwanasiasa mkubwa bado ni mshamba tu.
 
Back
Top Bottom