Lissu alikua kakaa sehemu nzuri ya kushinda au siku moja kuongoza CDM au hata TAIFA.Lkn kwa jinsi wapambe walivyomuingiza mkenge hawezi ataleta mpasuko.
Staili yake ya sasa ya kujifanya utafikiri yeye sio sehemu ya CHADEMA, kwamba yaliyokuwa yanafanyika humo yeye hayajui. Hasemi kwa mafasi yake alifanya nini kama kiongozi katika kurekebisha au kujaribu kuweka mambo sawa NA HAPO NDO ANGETOKEA.Lkn sio yeye ndo system yenyewe ya Chadema, kiongozi wa kamati ya maadili halafu hachukui hatua abasubiri kuja kusema majukwaani.
Hakuna mtu, taifa, chama, kampuni ambayo haina matatizo au hakuna kiongozi na mtu yoyote duniani hapa kanyooka kama ruler.
Lissu ni opportunitic, mbinafsi na msaliti - HATUWEZI kuwa na Rais kama huyu..atakuwa anakataa accountability ya vyombo vyake kwa kukaa pembeni na kujifanya yeye msafi.
Huwezi leo hii ukamsikia Mama Samia anakaa 24 hrs akilinanga jeshi la polisi - sababu yeye ni sehemu - anahusika nalo - kulisema as if alimuhusu ni ukichaa..anachoweza kufanya ni kujitahidi kurekebisha na hata akisema anasema kwa hekima na tahadhari - NDIO UONGOZI HUO.
Huwezi ukamsikia Trump au kiongozi yoyote wa kitaifa wa US akilisena jeshi lao licha ya shutuma kibao.
Huwezi ukamskia Netanyahu anawasema wanayeshi wake na kuwakandia mwanzo mwisho licha ta mauaji wanayofanya gaza.
Huwezi ukamsikia Dr.Nchimbi akimsema mwenyekiti wake au viongozi wenzake...hadharani..au unafikiri. CCM wamenyooka.
Nape,Kinana & Makamba walikuwa wanamsema JPM privately - sirini, isingekuwa kuingiliwa kwenye privacy yao watu baki wasingejua..lkn walikua na uwezo wa kuandika mapungufu yake mitandaoni etc...na ingekuwa na impact kubwa na hatari zaidi.
Hatuwasemi watoto wetu, wanafamilia wetu, wake zetu hadharani hata kama kuna ugomvi au mapungufu kiasi gani.
Lissu kwa hichi alichofanya kachemsha na hata akishinda atapasua chama..Huwezi kuwa commander in chief unapata taarifa zote kuhusu watu, mapungufu etc..then uwe na kifua chepesi ah fridge lako haligandishi - Kwanza utasumbua watu pili utakufa kwa presha na kihoro.