Mbowe: Wabunge wamejiongezea Mishahara Kutoka Tsh milioni 13 za awali na sasa wanalipwa Tsh milioni 18 kwa mwezi mbali na posho

Mbowe: Wabunge wamejiongezea Mishahara Kutoka Tsh milioni 13 za awali na sasa wanalipwa Tsh milioni 18 kwa mwezi mbali na posho

Mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe amesema Wabunge wa Bunge la JMT wamejiongezea Mishahara kutoka TSH 13 million walizokuwa wanalipwa awali hadi TSH 18 million

Mbowe amesema mshahara huo ni mbali na Posho mbalimbali wanazolipwa kila Siku

Jumaa Mubarak 😀🔥


----
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe amedai kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejiongezea mishahara yao kutoka milioni 13 waliyokuwa wanapata hapo awali hadi kufikia milioni 18 kwa mwezi, hiyo ikiwa ni nje ya posho ya vikao anayopatiwa Mbunge kila anapohudhuria kikao kimoja cha Bunge

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Machi 21.2024 Babati mjini, mkoani Manyara Mbowe amesema kuwa mara nyingi viongozi wa serikali wamekuwa wakijitokeza hadharani na kueleza kuwa uchumi umekua hapa nchini, jambo ambalo anakubaliananalo kwa kutumia kipimo cha pato la Taifa (GDP) lakini ameeleza kuwa uchumi huo umekua kwa watu wachache walioko serikalini na sio kwa mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla wake

Amesema viongozi walioko serikalini wamekuwa wakiendekeza maisha ya anasa ambayo kwa kiasi kikubwa hayaangalii maslahi ya nchi na wananchi wake ndio maana inawawia vigumu kukubali kufanya marekebisho ya msingi ya sheria za nchi kutokana na msingi wa uwepo wa Katiba mpya

Ametolea mfano kupitishwa kwa sheria ya mafao ya wenza wa viongozi kama sehemu ya anasa hizo kwa kuwa sasa mwenza wa Rais mstaafu analazimika kupokea asilimia 60 ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani, wakati Rais mstaafu akipokea asilimia 80 ya mshahara huo, hiyo ikienda sambamba na kupatiwa magari yanayobadilishwa kila baada ya muda, walinzi, nyumba na watumishi wengine binafsi.

Chanzo: Jambo Tv

Hapo usifikiri anayesema wanalipwa mihela anachukizwa na ulafi, bali anawaonea wivu na gele wenzie. Tanzania hakuna mtu anayechukia ulafi, badala yake wanaonea wivu.
 
Acha ujinga basi. Kwa hiyo wewe wabunge wanapojirundikia mishahara minene huku wananchi wakifa njaa kwa umasikini wewe unaaona sawa tu?
Wewe mpumbavu siungi mkono hata kuwa na bunge kabisa kwasababu kwa nyakati hizi za digitali unaweza kujua changamoto iliyopo Tandahimba ukiwa zako Nyamagana. Na kama hoja ni kutunga sheria ni kuwa hakuna mbunge anayetunga sheria.. mtu aliyemaliza darasa la 7 anatunga sheria kivipi? NILICHOPINGA ni huo UNAFIKI wa mwenyekiti wa nyumbu kujifanya ana uchungu na mishahara ya wabunge wakati kipindi yuko bungeni hakuwahi kukataa kuongezewa mshahara. Kina Lema ndo hao huchukua mikopo ya mabilioni kupitia mshahara wa bunge. SIKU NYINGINE TUMIA AKILI KABLA YA KUNIPINGA KIPUUZI.
 
Naunga mkono Serikali kuongezea watumishi mishahara wamekaa miaka sita bila nyongeza, wasiishie kwa wabunge tu watumishi wote wakumbukwe wamekaa muda bila nyongeza wala kupanda madaraja.
 
Hivi walivyojiongezea mpaka hio 10 walitwambia wapi ? Kwahio upuuzi huu sio mpya ni muendelezo wa tu upigaji
 
Nazani umeona wabunge wa uingereza walivyonamsimamo hata kama ni kama ni kiongozi wa Chama ukienda tofauti na malengo wanaacha kukuunga mkono sababu ya shinikizo kutoka kwa wananchi wao viongozi wanaamua kujiuzuru
Washafika hatua ya juu ya ustaarabu ila kwetu kuwajibishana tu nitatizo ndio tunavuna tulichopanda
 
Ni kwa sababu ya mfumuko wa bei lazima mshahara uongezeke🐼
 
Back
Top Bottom