Pre GE2025 Mbowe: Uchaguzi wa kwanza Lissu akiwa CHADEMA nilimpa gari yangu akafanyie kampeni. Nyumba ya Dodoma nilipewa na Serikali, nikampa yeye

Pre GE2025 Mbowe: Uchaguzi wa kwanza Lissu akiwa CHADEMA nilimpa gari yangu akafanyie kampeni. Nyumba ya Dodoma nilipewa na Serikali, nikampa yeye

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watoto wadogo na washamba ndio mnamhusisha Mbowe na pesa za Abdul. Kwa taarifa yako Mbowe ni tajiri tangu Mwalimu Nyerere anafundisha Pugu Sekondari! Nini Abdul! Ahahahahaha!!!
Hiyo historia tunaifahamu labda wafundishe watoto wenzako huko CCM.
 
Mbowe kupitia Crown FM anasema kwenye uchaguzi wa kwanza Lissu akiwa CHADEMA Mbowe alimpa gari yake binafsi ili akafanyie kampeni. Pia anasema Nyumba aliyokuwa akiishi Lissu pale Dodoma ilikuwa yake aliyopewa na Serikali Ila akamuachia Lissu aishi yeye Mbowe akaenda kupanga.

View attachment 3194386
Haahaa hizo ndo sera zake za kutaka uongozi? Mbowe akili zimepotelea wapi? Amwage sera asilielie
 
Lissu kumbe hana uungwana kwa kiwango hiki.
 
Lissu ana damu ya usaliti ukiangalia wema aliofanyiwa na Mbowe huwezi kutegemea angemkgeuka na kumtusi namna hii kisa madaraka.

Lissu wakati unafundishwa siasa hao kina Maria Sarungi walikuwa wapi?

Wakati unapewa nauli za ndege naembowe ukuwe kisiasa hao diaspora walikuwa wapi?

Wakati umepigwa risasi nani alikuepusha kwenda muhimbili kama sio Mbowe?

Lissu ni msaliti na hafai kuongoza taifa kama Tanzania wala chama kama chadema.
Hata Lisu akipata huu uongozi utamtesa,alipaswa kuweka akiba ya maneno,leo anasema biashara za Mbowe hazina TIN kumbe alikuwa anatumia magari ya mtu asiye na TIN.Kama anamfanyia hivyo Mbowe wasio na uwezo itakuwaje!!?
 
Ni aibu sana Chama kinachotafuta dola kuongozwa na Disco Joker, tena mlevi, aliefeli form four? These people are not serious!.
Wakati ni ukuta, demokrasia ya ukweli ni kuachiana viti sio kulazimisha kuwa kiongozi, the big boss must go aache kulia lia, aje kijana alete changamoto mpya japo ana ulemavu!!

However, DJ akiweza kung'oka tafadhali mnitag!! Ni ngumu mno. Ni rahisi kijana kupita kwenye tundu la sindano kuliko kushinda hicho kiti cha m/kiti wa maisha wa ukoo. The boss can't let it go kirahisi itakuwa Vita kubwa na figisu kama zote nje na ndani ya uwanja!!

Leo hii Mbowe kama Dj tu na form four failure au sio? hata shukurani mnakosa, ila tafuteni chama cha kwenda CHADEMA sio
 

Attachments

  • IMG-20250107-WA0016.jpg
    IMG-20250107-WA0016.jpg
    142.4 KB · Views: 1
Ni Kama anaweka zuio kistaarabu ili zisije kuvuja zaidi.
Upo sahihi sana ndugu Gautten Potten .
Mbowe anamjua Lissu vyema sana na anajua kuwa Lissu anazo siri zake nyingi sana, na ushahidi juu.

Mbowe anaogopa sana kwamba Lissu anaweza "kuropoka" mambo yake makubwa sana yatakayoishtua Taifa, hivyo anachojaribu ndio hicho cha kumsihi kistaarabu kuwa akumbuke fadhila zake za huko nyuma ili Mbowe asitiriwe.

Naamini Lissu akiwa provoked zaidi na Team FAM, anaweza kuendelea kutumia WMD zake kama ile moja ya "vikao vya siri kwa siku tatu".

Lissu anajua kucheza kete zake vyema na Mbowe analijua hilo, na linamuogopesha sana sana.
 
Hiyo nyumba aliyompatia ndio pale lissu aliposhambuliwa!? Manake nakumbuka lissu amewahi kusema kwamba yeye kama mnadhimu Mkuu wa Upinzani alikua pia anastahili kupatiwa nyumba na serikali. Na kama Kweli mbowe alimpatia Nyumba yake aliyopewa na Serikali na lissu akaishi pale for five years, basi naamini hii nchi ina tatizo mahali... hivi Bunge au serikali inawezaje kuacha Mali za umma zitumike kiholela hivyo!? Kumbe ata Makonda pale Arusha anaweza akaamua nyumba yake ya RC amwachie ndugu au rafiki yake aishi na yeye akaenda kukaa kwake njiro na serikali ikaona ni sawa tuu!?... System ya G.O.T itakua ina loopholes nyingi sana.. nahisi kuna mambo mengi yanafanyika nchii hii ya ajabu sana...ukimsikiliza kwa umakini Mbowe ndio utajua hii NCHi ni Ngumu na rahisi sana kwa wakati mmoja.
Kuna waziri aliwahi kuhonga nyumba ya serikali kwa hawara yake.

Kuna waziri aliwahi gonga gari ya serikali (gari ya waziri) ikiwa na namba binafsi akiwa anaendesha yeye na pembeni amekaa kimada wake.

Tanzania kila kitu kinawezekana.
 
Watoto wadogo na washamba ndio mnamhusisha Mbowe na pesa za Abdul. Kwa taarifa yako Mbowe ni tajiri tangu Mwalimu Nyerere anafundisha Pugu Sekondari! Nini Abdul! Ahahahahaha!!!
Pesa haijawahi kutosha hata siku moja, tena sana sana kwa mwenye fedha nyingi sana.

Ukishakuw tajiri, kila fursa unayoiona na kuipata ya kutengeneza shilingi kumi, utaitumia vyema hiyo fursa, sembuse fursa ya kupata fedha za bure ambazo ni kodi ya Watanzania!!
 
Napata taabu sana kuamini maneno yanayoandikwa kuwa yamesemwa na Mbowe mpaka nipate kuyasikia na kumuona akiyanena hayo, maana nimejiuliza sana FAM yule yule ninayemfahamu ndiye huyu huyu anayeongea haya kweli!!???

Busara zake zimeenda wapi!!??

Ama kweli madaraka hupofusha.
Ama kweli fedha hupofusha.
Ama kweli rushwa hupofusha macho, akili, mwili, roho, nafsi, mdomo,masikio na mwili mzima.

Ndugu yangu kaka Mbowe vipi kuhusu ile Zaburi 1: 1 -6 uliyowahi kuniambia nilipokutambulisha kwa shemeji yangu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa mwaka 2014!!???
 
Back
Top Bottom