Mbowe umesamehewa na Rais, nawe wasamehe Mdee na wenzake 18

Sijaelewa hii kauli ya kukataa matokeo ya uchaguzi kwasababu hayakuwa halali

Mbona yule mbunge mmoja anahudhuria kama kawaida bungeni na hajachukuliwa hatua

Au kulikuwa na chaguzi mbili tofauti.
Akina mbowe walikuwa wanataka hata yule mbunge aliyeshinda jimboni nkasi nae asiende bungeni, hii sio sawa kwakuwa tangu uchaguzi wa 1995 hadi wa 2020 malalamiko ya upinzani ni kuibiwa kura na tume lakini wabunge hawajawahi kuacha kwenda bungeni, labda tofauti pekee kwa uchaguzi wa 2020 ni wanaume wote wakiwemo Mbowe, Sugu, Msigwa, Joseph, nk hawakutangazwa kushinda uchaguzi. Labda hii ndiyo sababu ya chadema kusema hakuna mbunge kwenda bungeni safari hii. Ubinafsi.
 

Mbowe hajasamehewa bali amefutiwa mashtaka. Kusamehewa Ni pale ambapo angekutwa na hatia.
 
Ulis
Ulisikia mama alichosema Jana, hakuna aliyemuumba radhi mwenzake.
 
Huwezi kumtenganisha mama Samia na urais wa nchi hata kama akienda kwenye sherehe ya kitchen party ya rafiki yake. Huwezi kumtenganisha Mbowe na chadema hata kama Yuko gerezani, Hana jambo lake binafsi kama chairperson wa Chama.
 
Mbowe hajasamehewa bali amefutiwa mashtaka. Kusamehewa Ni pale ambapo angekutwa na hatia.
Hizo zote ni mbwembwe TU, Mama amemsamehe Mbowe kwa nguvu zake za kikatiba.
 
Ulis

Ulisikia mama alichosema Jana, hakuna aliyemuumba radhi mwenzake.
Kikubwa ni Mbowe kuwa huru kuungana na watanzania wenzake na familia yake, hizo details hatuna haja nazo sisi. Lakini picha kubwa ni kwamba mama Samia ameruhusu mbowe atoke mahabusu iwe alikatamwa kimakosa au kihalali.
 
C19 wamevuliwa ubunge na wanakula kodi za wananchi bure, halafu wewe wasema wasamehewe..... seriously
Kwani hizo nafasi 19 zingebaki wazi kama wangesusia kwenda bungeni? Pili akina Halima wanalitumikia bunge na michango Yao bungeni tunaisikia wakichangia. Unaposema wanakula Kodi bure inaonekana huna uelewa wa kutosha.
 
Kwa hiyo unaamini Mbowe kasamehewa,na wale waliokutwa na bastora na madawa ya kulevya wamesamehewa kwa malahi mapana? Aaaaaiiiseee ๐Ÿค. Kwa hiyo unaamini wale Makomando walinunuliwa na Kingai chips kuku na energy ya Mo walipokuwa safarini kutoka Moshi kwenda Dar๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
 
Huwezi kumtenganisha mama Samia na urais wa nchi hata kama akienda kwenye sherehe ya kitchen party ya rafiki yake. Huwezi kumtenganisha Mbowe na chadema hata kama Yuko gerezani, Hana jambo lake binafsi kama chairperson wa Chama.
Nimekuwekea maswali 4 makusudi na nilijua ulivyo mbulula utajibu moja tu, umeingia king vizuri kabisa.
 
Kikubwa ni Mbowe kuwa huru kuungana na watanzania wenzake na familia yake, hizo details hatuna haja nazo sisi. Lakini picha kubwa ni kwamba mama Samia ameruhusu mbowe atoke mahabusu iwe alikatamwa kimakosa au kihalali.
Futa sasa kauli yako ya kuwa Mbowe amesamehewa
 
Aaaa bhana tuache ushamba, kwa mwendazake asingetoka. Kwa mama hata wale masheikh wa uamsho waliokaa miaka 8 mahabusu wametoka.
Je ulimusikia Rais? Alikiri kuwa hakuna aliyeomba msamaha.
 
Nina uhakika kuwa hawa jamaa wanataka wake zao, rafiki au ndugu zao wa karibu ndo waende bungeni. Chadema kama tunataka mshikamano na kuonyesha ukubwa na ukomavu na utayari wa Chama kushika dola tuwasamehe hawa wanawake ili tujikite kwenye ajenda mama ya Katiba, tume huru ya uchaguzi na maandalizi ya uchaguzi. Hawa wanawake walikuwa wanapotoshwa na system iliyoongozwa na Bw Ndugai na mamlaka nyingine kubwa.

Narudia tena, tutakosea sana kama tutawafukuza akina Mdee, badala ya kudai ruzuku yetu kama tulikuwa tumeisusia pia.
 
Kwanza Mbowe hajamkosea Rais hadi useme Rais amemsamehe,amsamehe kwa kosa lipi? Pili Halima na genge lake hawakumkosea Mbowe bali walikisaliti chama, hivyo hoja zako ni muflisi,ni propaganda chafu tu za CCM kutaka kuleta hali ya sintofahamu ndani ya Chadema. Please leave us alone.
 
Nadhan kama hawatambui uchaguzi wa 2020 ni vizuri pia hata yule mbunge asitambuliwe pia

Maana kumtambua yule mmoja ni sawa a kukinzana na maneno yao wenyewe juu ya uchaguzi mkuu uliopita

Na hapa ndio ninapoona tofauti ya siasa za Tanzania na nchi zingine waliotuzidi ukomavu wa kisiasa

Huwezi kupinga uchaguzi kwa kukataa wabunge 19 wasiende bungeni ila ukakubali mmoja aende bungeni

Huo utakuwa ni unafiki na kuwapeleka wafuasi wasiojielewa

Kama wamekubali mbunge mmoja aingie bungeni ni sawa na kuukubali uchaguzi wa 2020.
 
Futa sasa kauli yako ya kuwa Mbowe amesamehewa
Sifuti kauli, hata Babu Seya inaaminika kuwa alifungwa kimakosa lakini Rais JPM alimsamehe. Hata Mbowe angeweza kufungwa kimakosa na akaja Rais akamsamehe. Mama kaupiga mwingi Kwenye hili,
 
Kaka kazi ya kwanza waliyonayo chadema ni kuyatambua matokeo ya uchaguzi 2020
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ