Pre GE2025 Mbowe: Uchaguzi wa kwanza Lissu akiwa CHADEMA nilimpa gari yangu akafanyie kampeni. Nyumba ya Dodoma nilipewa na Serikali, nikampa yeye

Pre GE2025 Mbowe: Uchaguzi wa kwanza Lissu akiwa CHADEMA nilimpa gari yangu akafanyie kampeni. Nyumba ya Dodoma nilipewa na Serikali, nikampa yeye

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lissu ana damu ya usaliti ukiangalia wema aliofanyiwa na Mbowe huwezi kutegemea angemkgeuka na kumtusi namna hii kisa madaraka.

Lissu wakati unafundishwa siasa hao kina Maria Sarungi walikuwa wapi?

Wakati unapewa nauli za ndege naembowe ukuwe kisiasa hao diaspora walikuwa wapi?

Wakati umepigwa risasi nani alikuepusha kwenda muhimbili kama sio Mbowe?

Lissu ni msaliti na hafai kuongoza taifa kama Tanzania wala chama kama chadema.

Kwa akili yako, Lissu kugombea uenyekiti ni usaliti?
 
Lissu ana damu ya usaliti ukiangalia wema aliofanyiwa na Mbowe huwezi kutegemea angemkgeuka na kumtusi namna hii kisa madaraka.

Lissu wakati unafundishwa siasa hao kina Maria Sarungi walikuwa wapi?

Wakati unapewa nauli za ndege naembowe ukuwe kisiasa hao diaspora walikuwa wapi?

Wakati umepigwa risasi nani alikuepusha kwenda muhimbili kama sio Mbowe?

Lissu ni msaliti na hafai kuongoza taifa kama Tanzania wala chama kama chadema.
Huo wema kumbe ilikuwa rushwa?
 
Mbowe kupitia Crown FM anasema kwenye uchaguzi wa kwanza Lissu akiwa CHADEMA Mbowe alimpa gari yake binafsi ili akafanyie kampeni. Pia anasema Nyumba aliyokuwa akiishi Lissu pale Dodoma ilikuwa yake aliyopewa na Serikali Ila akamuachia Lissu aishi yeye Mbowe akaenda kupanga.

View attachment 3194386
Hizi Habari za kitoto
So what
Lisu asigombee uwenyekiti

Kwa Nini mbowe asijitoe ameachie lissu
 
Inatosha, ni wakati wa kuondoka kwenye jukwaa, hata ucheze vizuri namna gani, ukifika wakati unamuachia na mwenzako aonyeshe mambo yake.

Katiba haina kipengele cha kuachiana bali kugombea na kushinda nafasi uitakayo. Hiyo ndiyo CHADEMA.
 
Lissu nae alikubali kufa kwa ajili ya chama, lipo lubwa? Lissu ana risasi mwilini, hayo mbowe anaona ni kidogo?
Kwa hiyo aliulizwa kama yuko tayari kupigwa risasi akakubali? Mbowe amewekwa mahabusu, amekaa rumande na amekaa jela. Yote hayo unaona madogo?

Amandla...
 
Kama hizi ndo tetezi anazotambia FAM dhidi ya TAL .

Kweli ni mkubwa tu wa Umri basi, inamaana Mjomba alomsomesha Mpwa wake, ni lazima Mpwa wake akubalia na Kila jambo la Mjomba?.

Kwan hiyo nyumba na Gari hakuwapa wengine, kwann LISSU?.

Kumbe huyu jamaa naona kwake Mali ni kitu Cha msingi sana maishan mwake,

Kwa mashudu haya, MBOWE NI FISADI KUU.
 
Hiyo nyumba aliyompatia ndio pale lissu aliposhambuliwa!? Manake nakumbuka lissu amewahi kusema kwamba yeye kama mnadhimu Mkuu wa Upinzani alikua pia anastahili kupatiwa nyumba na serikali. Na kama Kweli mbowe alimpatia Nyumba yake aliyopewa na Serikali na lissu akaishi pale for five years, basi naamini hii nchi ina tatizo mahali... hivi Bunge au serikali inawezaje kuacha Mali za umma zitumike kiholela hivyo!? Kumbe ata Makonda pale Arusha anaweza akaamua nyumba yake ya RC amwachie ndugu au rafiki yake aishi na yeye akaenda kukaa kwake njiro na serikali ikaona ni sawa tuu!?... System ya G.O.T itakua ina loopholes nyingi sana.. nahisi kuna mambo mengi yanafanyika nchii hii ya ajabu sana...ukimsikiliza kwa umakini Mbowe ndio utajua hii NCHi ni Ngumu na rahisi sana kwa wakati mmoja.
 
Tatizo ni Uenyekiti tu???
Mbona FAM hoja zake ni dhaifu sana 😀😀😀
 
Back
Top Bottom