Mbowe umesamehewa na Rais, nawe wasamehe Mdee na wenzake 18

Nikajua DPP aliona hawana kesi ya kujibu, kumbe ni Rais ndio kawasamehe!!
 
Ni kama una magonjwa ya akili, hivi kama CHADEMA wangewarubuni na kuyafanya CCM waliyoyafanya kwa wanachama 19 ingechukua hatua gani?
Wote tunakubaliana kuwa mbaya wetu ni tume ya uchaguzi sio Halima Mdee na wenzake 18. Yaliyopita si ndwele tudai tume mpya na katiba mpya. Nikisikia chadema wanawashupalia akina Mdee najisikia homa, ukabila, chuki, na maslahi binafsi
 
Kwani hizo nafasi 19 zingebaki wazi kama wangesusia kwenda bungeni? Pili akina Halima wanalitumikia bunge na michango Yao bungeni tunaisikia wakichangia. Unaposema wanakula Kodi bure inaonekana huna uelewa wa kutosha.
Kuhusu kuona sina uwelewa wakutosha hayo ni maoni yako na huo ndio uhuru wa kujieleza tunaoutaka. Kama umefukuzwa uwanachama ya nini unang'ang'ania ? Siii wamefukuzwa sasa izo posho na mishahara wanazopokea si ndio kula kodi za wananchi
 
tuwe straight, mbowe ametoka mahabusu baada ya rais kuingilia kati...logically huo ni msamaha..maana hakushinda kesi..ndio maana akaenda ikulu kushukuru.
 
Akina mdee wamekikosea chama na sio wamemkosea mbowe. Msamaha wao utatolewa na chama na sio mbowe

Kuwasamehe covid 19 baada ya kuonesha jeuri na dharau kwa chama kutadhoofisha chama irreparably ! Maadui wa Chadema ndio waliosuka mpango wa hao wanawake kukiasi chama; na sasa wanasuka mpango wa kukipasua chama kwa kutaka kutumia watu ili warudi chadema ili wawatumie kama wapelelezi wao ndani ya chama!! LET THE CORONA WOMEN GO!!
 
Sidhani kama Mboye ana hayo mamlaka.Hizo nafasi za akina mdee zilitakiwa kuenda kwa wakina mama wanaokipigania chama
 
Awesomeness kwani wamemkisea Mbowe?

Hata wakisamehewa na Mbowe halafu iweje kuhusu mabwana zao.
 
Nikajua DPP aliona hawana kesi ya kujibu, kumbe ni Rais ndio kawasamehe!!
Mbaada ya kupitia ushahidi wote DPP kasema Mbowe alikuwa na kesi ya kujibu, ni nani kamfanya apige U turn? Wacheni uzuzu, nchi zetu za Afrika hizi hata jaji mkuu na DPP wote ni wateule wa Rais.
 
Wewe ni mfano mzuri wa akili zilizodumaa
Wewe huna akili kabisa Bora yangu imedumaa. Ulikuwa unafurahia Mbowe kuendelea kumkosa mke wake kwa miezi 7 wewe ukiwa uraiani na mkeo. Imekuuma sana Mbowe kuwa nje maana huna agenda tena. Mama Samia ametufilisi kwa kumuachia Mbowe, hata mabeberu wameishiwa hoja wanabaki kumwaga misaada iliyokuwa imesimamishwa.

Mbowe kasamehewa hata kama tukitumia lugha zilizonakshiwa.
 
Jana nilikuwa naangalia mahojiano ya Samia na Kikeke BBC, Samia kakiri binafsi yeye kwa kinywa chake kwamba kwenye sakata la Mbowe hakuna aliyemwomba mwenzake msamaha.
Lugha ya kiutu uzima hiyo,amekubali kutokukubaliana.
 
Kuhusu kuona sina uwelewa wakutosha hayo ni maoni yako na huo ndio uhuru wa kujieleza tunaoutaka. Kama umefukuzwa uwanachama ya nini unang'ang'ania ? Siii wamefukuzwa sasa izo posho na mishahara wanazopokea si ndio kula kodi za wananchi
Wanefukuzwa na nani mbona wanachapa kazi mjengoni na kulipwa sawa kazi Yao? Hawa wako kwenye kamati mbalimbali za bunge, wanahudhuria na kuchangia pia. Kaka mnyinge mnyongeni lakini
 
Hayo ni mawazo yako, chadema Kuna Siri gani ya kupeleleza? Chama kikubwa kama chadema kinachojiandaa kushika dola hakiwezi kukumbatia wanaofikiria kama wewe . Chadema walikuwepo hata akina Lowassa, Sumaye, zitto, mwigamba, kingunge na wengi TU wakarudi CCM, kama ni Siri basi zimejulikaba tayari.

Mbowe kasamehewa kwanini iwe dhambi kuwasamehe wanawake?
 
Embu elezea Hapo kwenye IPOTEEE AU ICHUKULIWE NA CCM !!!?? Humor kichwani itakuwa na makamasi mengi sana..... CCM anachukuaje matokeo ya kura za urais za chadema Ili apeleke hao wanawake wake kuwa viti maalum !!!?? Ila wajinga ni wengi.. na ndio mtaji wa CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…