Earthmover
JF-Expert Member
- Sep 28, 2012
- 24,977
- 23,799
Hao na Walimu wako fofofoo ni mapambio tu...Vyama vya wafanyakazi angalie nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao na Walimu wako fofofoo ni mapambio tu...Vyama vya wafanyakazi angalie nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma.
Wabunge walihongwa nyongeza ya mishahara ili kupitisha mkataba wa DP World.
Mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe amesema Wabunge wa Bunge la JMT wamejiongezea Mishahara kutoka TSH 13 million walizokuwa wanalipwa awali hadi TSH 18 million
Mbowe amesema mshahara huo ni mbali na Posho mbalimbali wanazolipwa kila Siku
Jumaa Mubarak 😀🔥
----
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe amedai kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejiongezea mishahara yao kutoka milioni 13 waliyokuwa wanapata hapo awali hadi kufikia milioni 18 kwa mwezi, hiyo ikiwa ni nje ya posho ya vikao anayopatiwa Mbunge kila anapohudhuria kikao kimoja cha Bunge
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Machi 21.2024 Babati mjini, mkoani Manyara Mbowe amesema kuwa mara nyingi viongozi wa serikali wamekuwa wakijitokeza hadharani na kueleza kuwa uchumi umekua hapa nchini, jambo ambalo anakubaliananalo kwa kutumia kipimo cha pato la Taifa (GDP) lakini ameeleza kuwa uchumi huo umekua kwa watu wachache walioko serikalini na sio kwa mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla wake
Amesema viongozi walioko serikalini wamekuwa wakiendekeza maisha ya anasa ambayo kwa kiasi kikubwa hayaangalii maslahi ya nchi na wananchi wake ndio maana inawawia vigumu kukubali kufanya marekebisho ya msingi ya sheria za nchi kutokana na msingi wa uwepo wa Katiba mpya
Ametolea mfano kupitishwa kwa sheria ya mafao ya wenza wa viongozi kama sehemu ya anasa hizo kwa kuwa sasa mwenza wa Rais mstaafu analazimika kupokea asilimia 60 ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani, wakati Rais mstaafu akipokea asilimia 80 ya mshahara huo, hiyo ikienda sambamba na kupatiwa magari yanayobadilishwa kila baada ya muda, walinzi, nyumba na watumishi wengine binafsi.
Chanzo: Jambo Tv
Wewe endelea kuamini hivyo lkn ujumbe umeshafika kwa Wapiga Kura.Hapo usifikiri anayesema wanalipya mihela anachukizwa na ulafi, bali anawaonea wivu na gele wenzie. Tanzania hakuna mtu anayechukia ulafi, badala yake wanaonea wivu.
Wewe mpumbavu siungi mkono hata kuwa na bunge kabisa kwasababu kwa nyakati hizi za digitali unaweza kujua changamoto iliyopo Tandahimba ukiwa zako Nyamagana. Na kama hoja ni kutunga sheria ni kuwa hakuna mbunge anayetunga sheria.. mtu aliyemaliza darasa la 7 anatunga sheria kivipi? NILICHOPINGA ni huo UNAFIKI wa mwenyekiti wa nyumbu kujifanya ana uchungu na mishahara ya wabunge wakati kipindi yuko bungeni hakuwahi kukataa kuongezewa mshahara. Kina Lema ndo hao huchukua mikopo ya mabilioni kupitia mshahara wa bunge. SIKU NYINGINE TUMIA AKILI KABLA YA KUNIPINGA KIPUUZI.Acha ujinga basi. Kwa hiyo wewe wabunge wanapojirundikia mishahara minene huku wananchi wakifa njaa kwa umasikini wewe unaaona sawa tu?
Yule jamaa wa tucta alivyo muoga..sidhani kama wataibua hii ishu.Vyama vya wafanyakazi angalie nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma.
Kalale kama umechokaMsituchanganye bhana kipindi nyie mpo bungeni na posho zikaongezwa kwa fujo mbona hatikuwasikia mkilalamika?
CCM ni majangili tupuHii nchi itakuwa imefikia uchumi wa juu kwa pembeni,sisi wa upande huu ndiyo hatujui tu,kumbe ni muda wa kutafuna kilichoandaliwa.
Jamaa wapo busy kuiba na kupiga pesandiyo mana wanapigana kufa na kupona na kurogana ili kuendelea kuwa wabunge, na pale wanaposhindwa huwa wanakufa haraka sana kwa kihoro.
Washafika hatua ya juu ya ustaarabu ila kwetu kuwajibishana tu nitatizo ndio tunavuna tulichopandaNazani umeona wabunge wa uingereza walivyonamsimamo hata kama ni kama ni kiongozi wa Chama ukienda tofauti na malengo wanaacha kukuunga mkono sababu ya shinikizo kutoka kwa wananchi wao viongozi wanaamua kujiuzuru
Kosa moja halihalalishi jingine kwa wenye akili.Msituchanganye bhana kipindi nyie mpo bungeni na posho zikaongezwa kwa fujo mbona hatikuwasikia mkilalamika?
😆😆😆😆😆😆Ndiyo maana Kuna jamaa angu ameandika barua ya kuacha kazi ili akagombee kwao mwakani 2025
Mafara sana hao ila wakiumwa kutwa kuomba msaaada kwa serikari na kwa wanainch hovyo sana pesa wanafanyia anasaPension yao itakuwa 0.4 x 12 x 5 x 18,000,000=432,000,000/=